2021
Husisha
Machi 2021


“Husisha,” Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2021, ndani ya jalada la mbele.

Husisha

Liah T.

16, Louisiana, Marekani

Picha
msichana akichora

Muziki ni sehemu kubwa ya maisha yangu. Ninapenda kucheza viola na fidla. Nilipokuwa mdogo, mama yangu aliitwa kufundisha muziki katika Msingi. Alinifunza kupenda nyimbo zilizo kwenye Kitabu cha Nyimbo za Watoto, na mimi huhisi Roho kila wakati ninapozipiga.

Mimi pia ni mcheza dansi kwenye kikundi cha Louisiana Vintage Dancers na huchora michoro ya sanaa kwa ajili ya wazazi wangu na nyumbani kwangu. Ninawashukuru na ninawathamini watu wanaotenga muda wao kuchora michoro tunayoiona kanisani. Ninaichukulia kuwa jambo la kuvutia kuwa uchoraji ni njia moja zaidi ambayo watu wanaweza kutumia kuonyesha hisia zao kuhusu injili.

Kwenye mkutano mkuu wa Oktoba 2018, Mzee Gerrit W. Gong wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alirejelea mchoro unaoonyesha jua likichwea nyuma ya msitu. Ulikuwa wa kupendeza! Mchoro huo ulinikumbusha kuwa jua siku zote huchomoza baada ya usiku wa giza.

Injili ni maisha yangu! Ninapenda kuhusisha upendo wangu wa sanaa kwenye injili. Wakati mwingine hauhitaji kuwa mchoro wa kidini kwangu mimi kuhisi upendo wa Mungu. Nimewahi hata kuangalia michoro ya ndege hapo awali na nikawaza, “Aha, Mungu alimuumba ndege huyo kwa ajili yangu.”

Chapisha