2021
Ufunuo Endelevu
Machi 2021


“Ufunuo Usiokoma,” Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2021, 16.

Neno la Mwisho

Ufunuo Endelevu

Kutoka kwenye hotuba ya mkutano mkuu wa Aprili 2020.

Ono la Kwanza

Kielelezo na Ben Simonsen

Nabii Joseph Smith alipokea ufunuo baada ya ufunuo. Ufunuo mwingi aliopokea Nabii Joseph umehifadhiwa kwa ajili yetu katika Mafundisho na Maagano.

Pia, tumebarikiwa kuwa na ufunuo endelevu kupitia manabii wa sasa ambao ni “mabalozi waliotawazwa wa Bwana, waliopewa mamlaka ya kuzungumza kwa niaba Yake.”1

Ufunuo binafsi unapatikana pia kwa wote ambao kwa unyenyekevu wanatafuta mwongozo kutoka kwa Bwana. Ni muhimu kama ufunuo wa kinabii.

Ufunuo binafsi unategemea ukweli wa kiroho uliopokelewa kutoka kwa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ndiye mfunuaji na mshuhudiaji wa ukweli wote, hasa ule wa Mwokozi. Pasipo Roho Mtakatifu, tusingeweza kujua kwamba Yesu ndiye Kristo. Jukumu lake la msingi ni kushuhudia kuhusu Baba na Mwana na vyeo Vyao na utukufu Wao.

Ninawahakikishia kwamba kila mmoja wetu anaweza kupokea mwongozo wa kiufunuo pale tunapofanya kazi kwa unyenyevu katika shamba la Bwana.

Ombi langu la unyenyekevu ni kuwa kila mmoja wetu ataendelea kutafuta ufunuo usiokoma ili kuongoza maisha yetu na kumsikiliza Roho pale tunapomwabudu Mungu Baba na Mwokozi wetu, Yesu Kristo.

Muhtasari

  1. Hugh B. Brown, “Joseph Smith among the Prophets” (Sixteenth Annual Joseph Smith Memorial Sermon, Logan Institute of Religion, Dec. 7, 1958), 7.