2021
Jinsi ya Kuwa na Roho Daima
Machi 2021


“Jinsi ya Kuwa na Roho Daima,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2021, 26–29.

Njoo, Unifuate

Kujiandaa kuwa na Roho Wake

Kujiandaa kupokea sakramenti kwa kustahili kila wiki kunaweza kutusaidia kuwa na Roho pamoja nasi daima.

Picha
wavulana wakipitisha na kupokea sakramenti

Nilipokuwa na miaka 12, nilikwenda pamoja na wazazi wangu kuzuru maeneo ya kihistoria ya Kanisa huko kaskazini mwa New York, Marekani. Katika Kijisitu Kitakatifu, ninakumbuka kutafakari kuhusu Ono la Kwanza na maono mengine ya kupendeza Joseph aliyoyaona na kuwaza, “Lo! ikiwa ningekuwa na tukio la kupendeza la kiroho na viumbe wa mbinguni kama ilivyokuwa kwa Joseph, maisha yangu yangetulia.”

Nimejifunza tangu hapo kwamba badala ya tukio kubwa la kiroho la mara moja katika maisha yangu, ninahitaji uzoefu mdogo mdogo mara kwa mara ili kuniweka imara katika ushuhuda na usalama wangu kwenye njia ya kurudi nyumbani. Baba wa Mbinguni alijua kwamba tungehitaji mwongozo wa mara kwa mara katika maisha yetu, na Yeye aliandaa njia kwa ajili yetu kuupokea.

Kwa wale wote wenye imani ya kutosha katika Mwana Wake ya kutubu na kubatizwa, Yeye anatoa kipawa cha Roho Mtakatifu. Kupitia ibada ya kila wiki ya sakramenti, Yeye anatupatia uwezekano wa “daima roho wake kuwa [nasi]” ikiwa tutamkumbuka Mwokozi na kushika amri Zake (Mafundisho na Maagano 20:77). Hii inafanya iwezekane kwetu sisi kupata mwongozo wa kila siku wa Roho katika maisha yetu pale tunapotumia haki yetu ya kujiamulia kufanya maamuzi ambayo yatatusaidia njiani kurejea kwa Baba wa Mbinguni.

Sakramenti na Roho

Picha
sakramenti

Baba wa Mbinguni alijua tungehitaji mara kwa mara mwongozo wa Roho Wake, si tu uzoefu mkubwa wa mara moja. Kupitia Nabii Joseph Smith, Alirejesha ibada ya ubatizo kwa kuzamishwa majini, ambayo inatusaidia kuwa wasafi. Kisha tunaandaliwa kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu kwa kuthibitishwa, ikitupatia uwezekano wa mwongozo wa kila siku wa Roho.

Baba wa Mbinguni alijua kwamba kuwa wasafi mara moja hakungetosha na kwamba tungehitaji kumkumbuka Mwokozi na kuwa wasafi tena na tena ili kubaki na Roho pamoja nasi daima. Alirejesha ibada ya sakramenti kwa kusudi hilo. Ikiwa tutajiandaa kwa uangalifu kwa ajili ya na kupokea sakramenti mara kwa mara, tunaahidiwa “kwamba daima Roho wake apate kuwa pamoja [nasi]” (Mafundisho na Maagano 20:77; msisitizo umeongezwa).

Hata hivyo, kuhudhuria tu Kanisani na kula mkate na kunywa maji hakutaturuhusu kupata ahadi ya Bwana. Maandalizi yetu ya makusudi kwa ajili ya ibada hutusaidia kupokea nguvu ya Mwokozi katika maisha yetu.

Wanariadha hawawi mabingwa kwa kuvaa tu sare au kutembea uwanjani au kwenye eneo la kuchezea. Lazima waifunze miili yao, wajifunze mbinu, na kufanya mazoezi ili kuwa mabingwa katika mchezo wao. Kadhalika, sisi lazima tujifunze jinsi ya kujiandaa kupokea sakramenti kwa unyenyekevu na kwa kustahili ili tuweze kupokea nguvu ambayo Yeye anatupatia.

Njia moja ya kuuandaa moyo na roho yako kupokea sakramenti ni kuwa na usaili mdogo na nafsi yako kila wiki. Ninapenda kutumia Mafundisho na Maagano 20:37 kujifanyia usaili mwenyewe. Mstari huu una yanayohitajika kwa ajili ya ubatizo ambayo Mungu aliyafunua kwa Nabii Joseph. Una vigezo ambavyo wote wanaohitaji kubatizwa lazima wavikidhi. Ninapata kwamba unanisaidia kujiandaa mwenyewe kupokea ahadi za kufanya upya zinazopatikana kupitia sakramenti.

Picha
msichana akitafakari

Picha kutoka Getty Images

Kwa kutumia andiko hilo kama mwongozo wangu, haya ni baadhi ya maswali ninayojiuliza mwenyewe ili kuona ikiwa nimejiandaa kupokea sakramenti.

Je, nimenyenyekea mbele za Mungu?

Hitaji la kwanza lililoorodheshwa katika Mafundisho na Maagano 20:37 ni kunyenyekea mbele za Mungu. Tunafanya hili kwa kukubali na kuwa radhi kufuata mapenzi Yake kama yalivyoandikwa katika maandiko matakatifu, yalivyofundishwa na watumishi Wake, au kama yanavyokuja kwetu katika ushawishi.

Ninajiuliza mwenyewe ikiwa ninapigana na Mungu kwenye chochote katika maisha yangu hivi sasa. Je, ninaepuka mwongozo Wake? Je, mimi ni msikivu kwenye mafundisho ya watumishi Wake? Ikiwa sifanyi hivyo, ninaweka mipango ya kujiboresha na kuweka msimamo wa kufanya vizuri zaidi pale ninapojiandaa kupokea sakramenti. Mungu anafahamu yote—wakati ninapotambua kwamba Yeye anaweza kuona picha kubwa kwa ajili ya maisha yangu, inakuwa rahisi kujinyenyekeza mbele Zake na kuamini kwamba Ataniongoza kwenye kile kilicho kizuri sana.

Je, nina moyo uliovunjika na roho iliyopondeka?

Kuwa na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka kunahusiana na unyenyekevu. Inamaanisha kuwa radhi kujiweka chini ya mapenzi ya Mungu. Kuwa mnyenyekevu inamaanisha kusema tumekosea na kusamehe hata wakati ni vigumu au wakati tunapoweza kuhisi wengine walikuwa na makosa. Je, unaweza kusema, “Moyo wangu uko sawa na kila mtu”? Je, umemuumiza yeyote aliye karibu yako, au je, una hisia mbaya kuhusu mtu fulani? Je, unahitaji kuomba msamaha?

Wakati ninapokuwa na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka, ninakuwa radhi kufanya juhudi kuweka mambo sawa na Mungu pamoja na wale walio karibu yangu. Ninajaribu kuondoa mawazo na hisia mbaya dhidi ya wengine. Roho hakai nasi pale tunapokuwa na hisia za mabishano, hivyo kuziondoa ni hatua muhimu katika kujiandaa kupokea ahadi ya sakramenti.

Je, nina hamu ya kuwa msafi tena, na je, ninaweza kushuhudia kwamba nimetubu dhambi zangu zote?

Hitaji lingine katika Mafundisho na Maagano 20:37 ni “kwa hakika kutubu dhambi zetu zote.” Wakati tulipobatizwa, tulifanywa safi kutoka dhambi zetu. Tuliweka ahadi ya kujaribu kutii amri za Mungu na kutubu wakati tunapofanya makosa.

Ninajiuliza mwenyewe, “Je, ninapokea tu sakramenti kwa sababu ninadhani ninapaswa kufanya hivyo, au hakika ninataka kuwa msafi tena?” Ninatazama nyuma kwenye dhambi na makosa yangu ya wiki hiyo na kujiuliza mwenyewe ikiwa hakika ninataka kubadilika na kuyaacha. Pale unapokuwa na hamu ya kuwa msafi, utaona, kwa Roho, mambo unayohitaji kuboresha, na Yeye ataendelea kukupa msukumo wa kutubu na kufanya chaguzi nzuri.

Kuungama kwa Bwana (na kwa wengine ambao yaweza kuwa tumewadhuru au kuwakwaza ikiwa ni muhimu) ni sehemu ya maandalizi yetu.

Jiulize, “Je, kuna chochote ninahitaji kubadilisha ambacho bado sijabadilisha? Je kuna jambo ambalo bado ninahitaji kulifanyia toba?” Kutatua mambo kupitia toba ya dhati kunaweza kutustahilisha kupokea sakramenti kwa kustahili.

Je, niko radhi kujichukulia juu yangu jina la Yesu Kristo?

Kila agano tunalofanya huashiria msimamo wa kujichukulia jina la Kristo kikamilifu juu yetu. Wakati tunapobatizwa, tunaonesha utayari wetu wa kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo na kutii amri zake. Wakati tunapofanya maagano ya ziada hekaluni au kukubali miito, tunajichukulia zaidi kusudi la Kristo na mafundisho Yake juu yetu. Kuonesha utayari wetu wa kujichukulia juu yetu jina Lake kama sehemu ya sakramenti kila wiki humaanisha kuweka msimamo mpya kwenye maagano yote na misimamo tuliyofanya Naye siku za nyuma.

Katika kutathmini maandalizi yangu ya kupokea sakramenti, ninajiuliza mwenyewe maswali kama vile: “je, ninafanya vizuri kadiri niwezavyo kuwa mfano wa Kristo na mafundisho Yake? Je, ninatii ahadi zote nilizofanya zinazohusiana na maagano yangu? Je, msimamo wangu leo kwa Kristo na maagano yangu Kwake ni sawa na ule wa siku ambapo niliyafanya mwanzo?”

Je, nina ari ya kumtumikia Yeye mpaka mwisho?

Tulimwahidi Bwana wakati tulipofanya maagano yetu ya ubatizo kwamba tutajitahidi kutii amri Zake. Amri kuu mbili ni kumpenda Mungu na kumpenda jirani yako (ona Mathayo 22:36–40). Tunaonesha upendo wetu kwa wote Mungu na wanadamu wenzetu kwa kuwatumikia.

Ninajiuliza mwenyewe, “Je ninatenga muda wa kutumikia? Je, mimi ni mzito kutumikia, au nina furahi kutumikia?” “Je, ninajaribu kukuza wito wangu?” Kuwatumikia wengine ni njia ya kupendeza ya kujiandaa kupokea sakramenti. Kwa kweli, mara nyingi ni katika kuwatumikia wengine ambapo tunahitaji mwongozo wa Roho.

Amini katika Ahadi za Bwana

Tunapojiandaa kwa kukusudia kila wiki kupokea sakramenti, tutastahili daima kuwa na Roho kutushawishi na kuongoza maisha yetu. Hiyo ni ahadi kutoka kwa Bwana.

Chapisha