Historia ya Kanisa
Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo: Mpangilio wa Matukio


“Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo: Mpangilio wa Matukio,” Historia za Ulimwengu: Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (2020)

“Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo: Mpangilio wa Matukio,” Historia za Ulimwengu:Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo

Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo: Mpangilio wa Matukio

Septemba 1970 • Kinshasa, Jamhuri ya Demokrasia ya KongoKundi dogo la Watakatifu kutoka ughaibuni wanaoishi Kinshasa walianza kufanya mikutano ya Kanisa.

Miaka ya 1970–80 • nje ya ZaireWananchi wa Kongo walianza kujiunga na Kanisa wakiwa wanaishi ughaibuni, ikijumuisha Ubelgiji, Ufaransa, Ujerumani, uswisi, na Marekani.

Miaka ya 1970–80 • ZaireWatakatifu wa Kongo ambao walikuwa wamerudi kwenye nchi yao vilevile waumini wa Kanisa watarajiwa walianza kuwaandikia viongozi wa Kanisa, wakiomba taarifa, wamisionari, na misaada mingine ya Kanisa.

Agosti–Septemba 1979 • ZaireRais Spencer W. Kimball alimtuma Oscar McConkie Jr. kwenda Zaire kwenye ziara ya kuchunguza ukweli. Hii ilikuwa ya kwanza kati ya safari kadhaa kati ya mwaka 1979 na 1986 ili kujaribu kuanzisha Kanisa huko.

Miaka ya 1980 • Kinshasa na Jimbo la Shaba, ZaireMikutano isiyo rasmi ikitumia jina la Kanisa iliundwa na kuanza kuwasiliana na makao makuu ya Kanisa.

Februari 1986 • KinshasaWamisionari wa kwanza Zaire, Ralph na Jean Hutchings, waliwasili.

Aprili 1986 • ZaireBaada ya miaka saba ya kazi ya kuanzisha Kanisa katika nchi, Kanisa lilipewa utambulisho wa kisheria ndani ya Zaire.

Juni 1, 1986 • Kinshasa Junior Mucioko Banza na Philippe Banza wakawa watu wa kwanza kubatizwa Zaire. Wazazi wao, Mucioko Wa Mutombo Banza na Régine Mbuyi Banza walikuwa wamekwishajiunga na Kanisa nchini Switzerland mwaka 1979.

Septemba 1986 • KinshasaTawi la Kinshasa lilianzishwa. Michael C. Bowcutt aliitwa kama rais wa tawi pamoja na Mucioko Wa Mutombo Banza na Mbuyi Nkitabungi kama washauri na Régine Mbuyi Banza kama rais wa Muungano wa Usaidizi.

1986 • KinshasaWakati Uumini ulipoongezeka, mikutano ya Kanisa ilihamishwa kutoka nyumba ya Mbuyi Nkitabungi kwenda kwenye jengo lililokuwa Limete.

Februari 1987 • Lubumbashi, ZaireRoger na Simone Dock, wamisionari wakubwa, wakawa wamisionari wa kwanza kupangiwa kwenda Lubumbashi.

June 1987 • KinshasaMisheni ya Zaire Kinshasa ilianzishwa rasmi.

Julai 25, 1987 • LubumbashiTawi la Lubumbashi lilianzishwa, pamoja na Clement Mubalamate Kavuala kama rais.

Kuwekwa wakfu kwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo

Agosti 30, 1987 • Kinshasa

Mzee Marvin J. Ashton wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili aliiweka wakfu Zaire kwa ajili ya kuhubiriwa injili.

Agosti 1988• Jijini Salt Lake, UtahTeuzi za Kitabu cha Mormoni zilichapishwa katika Kilingala. Kitabu cha Mormoni chote kilichapishwa katika Kilingala mwaka 2004.

Septemba 18, 1988 • KinshasaWilaya ya Kinshasa Zaire ilianzishwa.

Desemba 1989 • LubumbashiMkutano wa kwanza wa wilaya wa Wasichana huko Zaire ulifanyika.

Januari—Februari 1991 • ZaireJunior Mucioko Banza, Ngalamulume Diamany, Thomas Nkadi Mutombo, na Kanda Malu‑Malu waliitwa kama wamisionari wa kwanza wa Kongo kuhudumu katika Misheni ya Zaire Kinshasa.

Aprili 1991 • ZaireMkutano wa Kitaifa wa watu wa Zaire ulianzisha uhuru wa dini.

Septemba 13, 1991 • ZaireProgramu ya seminari ilianzishwa Zaire, Kabwika Natambwe akiwa kama mkurugenzi wake.

1991–94 • Kinshasa, Zaire, na Brazzaville, Jamhuri ya KongoVurugu za kiraia zilivuruga utendaji kazi wa makao makuu ya misheni, ambayo yalitolewa kutoka Kinshasa kwenda Brazzaville mwaka 1991 na kufungwa kwa muda mnamo mwaka 1993–94.

Julai 1996• Johannesburg, Afrika KusiniKundi la kwanza la Watakatifu kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo lilisafiri kwenda hekalu la Johannesburg, Afrika Kusini kupokea ibada za hekaluni.

Novemba 3, 1996 • KinshasaKigingi cha kwanza Zaire, Kigingi cha Zaire Kinshasa, kilianzishwa, Wa Musithi Jacques Muliele akiitwa kama rais. Mwezi Mei uliofuata, Ekezi Imbale Baenda Ise’Ekungola Liyanzi akawa patriaki wa kwanza nchini.

Agosti 12, 1997 • Jamhuri ya Demokrasia ya KongoBaada ya nchi kubadili jina lake, jina la misheni lilibadilishwa kuwa misheni ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo Kinshasa.

Septemba 7, 1997 • LubumbashiKigingi cha Lubumbashi Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo kilianzishwa, Nzembelenge Milambo akiwa rais.

2000 • Jijini Salt LakeKitabu cha Mormoni kilichapishwa katika lugha ya Kiswahili.

Januari 2005 • Jamhuri ya Demokrasia ya KongoProgramu ya ajira ya Kanisa, warsha za kazi, na Mfuko wa Msaada wa Elimu vilitekelezwa. Kupitia programu ya misaada ya kibinadamu ya Kanisa, miwani zilizotolewa msaada ziligawiwa.

Septemba 9, 2006 • KinshasaVijana kutoka Kinshasa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo kigingi cha Masina waliratibu siku ya taifa ya huduma, kusafisha maeneo ya umma kwenye jumuiya.

Mei 1, 2007 • Jamhuri ya Demokrasia ya KongoDaniel Tusey Kola aliitwa kama Sabini wa eneo wa kwanza Mkongo.

Mei 22, 2011 • Kananga, Jamhuri ya Demokrasia ya KongoKigingi cha Kananga Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo kilianzishwa, Christophe Kawaya akiwa kama rais.

Julai 23 na 30, 2011• KinshasaMikutano miwili ya kwanza ya vijana nchini ilifanyika, ikiwa na zaidi ya watu 1,200 waliohudhuria.

Oktoba 1, 2011 • Jijini Salt LakeRais wa Kanisa Thomas S. Monson alitangaza hekalu litajengwa Kinshasa.

Julai 2014 • Brazzaville Elie Kyungu Monga na Vianney mwenze Monga waliitwa kusimamia misheni ya Brazzaville Jamhuri ya Kongo.

Februari 12, 2016 • KinshasaMzee Neil L. Andersen wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisimamia sherehe ya uwekaji msingi wa hekalu la Kinshasa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

Aprili 24, 2016 • Mbuji‑Mayi, Jamhuri ya Demokrasia ya KongoKigingi cha Mbuji‑May Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kigingi cha 15 katika nchi, kilianzishwa, N’sumbu Jean‑Pierre akiwa rais.

Agosti 2016 • KinshasaKanisa lilifikia makubaliano na serikali kuweka kidijitali zaidi ya rekodi milioni 20 za familia. Waumini wa Kanisa Richard Dadzie na Thierry Mutombo walikutana na Jean Claude Mabaya, katibu wa waziri wa mambo ya ndani, kusaini mkataba.

2016 • Jamhuri ya Demokrasia ya KongoUumini wa Kanisa ulipita 50,000

Oktoba 9, 2017 • Jijini Salt LakeKanisa lilitangaza mipango ya kutafsiri Kitabu cha Mormoni katika Kitshiluba na kuwapa waumini fursa ya kutengeneza sehemu za miswada kabla ya uchapishaji wa tafsiri ya mwisho.

Hekalu la Kinshasa

Aprili 14, 2019 • Kinshasa

Hekalu la Kinshasa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo liliwekwa wakfu.