Historia ya Kanisa
Kuileta Injili nchini Kongo


“Kuileta Injili nchini Kongo,” Historia za Ulimwengu: Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (2020)

“Kuileta Injili nchini Kongo,” Historia za Ulimwengu:Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo

Kuileta Injili nchini Kongo

Mapema yapata miaka ya 1960, watu wanaoishi katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ya sasa (iliyojulikana kama Zaire kutoka mwaka 1971 mpaka 1997) walianza kuwasiliana na makao makuu ya Kanisa. Ingawa Kanisa halikuwepo nchini, wawakilishi wa Kanisa walipeleka vitabu na matumaini kwa wale walioandika. Wengi wao walianza kufundisha injili na kuanzisha mikutano isiyo rasmi. Wakijibu juhudi hizi, Viongozi wa Kanisa walituma wawakilishi kuanzisha uwepo rasmi kuanzia mwaka 1979 na kuendelea mpaka katikati ya miaka ya 1980.

Wakati huo huo, wahamiaji wengi wa Kongo walikuwa wamelipata Kanisa Ulaya na Marekani. Mbuyi Nkitabungi alibatizwa nchini Ubelgiji mnamo 1980, alihudumu umisionari nchini Uingereza, na kisha alihisi msukumo kurudi nyumbani mnamo mwaka 1985. “Mojawapo ya lengo langu la haki ni kuijenga … Sayuni katikati ya Zaire,” aliandika kwa Makao Makuu ya Kanisa. “Ninajua kuna waumini wachache sana kutoka nchi yangu ambao wanasubiri fursa hiyo. … Niambieni kila kitu ninachotakiwa kukifanya.”

Nkitabungi aliunganishwa kwenye mawasiliano pamoja na waumini wengine wa Kinshasa, waliokutana katika nyumba ya Mike na Katie Bowcutt, wanandoa wa Marekani. Kama Nkitabungi, waumini wengi walikuwa Watakatifu wa Kongo waliojiunga na Kanisa ughaibuni. Kwa sababu Kanisa lilikuwa bado halijatambulika kisheria, hata hivyo, waumini hawakufanya mikutano ya wazi. Hata hivyo, kikundi kwa haraka kilizidi uwezo wa nyumba ya Bowcutt na walihamishia mikutano yao kwenye gereji ya Nkitabungi.

Picha
mkutano wa waumini ndani ya gereji ya Nkitabungi

Waumini wa mwanzo wa Tawi la Kinshasa wakikutana ndani ya gereji ya Mbuyi Nkitabungi, takriban mwaka 1986.

Mnamo Februari 1986 rais wa nchi aliahidi wakati wa taarifa ya habari kwenye runinga ya serikali kwamba angeruhusu kutambuliwa kisheria kwa Kanisa, na waumini hatimaye walianza kuhubiri injili kwa uwazi. Mwezi huo huo, Ralph na Jean Hutchings, wamisionari wa kwanza kuitwa kwenda Zaire, waliwasili na kukuta kikundi kinachokua ndani ya Kinshasa. Utambulisho ulitolewa rasmi mnamo Aprili, na ilipofika Juni 1987 Kanisa lilikuwa linakua kwa haraka sana nchini Zaire kiasi kwamba misheni ilianzishwa, na Ralph Hutchings kama rais.

Wamisionari pia walifikia mikutano isiyo rasmi karibu na Lubumbashi. Ingawa mabadiliko yalionekana magumu kwa baadhi, kitovu cha pili cha tegemeo mara kilijitokeza. Kati ya Mei na Julai 1987, watu 170 walibatizwa. Baadhi walikuwa wakisafiri umbali kama kilomita 300 (maili 186) kutoka Pweto, Kolwezi, na Likasi kuhudhuria mikutano.

Wakati Elie Monga mwenye umri wa miaka 21 wa Kolwezi aliposoma Kitabu cha Mormoni mwaka 1987, alivutiwa. “Nilihisi kwa nguvu”, alisema baadae, “kwamba hicho ndicho nilichohitaji.” Monga alisafiri kilomita 300 mpaka Lubumbashi kukutana na wamisionari. Baada ya majadiliano ya mara moja, aliamua kubatizwa. Baada ya ubatizo wake, pamoja na kutiwa moyo na wamisionari, alianzisha mikutano ya Shule ya Jumapili nyumbani kwake. “Tulianza kukusanyika na kuwafundisha rafiki zetu [na familia],” alisema, “tukiwaletea ujumbe wa matumaini kupitia injili ya urejesho.” Kundi kubwa punde lilikuwa likikusanyika nyumbani kwa Monga. Wakati huduma ya kwanza ya ubatizo huko Kolwezi ilipofanyika mwaka uliofuata, ilichukua zaidi ya masaa matatu na nusu kwa Monga kuwabatiza waongofu 82 ambao walikuwa wameikubali injili. Ilikuwa moja ya mafanikio miongoni mwa mengi: mnamo mwaka 1990, miaka minne tu baada ya Kanisa kupata kutambuliwa na serikali, matawi na wilaya zilikuwa zikistawi Kinshasa, Lubumbashi na kwenye majiji mengine mengi nchi nzima.

Chapisha