Historia ya Kanisa
Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo: Maelezo ya Jumla


“Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo:Maelezo ya Jumla,” Historia za Ulimwengu: Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (2020)

“Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo:Maelezo ya Jumla,” Historia za Ulimwengu: Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo

Historia Fupi ya Kanisa katika

Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo

ramani ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo

Maelezo ya jumla

Katika miaka ya 1960, waongofu kadhaa wa Kongo ambao walikuwa wamebatizwa nje ya nchi walirudi katika nchi yao ya asili na walianza kuomba makao makuu ya Kanisa kutuma wamisionari kwenye nchi yao. Mnamo mwaka 1979, baada ya kupokea barua kadhaa kutoka nchini, Rais wa Kanisa Spencer W. Kimball alimtuma Oscar McCknkie, Mwanasheria wa Kanisa, kukagua uwezekano wa kuanzisha Kanisa Zaire (baadae iliitwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo).

Ingawa usajili wa kisheria ulichukuwa karibia miaka saba, waongofu kwa mwanzo walikutana pamoja katika vikundi vidogo na walishiriki imani yao kwa majirani. Wakati wamisionari wa kwanza, Ralph na Jean Hutchings, walipowasili mwezi Februari 1986, palikuwa na makundi kadhaa wakikutana kila wiki. Mnamo Juni 1986 wilaya ilianzishwa, na mwaka uliofuata misheni iliundwa Kinshasa. Mnamo Agosti 30, 1987, Mzee Marvin J. Ashton wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alialisafiri kwenda Kinshasa na aliiweka wakfu nchi kwa ajili ya kuhubiriwa injili.

Ingawa misheni kwa muda mfupi ilifungwa mwanzoni mwa miaka ya 1990; waumini waliendelea kushiriki injili. Mwaka 1996, kigingi cha kwanza kinshasa kilianzishwa, na mnamo mwaka 1997 kigingi cha kwanza katika Lubumbashi kiliundwa. Waumini wa Kanisa walikuwa na imani na walihudumiana kupitia mapigano ya mwishoni mwa miaka ya 1990 na mapema 2000, wakifanya kazi kutengeneza vigingi vya Sayuni kuwa “sehemu ya kimbilio kutoka kwenye tufani” katika wakati wa matatizo (Mafundisho na Maagano 115:6). Wakati wa mkutano mkuu wa Oktoba 2011, Rais wa Kanisa Thomas S.Monson alitangaza mipango kwa ajili ya hekalu kujengwa Kinshasa. Liliwekwa wakfu mwaka 2019.

Vidokezo

  • Jina Rasmi: Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo/Republique democratique du Congo/Repubilika ya Kongo ya Dimokalasi/Republiki ya Kongo Demokratiki/Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo/Ditunga dia Kongu wa Mungalaata

  • Mji mkuu: Kinshasa

  • Jiji Kuu: Kinshasa

  • Lugha: Kifaransa, Kikongo, Kilingala, Kiswahili, na Kiluba‑Katanga

  • Eneo la nchi: 2,345,409 km2 (905,567mi2)

  • Eneo la Kanisa: Kusini Mashariki ya Afrika

  • Misheni: 3 (Kinshasa, Lubumbashi, na Mbuji‑Mayi)

  • Mikusanyiko: 181

  • Mahekalu: 1 (Kinshasa)