Historia ya Kanisa
“Tulikuwa na Shangwe Hiyo Mioyoni Mwetu”


“‘Tulikuwa na Shangwe Hiyo Mioyoni Mwetu,’” Historia za Ulimwengu: Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (2020)

“‘Tulikuwa na Shangwe Hiyo Mioyoni Mwetu,’” Historia za Ulimwengu:Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo

“Tulikuwa na Shangwe Hiyo Mioyoni Mwetu”

Mnamo mwaka 1989 wakati Daniel na Thérèse Kola walipojifunza kuhusu injili ya urejesho, mapato yao mengi yalitokana na mauzo ya kahawa, tumbaku, na pombe kwenye mgahawa wao. Baada ya kulikubali Neno la Hekima, hata hivyo, walijiuliza kama ilikuwa sawa kuuza vitu walivyotaka kuviepuka. Walijadiliana wafanye nini mpaka siku ya ubatizo wao. Waliamua kuacha kazi yao ya zamani, kama wafuasi wa kale wa Kristo. “Asubuhi, uamuzi ulifanyika ,” Daniel Kola anakumbuka. Waliuza duka lao na walibatizwa, wakiamini wamefanya kile ambacho Bwana angewataka wafanye. “Tulikuwa na shangwe hiyo Mioyoni mwetu kwa sababu tulihisi kitu fulani.”

Kwa miaka saba iliyofuata, Daniel na Thérèse walihudumu kwa uaminifu wakati Kanisa lilipokuwa linakua katika nchi yao. Kama wengine katika kizazi cha kwanza cha Watakatifu wa Siku za Mwisho katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, walijifunza hatua kwa hatua. Mnamo mwaka 1996 Viongozi wa Kanisa wa Kongo walipewa changamoto kuchukua hatua inayofuata katika maendeleo yao. Ingawa Kinshasa ilikuwa karibia kilomita 4,000 (maili 2485) kutoka hekalu lililo karibu sana, huko Johannesburg, Afrika Kusini, kikundi cha zaidi ya viongozi 20 walialikwa kusafiri kwenda hekaluni pamoja ili kupewa endaumenti ya nguvu kutoka mbinguni na kuunganishwa kwa waume au wake zao milele na milele. Ilikuwa safari ya kwanza ya kikundi kwenda hekaluni katika historia ya Kongo.

Miaka ya baadae safari za hekaluni zilikuwa za muhimu kwa ajili ya Kanisa katika Kongo. Mwishoni mwa miaka ya 1990, kigingi baada ya kigingi vilianzishwa katika Kongo. Wengi wa watu walioitwa mwanzo kama marais wa vigingi, ikiwa ni pamoja na Daniel Kola, walikuwa wameshiriki katika msafara ule wa hekaluni.

Mnamo mwaka 2007 Daniel Kola aliitwa kama Sabini wa Eneo. Mwaka uliofuata, alisafiri kwenda Utah kuhudhuria mkutano mkuu na alibarikiwa kuhudhuria hekaluni mara tano zaidi kufanya ibada za mwanzo, endaumenti, na kuunganishwa kwa niaba ya mababu zake, ikiwa ni pamoja na kuunganishwa kwa wazazi wake. “Wakati nilipopokea endaumenti yangu, kulikuwa na mengi ambayo sikuweza kuyaelewa,” Kola alikumbuka. “Lakini leo, ninaelewa na ufahamu wangu ni wa kina zaidi.”

Alipokuza uelewa zaidi wa hekalu, Kola pia alikuza hamu kubwa ya kupenda historia ya familia. Pamoja na wengine wengi, alikuja kutambua kwamba aliishi wakati wa muhimu sana, wakati majina na hadithi za mababu wengi zilikuwa bado katika kumbukumbu zinazoishi lakini katika hatari ya kupotea kama hazikuwekwa kwenye kumbukumbu. Mnamo mwaka 2018 shirika lisilo la faida la Daniel Kola liliingia mkataba na Family Search kusafiri kuzunguka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo wakiandika simulizi za historia, wakiazimia kukusanya majina 400,000 ndani ya miezi 12.