Historia ya Kanisa
Kurejesha Wema


“Kurejesha Wema,” Historia za Ulimwengu: Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (2020)

“Kurejesha Wema,” Historia za Ulimwengu: Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo

Kurejesha Wema

Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1990, watu wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo walivumilia mapigano makali sana waangalizi wengi waliyoyaita “Vita Kuu ya Ulimwengu ya Afrika.” Wakati wa mapigano, mamilioni ya wananchi wa Kongo walihamishwa kutoka majumbani mwao, wakati mwingine waliweka makazi ughaibuni. Rossette Bahati alikuwa miongoni mwa wakimbizi hao. Mnamo mwaka 1998, baada ya mumewe kuchukuliwa na askari, Rosette na watoto wake saba walikimbilia Uganda, ambako walifanya makazi kwa muda katika kambi ya wakimbizi. Wakiwa pale, vifurushi vya misaada ya kibinadamu vilisaidia kuwapa riziki. “Nilitambua nembo ya samawati na nyeupe kwenye maboksi,” alikumbuka Rosette juu ya baadhi ya vifurushi. “Sikujua Kingereza, lakini nilikumbuka alama.”

Mwaka mmoja baada ya kuwasili kwa Rosette katika kambi, mumewe aliweza kufika pale, na mnamo Julai 2006 familia yake ilikubaliwa kuingia marekani na kuweka makazi Utah. Walipotafuta Kanisa ili wahudhurie, wamisionari waliwaalika kwenye mikutano ya Watakatifu wa Siku za Mwisho. “Kamwe hatutasahau mkutano ule wa kwanza tuliohudhuria.” alikumbuka Rosette. “Waumini walitupokea kwa wema mkubwa.” Rosette punde alipata fursa ya kuhudumu kwa kufanya kazi kwenye Kituo cha misaada ya kibinadamu cha Watakatifu wa siku za Mwisho katika Jiji la Salt Lake. Pale, alitambua nembo ya kifurushi inayofanana na ile kutoka kambi ya Uganda. “Nilijazwa na shangwe kuu kwamba nilikuwa nasaidia kurudisha wema niliofanyiwa mimi pamoja na familia yangu,” alisema.

Mnamo mwaka 2014, Rosette pia alipokea wito kuhudumu kama rais wa Muungano wa Usaidizi wa tawi la wanaozungumza-Kiswahili la Jiji la Salt Lake. Katika tawi, waumini karibu wote walikuwa wakimbizi—mara nyingi kutoka makundi ya kikabila kwenye pande zinazopingana za mapigano waliyoyakimbia. “Dada zetu wanakuja kutoka maeneo ya Afrika ambako bado kuna mapigano na machafuko kati ya makabila,” Rosette alisema. “Lakini katika tawi tunajaribu kuungana katika udada wetu na tunajaribu kumfanya kila dada ahisi kwamba yeye ni kipenzi na ni wa kipekee katika macho ya Baba wa Mbinguni.”

Chapisha