UJUMBE WA KIONGOZI WA UKUHANI
Kumpenda Baba Yetu wa Mbinguni na Mwanaye Yesu Kristo kwa Moyo Wetu Wote
“Kutuwezesha kuonesha upendo wetu kwa Mungu na Mwanaye Yesu Kristo kwa vitendo, kila muumini wa Kanisa anapaswa kuongeza kwa kina kiwango chake cha uongofu.”
Mara nyingi hutokea kwamba kwa moyo tunawashukuru watu kwa kila kitu walichofanya kwa ajili yetu. Hata hivyo, njia nzuri ya kuonesha shukrani zetu ni kuweka wazi jinsi gani tunajali kuhusu watu hawa na jinsi gani tulivyo na shukrani kwa yote waliyoweza kufanya kwa ajili yetu.
Miongoni mwa watu ambao tunapaswa kuwashukuru tunaweza kuwaorodhesha, kwa mfano, wazazi wetu kwa ajili ya sababu nzuri kwamba walituleta katika ulimwengu na zaidi ya yote, kwa kuweza kutupa elimu nzuri kwenye kiwango cha kiroho na kimwili.
Kama ilivyotokea kwa Nefi, wakati aliposhuhudia juu ya uzuri wa wazazi wake kuhusu yeye, akitangaza kwamba: “Mimi, Nefi, nikiwa nimezaliwa na wazazi wema, kwa hiyo nilikuwa nimefunzwa karibu yote ambayo baba yangu alijua; na baada ya kushuhudia masumbuko mengi maishani mwangu, haidhuru, nikiwa nimebarikiwa na Bwana maishani mwangu; ndio, nikiwa nimepokea ufahamu wa wema na siri za Mungu, kwa hivyo naandika maandishi juu ya mambo ya maisha yangu.” (1 Nefi 1:1–3). Ushuhuda huu wa nefi ni tendo la shukrani lililomwagwa katika namna ya upendo uliooneshwa na moyo wake wote kwa wazazi wake.
Kama Nefi, kuna sababu mbili za msingi kwa ajili yetu kumpenda Mungu Baba yetu wa Mbinguni na Mwanaye Yesu Kristo kwa mioyo yetu yote:
Ya kwanza ni kutambua kwamba Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni na kwamba, kwa hiyo angeweza kuwa na jambo moja la mwisho akilini, kupanga mpango unaofaa wa wokovu ili kutupa sisi furaha ya milele kupitia kufufuka na msamaha wa dhambi zetu (ona Alma 12:25–34). Kwa vyovyote vile, kila kitu kilifanywa kiwezekane kupitia mpango wake wa ukombozi ambao ni ukamilifu wa injili ya Yesu Kristo (ona Mafundisho na Maagano 128:12; Musa 6:52–62).
Aidha, Baba yetu wa Mbinguni, katika kutuumba, aliweka katika mamlaka yetu amri Zake katika hizi njia ya mbinguni inaoneshwa wazi kwa ajili yetu kuifuata. Ametupa pia ushauri muhimu tunaouhitaji kuendelea na kufikia uwezo wetu wa kiungu. Hii inapaswa kututia moyo kwa jinsi Baba yetu wa Mbinguni anavyotujua vizuri kila mmoja wetu, watoto Wake, na kwa jinsi Anavyojua vizuri kusudi gani alituumba.
Kwa hiyo, Anatuonya kupitia manabii Wake wakati akibaki mwenye huruma kwa wale wanaotubu dhambi zao. Wakati mwingine Yeye (Mungu) huwatumia manabii wake kama waangalizi juu ya ukuta au mnara kuonesha hatari yoyote inayokuja (ona Isaya 62:6; Ezekieli 33:1–7; Helamani 13:2–5).
Sababu ya pili inahusiana na chochote ambacho kinaweza kututia hamasa kwa unyenyekevu kutafakari juu ya kweli kamili kama zilivyoelezwa kwa muhtasari hapo chini:
“Kwa maana hapana jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu, litupasalo sisi kuokolewa nalo” (matendo ya Mitume 4:12; ona pia 1 Wakorintho 15:22).
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).
“Maana hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika Yeye” (Yohana 3:17; ona pia Yohana 8:12; Waibrania 5:8–9; Alma 12:25–34).
Ili kutuwezesha sisi kuonesha upendo wetu kwa Mungu na Mwanawe Yesu Kristo kwa vitendo, kila muumini wa Kanisa anapaswa kuongeza kwa kina kiwango chake cha uongofu. Kama vile Nefi alivyoshuhudia juu ya upendo wake kwa wazazi wake, tunapaswa kushuhudia juu ya upendo wetu kwa Baba wa Mbinguni na Mwanawe Yesu Kristo.
Tunapaswa kuboresha kanuni za siku ya Sabato nyumbani na Kanisani. Tunapaswa kuwa na kibali halali cha hekaluni ili kushiriki katika ibada za hekalu—Kwa sababu kila kitu tunachofanya kanisani kinatuelekeza hekaluni. Tunapaswa pia kusoma Kitabu cha Mormoni kila siku kuhusu swala hili, Rais Russell M. Nelson alitangaza kwamba, “Kweli za Kitabu cha Mormoni zina nguvu za kuponya, kufariji, kurejesha, kusaidia, kuimarisha, kuliwaza, na kuchangamsha nafsi zetu” (Russell M. Nelson, “Kitabu cha Mormoni: Je, Maisha Yako Yangekuwaje Bila Kitabu Hiki?”, Liahona, Novemba 2017, 62).
Tunapaswa kuonesha upendo wetu miongini mwa waumini, tunapaswa kuhudumia na kufundisha na kutunzana tunapohudumia (ona Mafundisho na Maagano 20:53). Tunapaswa mmoja mmoja, kuwasaidia wale wanaojitahidi na shuhuda zao, na kushiriki injili na watu ambao sio wa imani yetu (ona Mafundisho na Maagano 18:15).
Pia tunahitaji kulipa zaka za kweli na matoleo ya mfungo ya kikarimu (ona Malaki 3:10). Tunapaswa kuchukua jukumu binafsi kufanya kazi na kuwa wenye kujitegemea (ona Kitabu cha Mwongozo 2, 6,1,1). Na mwishowe, tunapaswa kuwaandaa vyema kizazi kinachochipua kuhudumia umisionari (ona Marko 16:15).
Najua kwamba ono kwa ajili ya eneo la Afrika ya Kati ni chapa iliyoundwa kwa mfano wa mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni na umesanifiwa kutuwezesha kufikia uwezo wetu wa kuweza kuwa watakatifu.
Mzee Christophe Kawaya aliitwa kama Sabini wa Eneo mnamo Aprili 2016. Amemwoa Souzane Kawaya. Wao ni wazazi wa watoto tisa.