2021
Acha Nuru Yako Iangaze
Januari 2021


SAUTI ZA WAUMINI

Acha Nuru Yako Iangaze

“Mibonyezo kadhaa baadaye—na kile kinachoweza kuelezewa kama msukumo kutoka kwa Roho—alifika mbali duniani.”

Nairobi ni nyumbani kwa wakazi wa jiji zaidi ya milioni 4. Unajulikana kwa ajili ya mitaa yenye msisimko, watu wanaopenda kushirikiana, na mandhari ya kustaajabisha, ni rahisi kuona kwa nini ni Jiji Kijanikibichi Juani unafikiriwa kuwa ndiyo mapigo ya moyo wa Kenya. Kukiwa na vigingi viwili vya Sayuni na mikusanyiko 54 iliyosambaa kote katika majimbo kadhaa, ya hili taifa la Afrika Mashariki lenye msisimko linaloongezeka na kuwa kitovu cha nguvu, ngome ya kweli ya watakatifu waaminifu ambao wanamstahi Bwana na wanaotafuta kutembea katika njia Zake.

Stephen Owino ni mkazi wa muda mrefu wa jiji hili na mwanzilishi wa kisasa katika kila maana ya neno. Kilichosukwa kwa unadhifu kuwa pambo zuri la imani ni nyuzi za udadisi na subira katika kutafuta ukweli. Hadithi yake ya kuchochoea nafsi inajumuisha wahusika wengi, kote katika mabara mawili, wakifanya kwa pamoja ili kumsaidia katika mapito yaliyotembelewa ya uanafunzi. Huyu baba wa watoto watatu mpole mwenye bashasha alikabiliana na maswala yale yale ambayo Joseph Smith na kile mtafutaji mwaminifu wa ukweli ambayo sharti aulize. Mimi ni nani? Ni nini azma ya maisha? Ni kanisa gani ninapaswa kujiunga nalo?

Safari ya kusonga mbele ya Stephen kwenye njia ya agano ilianza na utafutaji mtandaoni wa makanisa katika Kenya , mwaka wa 2018. Ilikuwa katika mojawapo ya utafutaji huo ambapo alipata rejeo la Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho na akafikiria, “Jina refu la kipekee la kanisa.” Mibonyezo kadhaa baadaye—na kile kinachoweza kuelezewa kama msukumo kutoka kwa Roho—alifika mbali duniani hadi kwa Tonya Isom, akiuliza kuhusu uwezekano wa kukutana na wamisionari ili aweze kujifunza zaidi kuhusu imani yake. Kwa nini Tonya? Kwa baadhi ya sababu hawezi kuelezea, picha ilikuwa wazi kwenye ukurasa rasmi wa Facebook wa Kanisa na alihisi angempatia msaada kupata majibu aliyokuwa anatafuta.

Majuma kadhaa yalipita kabla ya Tonya kusoma ujumbe wa Stephen. Katika majibu yake, alijumuisha kiungo cha tovuti rasmi ya Kanisa na kumuelekeza jinsi ambavyo angeweza kuwasiliana na wamisionari walio katika eneo lake. Kwa msaada wa kitambuzi cha mtandaoni cha Kanisa, alimsaidia Stephen kupata jumba la kanisa lililo karibu, ambalo lilikuwa maili 9,570 kutoka mji wa Alamo, Calfornia.

Wakati Kamili wa Bwana

Mnamo Januari 24, 2020, Tonya alimsaidia Stephen kukutana na Mzee James Steward na mmisionari mwenza ambao walikuwa wamisionari waliokuwa wanatumikia katika kata ya Calfornia wakati huo. Kwa muda wa miezi mitatu iliyofuata, hawa wamisionari walizungumza na Stephen kwa njia ya WhatsApp, walishiriki naye ujumbe wa injili iliyorejeshwa. Walimhimiza asome Kitabu cha Mormoni na kuhudhuria kanisani kila mara.

Kwa sababu Stephen anaishi Nairobi, jukumu la kumfundisha na kumuandaa Stephen kwa ajili ya ubatizo lilitolewa na Rais Khumbulani Mdletshe wa Misheni ya Nairobi Kenya kwa kina Dada Clementine, Fretton, na Dingili—wanaotumikia Nairobi kama wamisionari. Walianza kumfundisha Stephen masomo ya kimisionari.

Mzee Steward—ambaye aliweka kumbukumbu makini ya kidigitali ya maendeleo ya Stephen—hangeweza kuficha furaha yake alipojua kwamba, miezi sita baada ya kukutana kwa njia ya mtandao, Stephen aliweka sharti la ubatizo. Mzee Steward anasifia uzoefu wa mapema wa kufundisha mtandaoni—kitambo kabla haijakuwa kawaida katika misheni yake mwenyewe—“Wakati Kamili wa Bwana”.

23 Agosti 2020, Mzee Edward—pamoja na Tonya (na baadhi ya washiriki walioalikwa wa familia ya Tonya)—waliwasha simu janja yenye video na kutazama ubatizo wa Stephen, uthibitisho, na baadaye kutawazwa kwenye Ukuhani wa Haruni chini ya Askofu Benard Oliech, wa Kata ya Upperhill huko Nairobi. Inastaajabisha unapofikiria mambo haya yote yakiwezeshwa na teknolojia ya kisasa—ambayo hata wakati wa COVID-19, kazi ya Bwana inaweza kusonga mbele. Wale waliokuwa karibu na video hiyo walielezea kuhisi Roho kutoka maeneo tofauti ulimwenguni. “Ni muujiza wa siku ya leo,” Tonya alisema.

Tonya anapata faraja kuu katika kushiriki injili. Anaamini kwa dhati, pale mengi yametolewa, mengi yanatarajiwa. Hivi karibuni kwa maongezi kwa njia simu ya video yaliyohudhuriwa na waumini wa Kata ya Upperhill, aliwaasa wote, “Kumbuka thamani ya nafsi ni kubwa mbele za Mungu” (Mafundisho na Maagano 18:10).

Sheheneza Ulimwengu na Nuru

Stephen, kama maelfu ya waumini wa Kanisa kote duniani, haoni haya kusheheneza ulimwengu kwa nuru ya injili yake mwenyewe kupitia mtandao wa kijamii. Nani ajuaye? Pengine nafsi nyingine inayozurura katika sehemu ya ulimwengu, karibu au mbali na Stephen, watapata nuru ambayo ameshiriki, na kupata rafiki—na hata ukombozi.

Screven Usi ni muumini wa Kata ya Upperhill, Kigingi cha Nairobi Kenya Magharibi.