2022
Januari 1993: Tawi la kwanza huko Cameroon
Januari/Februari 2022


MWEZI HUU KATIKA HISTORIA YA KANISA

Januari 1993: Tawi la kwanza huko Cameroon

Akiwa anasomea upasuaji wa kinywa huko Nantes, Ufaransa, Gervais Gerald Zang alianza kuwa na maswali mengi kuhusu maisha, maswali ambayo imani yake ya Kikatoliki haikuwa na majibu yake. Alianza kuchunguza makanisa mengi na, katika safari hii, alikutana na wamisionari Watakatifu wa Siku za Mwisho. Alibatizwa mnamo 11 Novemba 1989 na baada ya miezi michache alipokea Ukuhani wa Melkizedeki na alitawazwa kuwa mzee ndani ya kanisa. Baada ya kupata stashahada zake katika upasuaji wa kinywa, alirejea Cameroon.

Mnamo tarehe 10 Januari 1993 Tawi la kwanza la Kanisa huko Cameroon liliundwa. Likijulikana kama Tawi la Bastos, lilianzishwa huko Yaoundé, Cameroon, Kaka Zang akiwa kama rais wa tawi.

Mnamo Septemba ya mwaka huo huo Kanisa lilipata kibali cha kutambulika kisheria kutoka kwa Rais wa Cameroon. Kabla ya serikali kuruhusu kutambulika huko, takribani watu 30 walikuwa wamebatizwa na wachunguzi wengine wa Kanisa 60 walikuwa wakihudhuria mikutano ya Jumapili. —Dada Julie Brough, Mmisionari wa Historia ya Kanisa Afrika ya Kati