“Julai 7–13: ‘Tuzo Lao Litakuwa Kuu na Utukufu Wao Utakuwa wa Milele’: Mafundisho na Maagano 76,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Mafundisho na Maagano 76,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Julai 7–13: “Tuzo Lao Litakuwa Kuu na Utukufu Wao Utakuwa wa Milele”
Mafundisho na Maagano 76
“Nini kitatokea kwangu baada ya mimi kufa?” Karibu kila mtu huuliza swali hili katika njia moja au nyingine. Kwa karne nyingi, tamaduni nyingi za Kikristo, zikitegemea mafundisho ya biblia, zimefundisha juu ya mbinguni na jehanamu, juu ya paradiso kwa ajili ya wenye haki na mateso kwa ajili ya waovu. Lakini je, familia yote ya mwanadamu inaweza kweli kugawanyika kwa ukomo hivi? Mnamo Februari 1832, Joseph Smith na Sidney Rigdon walijiuliza ikiwa kulikuwa na cha ziada cha kujua kuhusu mada hiyo (ona Mafundisho na Maagano 76, kichwa cha habari cha sehemu).
Hakika kilikuwepo. Wakati Joseph na Sidney wakitafakari mambo haya, Bwana “aligusa macho ya ufahamu [wao] nayo yakafunguka” (mstari wa 19). Walipokea ufunuo wa kupendeza sana, mpana sana, wa kuangaza sana, ambao Watakatifu kwa urahisi waliuita “Ono.” Lilifungua madirisha ya mbinguni na kuwapa watoto wa Mungu mtazamo wa milele wa kupanua akili. Ono lilifunua kwamba mbingu ni tukufu na pana na yenye mjumuisho zaidi kuliko watu wengi walivyowahi kufikiria awali. Mungu ana rehema nyingi na ni mwenye haki kuliko tunavyoweza kuelewa. Na watoto wa Mungu wana hatma ya milele yenye utukufu kuliko tunavyoweza kudhani.
Ona Saints, 1:147–50; “Vision,” katika Revelations in Context, 148–54.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Wokovu huja kupitia Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.
Sehemu ya 76 inafunua kweli muhimu kuhusu hatma yetu ya milele, lakini ingekuwa si kamili kusema kwamba ufunuo huu ni kuhusu falme tatu za utukufu au hata tu kuhusu mpango wa wokovu. Sahihi zaidi, sehemu ya 76 ni kuhusu Yesu Kristo, ambaye hufanya mpango wa Mungu kwa ajili ya wokovu wetu na utukufu wa milele viwezekane. Unaposoma, ungeweza kutafuta maneno au virai ambavyo vinaelezea uhusiano baina ya Yesu Kristo na watu wanaorithi falme tofauti za utukufu. Pengine jedwali kama lifuatalo lingeweza kukusaidia uandike kile unachokipata.
Ufalme wa utukufu |
Uhusiano na Yesu Kristo |
Baraka za milele |
---|---|---|
Ufalme wa utukufu Selestia: (mstari wa 50–70, 92–96) | Uhusiano na Yesu Kristo
| Baraka za milele
|
Ufalme wa utukufu Terestria (mstari wa 71–79, 97) | Uhusiano na Yesu Kristo | Baraka za milele |
Ufalme wa utukufu Telestia (mstari wa 81–90, 98–106, 109–12) | Uhusiano na Yesu Kristo | Baraka za milele |
Unahisi mwongozo wa kufanya nini ili kuimarisha uhusiano wako na Mwokozi?
Wakati Wilford Woodruff aliposoma ono hili, alisema, “Nilihisi kumpenda Bwana zaidi kuliko hapo kabla katika maisha yangu” (ona, “Sauti za Urejesho: Shuhuda za Ono”). Unajifunza nini kumhusu Yesu Kristo kutoka kwenye mstari wa 1–5, 20–24, 39–43, 107–8 ambacho kinakufanya wewe umpende Yeye zaidi?
Ona pia 1 Petro 3:18–19; 4:6; Dallin H. Oaks, “Je, Mwokozi Wetu Amefanya Nini kwa ajili Yetu?,” Liahona, Mei 2021, 75–77; “Nastaajabu,” Nyimbo za Dini, na. 106.
Mafundisho na Maagano 76:5–10; 114–18
Ninaweza kuyajua mapenzi ya Mungu “kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.”
Siyo waumini wote wa Kanisa, walikubali kwa urahisi ufunuo katika sehemu ya 76, kwa sababu ulifundisha kwamba karibu kila mmoja angeokolewa na kupokea baadhi ya falme za utukufu. Kwa mfano, Brigham Young alisema: “Desturi zangu zilikuwa hivi, kwamba wakati Ono lilipokuja kwangu kwa mara ya kwanza, lilikuwa moja kwa moja kinyume na lilipingana na elimu yangu ya awali. Nilisema, Subiri kidogo. Sikulikataa; lakini sikulielewa.” Alieleza kwamba ilimbidi “atafakari na kusali, asome na kutafakari, hadi alipojua na kuelewa yeye mwenyewe” (katika “The Vision,” katika Revelations in Context, 150). Unajifunza nini kutoka kwenye uzoefu wake kinachoweza kukusaidia wakati Mungu anapofunua vitu ambavyo ni tofauti na uelewa wako wa sasa? Unajifunza nini kuhusu Mungu katika Mafundisho na Maagano 76:5–10, 114–18? Mistari hii inafundisha nini kuhusu jinsi tunavyoweza kuelewa “uradhi wa mapenzi ya [Mungu]”? (mstari wa 7).
Mafundisho na Maagano 76:39–44; 50–70
Kuinuliwa ni aina ya juu zaidi ya wokovu.
Mafundisho na Maagano 76:39–44 inaelezea wokovu kwa ujumla. Mstari wa 50–70 inaelezea kuinuliwa, aina mahususi ya wokovu. Ni kwa jinsi gani ungeweza kuelezea tofauti kati ya wokovu na kuinuliwa? Ni lipi jukumu la Mwokozi katika yote? Unapata nini katika mistari hii ambacho kinakupa msukumo wa kutafuta kuinuliwa?
Mafundisho na Maagano 76:50–70; 92–95
Baba yangu wa Mbinguni anataka nipokee uzima wa milele katika ufalme wa selestia.
Je, umewahi kujiuliza—au kuwa na wasiwasi—kuhusu ikiwa wewe unaweza kuwa mtu wa aina ambaye atapokea utukufu wa selestia, kama ilivyoelezwa katika Mafundisho na Maagano 76:50–70; 92–95? Wakati ni muhimu kujua kile Mungu anachotarajia kutoka kwetu, fikiria pia kutafuta katika mistari hii kile ambacho Mungu amefanya kwa ajili yetu—na ambacho anafanya—ili kutusaidia sisi tuwe kama Yeye. Kwa nini unahisi juhudi zako zina maana Kwake?
Ni kwa jinsi gani ono hili la utukufu wa selestia linaathiri jinsi unavyotaka kuishi maisha yako ya kila siku?
Ona pia Musa 1:39; J. Devn Cornish, “Je, Mimi ni Mzuri vya Kutosha? Je, Nitaweza?,” Liahona, Nov. 2016, 32–34
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Sisi sote tu watoto wa Mungu.
-
Ili kuwasaidia watoto wako waelewe uwezekano wao wa kiungu, ungeweza kuwaonesha picha za watoto na wazazi wao. Ungeweza kisha kusoma Mafundisho na Maagano 76:24 na kushiriki mmoja na mwingine kwa nini mnafurahia kujua kwamba sisi sote ni “wana na mabinti wa Mungu.”
-
Mngeweza pia kuimba pamoja “I am a Child of God” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3) na waalike watoto wako wajioneshe kwa kidole wanapoimba “Mimi.” Kisha imbeni wimbo huu tena, mkibadili “Mimi ni” kuwa “Ninyi ni” huku wakimuonesha mtu mwingine.”
Mafundisho na Maagano 76:5, 41–42, 69
Yesu Kristo ni Mwokozi wangu.
-
Zingatia kuigiza nafasi pamoja na watoto wako tukio ambalo kwalo mtu anauliza, “Ni kipi Yesu Kristo amenifanyia mimi?” Wewe na watoto wako mnaweza kutafuta majibu yamkini katika mstari wa 5, 41–42, au 69 katika sehemu ya 76. Mngeweza pia kuimba “He Sent His Son,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonesha shukrani zetu kwa kile Mwokozi alichofanya kwa ajili yetu?
Baba wa Mbinguni ananitaka nirudi kuishi na Yeye milele.
-
Wewe na watoto wako mngeweza kusoma na kutazama sehemu ndogo au yote ya “Sura ya 26: Falme Tatu za Mbinguni” (katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 97–103, au video inayohusiana nayo katika Maktaba ya Injili) na shirikini mmoja na mwingine kile mnachopenda kuhusu ono ambalo Joseph Smith alilipokea. Waruhusu watoto wako washiriki mawazo yao na hisia zao kuhusu vile ambavyo ingekuwa kuishi na Baba wa Mbinguni katika ufalme wa selestia.
-
Mngeweza pia kusoma Mafundisho na Maagano 76:62 na uwaalike watoto wako wachore picha zao wenyewe pamoja na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo katika ufalme wa selestia (ona ukurasa wa shughuli ya wiki hii).
Mafundisho na Maagano 76:12; 15–19; 114–16
Kujifunza maandiko kunaweza kunisaidia “nielewe mambo ya Mungu.”
-
Ungeweza kuwaalika watoto wako wasome mstari wa 15–19 ili kujua ni kipi Joseph Smith na Sidney Rigdon walikuwa wanafanya wakati walipoona ono katika Mafundisho na Maagano 76. Waambie watoto kuhusu wakati ambapo wewe ulipokea mwongozo wakati ukisoma maandiko, na waulize watoto wako kama wamewahi kupata uzoefu sawa na huo.