“Oktoba 19–25. 3 Nefi 27–4 Nefi: ‘Hakujakuwa na Watu Ambao Wangekuwa na Furaha Zaidi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Oktoba 19–25. 3 Nefi 27–4 Nefi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020
Oktoba 19–25
3 Nefi 27–4 Nefi
“Hakujakuwa na Watu Ambao Wangekuwa Na Furaha Zaidi”
Mwokozi aliwaamuru wanafunzi Wake kuandika mambo ambayo waliyapitia (ona 3 Nefi 27:23–24). Unapojifunza, andika uzoefu wa kiroho ulionao.
Andika Misukumo Yako
Mafunzo ya Yesu Kristo siyo tu falsafa nzuri ya kutafakari. Ni zaidi ya hiyo—yana lengo la kubadili maisha yetu. Kitabu cha 4 Nefi kinatoa mfano wa ajabu wa hili, kikionyesha jinsi kwa ukamilifu injili ya Mwokozi inavyoweza kubadili watu. Kufuatia huduma fupi ya Yesu, karne za mabishano kati ya Wanefi na Walamani ziliisha. Mataifa mawili yaliyojulikana kwa uasi na majivuno yalikuja kuwa “kitu kimoja, watoto wa Kristo” (4 Nefi 1:17), na “vitu vyao vyote vilitumiwa kwa usawa miongoni mwao” (4 Nefi 1:3). Mapenzi ya Mungu … yaliishi katika mioyo ya watu” na “hakujakuwa na watu ambao wangekuwan a furaha Zaidi ” miongoni mwa watu wote ambao waliumbwa na mkono wa Mungu” (4 Nefi 1:15–16). Hivi ndivyo mafunzo ya Mwokozi yalivyowabadili Wanefi na Walamani. Ni jinsi gani yanakubadili?
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi
Kanisa la Yesu Kristo linaitwa kwa jina Lake.
Wanafunzi wa Mwokozi walipokuwa wanaanzisha Kanisa Lake kote nchini, kuliibuka swali kwamba, kwa baadhi, linaweza kuonekana kama hoja ndogo—nini lilingekuwa jina la Kanisa? (ona 3 Nefi 27:1–3). Unajifunza nini kuhusu umuhimu wa jina hili kutokana na jibu la Mwokozi katika 3 Nefi 27:4–12? Mnamo 1838 Bwana alifunua jina la Kanisa Lake leo hii (ona MM 115:4). Tafakari kila neno katika jina hilo. Ni jinsi gani maneno haya yanatusaidia sisi kujua ni akina nani, nini tunaamini, na jinsi tunavyopaswa kutenda?
Ona pia Russell. M. Nelson, “Jina Sahihi la Kanisa,” Ensign au Liahona, Nov. 2018, 87–80; M. Russell Ballard, “Umuhimu wa Jina,” Ensign au Liahona, Nov. 2011, 79–82.
Ninaposafisha tamaa zangu, ninakuwa mwanafunzi mwaminifu zaidi.
Ungesema nini kama Mwokozi angekuuliza, kama alivyowauliza wanafunzi wake, “Ni kitu gani ambacho mnatamani Kwangu?” (3 Nefi 28:1). Fikiria kuhusu hili unaposoma kuhusu uzoefu wa wanafunzi wa Mwokozi katika 3 Nefi 28:1–11. Unajifunza nini kuhusu tamaa za mioyo ya wanafunzi kutokana na majibu yao kwa swali Lake? Rais Dallin H. Oaks alifundisha: Ili tuweze kuifikia takdiri yetu ya milele, tutamani na kufanyia kazi kwa ajili ya sifa zinazohitajika kuwa kiumbe cha milele. … Tutatamani kuwa kama [Yesu Kristo]” (“Tamaa,” Ensign au Liahona, Mei 2011, 44–45). Unaweza kufanya nini kufanya tamaa za moyo wako ziwe zenye haki zaidi? (Kwa taarifa zaidi kuhusu “mabadiliko yaletwe kwenye miili ” ya wanafunzi watatu, ona 3 Nefi 28:37 na “Viumbe Waliobadilishwa,” Mwongozo wa Maandiko, scriptures.ChurchofJesusChrist.org.)
Kuongoka kwa Yesu Kristo na injili Yake kunapelekea kwenye umoja na furaha.
Unaweza kufikiria jinsi ambavyo ingekuwa kuishi katika miaka iliyofuatia ziara ya Mwokozi? Ni jinsi gani watu walidumisha amani hii takatifu kwa muda mrefu—takriban miaka 200? Unapojifunza 4 Nefi 1:1–18, fikiria kuweka alama au kuandika chaguzi ambazo watu walifanya ili waweze kupata maisha haya yaliyobarikiwa.
Tafakari kile unachoweza kufanya kuisaidia familia yako, kata, au jumuia kuishi katika umoja mkubwa zaidi na furaha, kama watu katika 4 Nefi walivyofanya. Ni mafundisho gani ya Yesu Kristo unayoweza kuishi kikamilifu zaidi ili kukamilisha lengo hili? Kitu gani unaweza kufanya kuwasaidia wengine kuelewa na kuishi mafunzo haya?
Uovu unaongoza kwenye mgawanyiko na huzuni.
Kwa huzuni, jamii ya Sayuni iliyoelezwa katika 4 Nefi (ona pia Musa 7:18) hatimaye haikufumuliwa. Unaposoma 4 Nefi 1:19–49, tafuta mitazamo na tabia zilizosababisha jumuia hii kuvunjika. Je, unaona alama zozote za mitazamo hii au tabia ndani yako?
Ona Pia “Sura ya 18: Jihadhari na Majivuno,” Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Ezra Taft Benson (2014), 229–40.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani
Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.
3 Nefi 27:13–21
Mistari hii inaweza kuwasaidia wanafamilia kuelewa vyema kile Mwokozi alichomaanisha alipozungumzia “injili yangu.” Baada ya kusoma na kujadiliana mistari hii, unaweza kuomba kila mwanafamilia kutoa muhtasari wa injili ni nini katika sentensi moja.
3 Nefi 27:23–26
Tunafanya vipi katika kuandika vitu ambavyo “tumeviona na kusikia”—kibinafsi au kama familia? Kwa nini ni muhimu kuweka kumbukumbu ya vitu vya kiroho?
3 Nefi 27:30–31
Kuwasaidia wanafamilia kuelewa furaha Mwokozi aliyoeleza katika mistari hii, mnaweza kucheza mchezo ambapo wanafamilia wanajificha na wanafamilia wengine wanajaribu kuwatafuta. Hii inaweza kuelekeza kwenye mazungumzo kuhusu kwa nini ni muhimu kutafuta kila mwanafamilia ili “kusiwe na mmoja wao aliyepotea.” Tunawezaje kuwasaidia wanafamilia wetu kubaki imara katika injili au kurudi ikiwa wameondoka?
3 Nefi 28:17–18, 36–40
Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Mormoni wakati hakuelewa kila kitu kuhusu mabadiliko ambayo yalitokea kwa wanafunzi watatu Wanefi? Ni kipi tunaweza kufanya wakati hatuelewi kila kitu kuhusu kanuni ya injili? Rais Dieter F.Uchtdorf alifundisha: “Mungu anawajali ninyi. Atasikiliza na Atajibu maswali yako binafsi. Majibu kwa sala zenu yatakuja katika njia Yake mwenyewe na kwa wakati Wake mwenyewe, na kwa hiyo, mnahitaji kujifunza kusikiliza sauti Yake.” (“Kupokea Ushuhuda wa Nuru na Kweli,” Ensign au Liahona, Nov. 2014, 21).
4 Nefi 1:15
Kupunguza mabishano nyumbani mwenu, pengine wanafamilia wanaweza kuweka lengo kuwa wenye upendo zaidi wenyewe kwa wenyewe wiki hii. Baada ya wiki kukamilika, fanya mapitio ya maendeleo yenu pamoja na mjadiliane jinsi kuonyesha upendo zaidi kulivyoathiri familia yenu.
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.