Agano la Kale 2022
Novemba 14–20. Amosi; Obadia: “Mtafuteni Bwana, Nanyi Mtaishi”


“Novemba 14–20. Amosi; Obadia: ‘Mtafuteni Bwana, Nanyi Mtaishi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Novemba 14–20. Amosi; Obadia,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
uso wa Yesu ulioangazwa na mishumaa kwenye chumba cha giza

Mkate wa Uzima, na Chris Young

Novemba 14–20

Amosi; Obadia

“Mtafuteni Bwana, Nanyi Mtaishi”

Roho Mtakatifu anaweza kufungua akili na moyo wako kwa jumbe katika neno la Mungu ambazo zimekusudiwa kwa ajili yako tu. Unahisi ni nini Bwana anakutaka wewe ujifunze wiki hii?

Andika Misukumo Yako

Mungu alichagua uzao wa Ibrahimu kuwa watu wake wa agano ili wawe “baraka” kwa watu wote (ona Mwanzo 2:6–16). Lakini badala yake, wakati wa huduma ya Amosi, watu wengi wa agano walikuwa wakikandamiza maskini na kuwapuuza manabii, wakifanya matendo yao ya ibada kuwa matupu na yasiyo na maana (ona Amosi 2:6–16). Kweli, mataifa yaliyowazunguka pia walikuwa na hatia ya dhambi kubwa (ona Amosi 1; 2:1–5), lakini hiyo haijawahi kuwa kisingizio kwa watu wa Mungu (ona Amosi 3:2). Kwa hivyo Mungu alimtuma mchungaji kutoka Yuda aliyeitwa Amosi kuhubiri toba kwa Ufalme wa Israeli. Baadaye, Mungu pia alitangaza kupitia nabii Obadia kwamba ingawa Ufalme wa Yuda ulikuwa umeharibiwa, Bwana atakusanya na kuwabariki watu wake tena. Watu wa agano walikuwa wamepotea kutoka kwa Bwana, manabii wote walishuhudia, lakini hawatatupiliwa mbali milele. Wakati Mungu anafunua siri zake kwa watumishi wake manabii (ona Amosi 3:7), tunaweza kuchukua kama ishara kwamba bado anataka kutusaidia kuishi kulingana na maagano ambayo tulifanya Naye.

Kwa habari zaidi kuhusu vitabu vya Amosi na Obadia, ona “Amosi” na “Obadia” katika Kamusi ya Biblia.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Amosi 3:1–8; 7:10–15

Bwana hufunua kweli kupitia manabii Wake.

Katika Amosi 3:3–6, nabii Amosi aliwasilisha mifano kadhaa ya sababu na athari: kwa sababu simba hupata mawindo, simba hunguruma; kwa sababu mtego uliowekewa ni kwa ajili ya ndege, ndege huyo akanaswa. (Kumbuka kuwa katika Tafsiri ya Joseph Smith ya mstari wa 6, neno “tayari” lilibadilishwa kwenda “kujulikana” [katika Amosi 3:6, tanbihi ya chinib].) Katika mstari wa 7–8, Amosi alitumia mantiki hii kwa manabii. Ni nini husababisha nabii atabiri? Unajifunza nini zaidi kuhusu manabii unaposoma Amosi 7:10–15? Tafakari kwa nini unashukuru kwamba Bwana bado “anafunua siri yake kwa watumishi wake manabii” (Amosi 3:7). Je! Ukweli huu unapendekeza nini kwako juu ya Mungu?

Ona pia Mafundisho na Maagano 1:38; 21:4–8; 35:13–14.

Amosi 4–5

“Mtafuteni Bwana, Nanyi Mtaishi.”

Unaposoma Amosi 4:6–13, angalia hukumu ambazo Bwana alikuwa amewatolea watu wa Israeli. Je! vifungu hivi vinaonyesha nini juu ya kile ambacho Bwana alitarajia kitatokea baada ya kila uzoefu? (ona pia Helamani 12:3). Fikiria kuhusu jaribio la hivi karibuni ulilolipata. Wakati jaribu lako linaweza kuwa halijatumwa na Mungu, tafakari jinsi linavyoweza kukupa fursa za kumtafuta Yeye.

Soma Amosi 5:4, 14–15, na utafakari jinsi Bwana amekuwa “mwenye neema” (mstari wa 15) kwako jinsi ulivyomtafuta, hata wakati wako wa majaribu.

Ona pia Donald L. Hallstrom, “Mgeukie Bwana,” Ensign au Liahona, Mei 2010, 78–80.

Amosi 8:11–12

Neno la Bwana linaweza kukidhi njaa na kiu ya kiroho.

Sisi sote tunapata vipindi vya njaa na kiu kiroho, lakini hakuna haja ya sisi “kutangatanga kutoka bahari hadi bahari” (Amosi 8:12) kutafuta kitu cha kuturidhisha. Tunajua ni nini kitakidhi njaa hiyo ya kiroho, na tumebarikiwa na neno la Bwana kwa wingi. Unaposoma Amosi 8:11–12, fikiria kwa nini njaa ni mlinganisho mzuri wa kuishi bila neno la Mungu. Je! Unapata umaizi gani wa ziada katika Mathayo 5:6; Yohana 6:26–35; 2 Nefi 9:50–51; 32:3; Enoshi 1:4–8?

Ona pia Jeffrey R. Holland, “Wenye Njaa Amewasababisha Mema,” Ensign, Nov. 1997, 64–66; Gospel Topics, “Ukengeufu,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

Picha
kikundi cha vijana kimesimama mbele ya hekalu

Tunaweza kuwa waokozi kwenye Mlima Sayuni kwa kufanya kazi ya hekalu na historia ya familia.

Obadia 1:21.

Ni nani ndiyo “waokozi … juu ya mlima Sayuni”?

Rais Gordon B. Hinckley alitoa tafsiri moja inayowezekana ya kifungu “waokozi juu ya mlima Sayuni,” akiunganisha kifungu hicho na kazi ya historia ya familia: “[Hekaluni] tunakuwa waokozi kwenye Mlima Sayuni. Hii inamaanisha nini? Kama vile Mkombozi wetu alivyoyatoa maisha Yake kama dhabihu ya uhai kwa watu wote, na kwa kufanya hivyo akawa Mwokozi wetu, hata hivyo sisi, kwa kiwango kidogo, tunapofanya kazi ya wakala hekaluni, tunakuwa kama waokozi kwa wale wengine upande ambao hawana njia ya kusonga mbele isipokuwa kama kuna kitu kimefanywa kwa niaba yao na wale walio duniani” (“Maneno ya Kufunga,” Ensign au Liahona, Nov. 2004, 105).

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Amosi 3:7Unaweza kupitia ujumbe kadhaa wa hivi karibuni kutoka kwa Rais wa Kanisa na kujadili kile Bwana anafunua kwa familia yako kupitia kwake. Kwa nini ni muhimu kuwa na nabii kuliongoza Kanisa? Ni kwa jinsi gani tumekuja kujua ni nabii wa kweli? Tunafanya nini ili kufuata ushauri wake?

Amosi 5:4Familia yako inaweza kuunda bango la kutundika nyumbani kwako likiwa na mstari huu. Inamaanisha nini kumtafuta Bwana? Tunamtafutaje? Ni baraka zipi tunazozipokea wakati tunapofanya hivyo? Unaweza kualika wanafamilia kushiriki na kujadili vifungu vingine ambavyo vinafundisha juu ya kumtafuta Bwana, kama vile Mathayo 7:7–8; Etheri 12:41; na Mafundisho na Maagano 88:63.

Amosi 8:11–12.Watoto wanaweza kufurahia kufanya vitendo vinavyoendana na vifungu katika mistari hii. Wakati miili yetu ina njaa au kiu, tunafanya nini? Wakati roho zetu zina njaa au kiu, tunafanya nini? Unaweza pia kutazama video “Great Apostasy” (ChurchofJesusChrist.org) na uzungumze juu ya jinsi Urejesho wa Injili unavyokidhi njaa yetu ya kiroho.

Obadia 1:21.Inaweza kumaanisha nini kuwa “waokozi … juu ya mlima Sayuni”? (Kwa mojawapo ya maelezo yanayowezekana, ona taarifa ya Rais Gordon B. Hinckley katika “Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko.”) Ni yupi kati ya mababu zetu anayehitaji ibada za kuokoa? Je, tutafanya nini ili kuwasaidia?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “We Thank Thee, OGod, for a Prophet,” Nyimbo za Kanisa, na.221.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Tumia Muziki Kumwalika Roho Mtakatifu na kujifunza mafundisho. Kusikiliza au kusoma wimbo kunaweza kukusaidia kujifunza kanuni za injili. Kwa mfano, unaweza kusikiliza au kusoma “We Thank Thee, O God, for a Prophet” (Nyimbo za Kanisa, na.19) kuhamasisha imani kubwa kwa manabii walio hai. (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 22.)

Picha
Hekalu la Santo Domingo Dominican Republic

Hekalu la Santo Domingo Dominican Republic

Chapisha