“Januari 17–23. Mwanzo 5; Musa 6: ‘Wafundisheni Vitu Hivi Watoto Wenu kwa Uwazi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)
“Januari 17–23. Mwanzo 5; Musa 6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022
Januari 17–23
Mwanzo 5; Musa 6
“Wafundisheni Vitu Hivi Watoto Wenu kwa Uwazi”
Maandalizi yako ya kufundisha yanaanza unaposoma Mwanzo 5 na Musa 6. Unapofanya hivyo, sikiliza hisia kutoka kwa Roho Mtakatifu juu ya kile watoto wanahitaji kujifunza.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Kwenye karatasi, andika maneno kadhaa muhimu ambayo yangesaidia watoto kukumbuka kitu walichojifunza nyumbani wiki hii au kwenye somo la awali la Msingi. Pasipo utaratibu malum acha watoto wachukue nafasi ya kuchagua neno. Baada ya neno kuchaguliwa, mwalike yeyote wa watoto kushiriki jambo ambalo wamejifunza kuhusiana na neno hilo.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Mungu anaweza kunisaidia kufanya mambo magumu.
Wakati Henoko alipoitwa kuhubiri injili, alihofu kwamba atashindwa. Lakini Mungu alimsaidia kutenda vitu vikubwa.
Shughuli Yamkini
-
Waombe watoto kushiriki wakati ambao waliombwa kufanya kitu ambacho ni kigumu au cha kutisha kwao. Shiriki hadithi ya Henoko alipoitwa kuwa nabii, inapatikana katika Musa 6:27, 31–34 (ona pia “Henoko Nabii,” katika Hadithi za Agano la Kale). Sisitiza kwamba ingawa Henoko hakuhisi kuwa tayari kuitwa kuwa nabii, Mungu aliahidi kumsaidia. Wasaidie watoto kuelewa baadhi ya njia ambazo Mungu anatusaidia wakati tunapoombwa kufanya mambo magumu.
-
Shiriki mifano kadhaa ya maandiko ya wakati Mungu alipowasaidia watu kufanya mambo magumu—kwa mfano, Nuhu akijenga safina, Daudi alipigana na Goliati, Amoni akitetea kundi la mifugo la mfalme, au Samweli Mlamani akihubiri. (Kwa ajili ya picha na marejeleo ya maandiko, ona Kitabu Cha Sanaa ya Injili, na. 7, 19, 78, 81.) Shiriki uzoefu wa wakati ambapo Mwokozi alikusaidia kufanya jambo gumu.
Injili inanifundisha mimi jinsi ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni.
Mungu alimfundisha Adamu tunachohitaji kufanya ili kurudi Kwake— kuwa na imani, kutubu, kubatizwa, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujifunza vitu hivi?
Shughuli Yamkini
-
Tafuta au chora picha kuwakilisha imani, toba, ubatizo, na kipawa cha Roho Mtakatifu (tazama ukurasa wa shughuli wa wiki hii). Weka picha katika mstari unaoongoza kwenye picha ya Yesu Kristo. Soma Musa 6:52 kwa watoto, na uwaombe wasimame karibu na picha sahihi wanaposikia maneno ambayo picha inawakilisha (katika aya hii, neno “amini” linatumika kwa ajili ya neno “imani” ).
-
Imba nyimbo ambazo zinafundisha kanuni katika Musa 6:52, kama vile “Faith,” “Help Me, Dear Father” (verse 2), “When I Am Baptized,” and “The Holy Ghost” (Children’s Songbook, 96–97, 99, 103, 105). Wasaidie watoto kuelewa kuwa kufanya vitu vilivyofundishwa kwenye nyimbo kutatusaidia kurudi kwa Baba wa Mbinguni.
Baba wa Mbinguni anawataka wazazi kuwafundisha watoto wao.
Kuanzia wakati wa Adamu na Hawa, wazazi wameamriwa kuwafundisha watoto wao injili. Unawezaje kuhamasisha watoto kusikiliza na kufuata mafundisho mema ya wazazi wao?
Shughuli Yamkini
-
Soma Musa 6:58 kwa watoto, na uonyeshe picha ya familia ya Adamu na Hawa katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Wasaidie watoto kurudia msemo “Wafundisheni Watoto Wenu kwa Uwazi” Eleza kwamba Mungu anataka wazazi wote kufuata mfano wa Adamu na Hawa kwa kuwafundisha watoto wao juu ya Yesu Kristo na injili Yake. Waulize watoto nini wanaweza kufanya wakati wazazi wao au wengine wanawafundisha injili.
-
Wasaidie watoto kulinganisha picha zao na wazazi wao au picha za wanyama watoto na wanyama wakubwa. Wazazi wanawasaidiaje watoto wao? Wanawafundisha nini? Waombe watoto kuchora picha za familia zao nyakati ambazo wazazi hufundisha watoto, kama kusoma maandiko pamoja, kusali pamoja, au kula pamoja.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Mungu anaweza kunisaidia kufanya mambo magumu.
Hata hivyo Henoko alihisi hastahili, Mungu alimsaidia kutimiza wito wake kama nabii. Mungu pia anaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kufanya mambo magumu.
Shughuli Yamkini
-
Soma Musa 6:26–34 pamoja na watoto. Kwa nini Henoko alihisi kuwa hangeweza kuhubiri injili? (ona Musa 6:31). Je!, Mungu alimsaidiaje Henoko? (ona Musa 6:32–34; 7:13).
-
Waalike watoto kutaja mambo kadhaa magumu ambayo watoto wa rika zao hufanya wakati mwingine (kama vile kumaliza kazi za shule, kuwa mkarimu kwa mtu ambaye hana fadhili, au kusema ukweli wakati wamefanya makosa). Wasaidie watoto kupata misemo katika Musa 6:32–34 ambayo inaweza kuwasaidia wao. Waombe watoto washiriki uzoefu wao wakati Mungu alipowasaidia mambo magumu. Pia shiriki uzoefu wako mwenyewe.
Imani, toba, ubatizo na kupokea Roho Mtakatifu kunaniandaa mimi kurudi kwa Mungu.
Adamu na Henoko waliwafundisha watu wao kanuni na maagizo ya kwanza ya injili: imani, toba, Ubatizo, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu (tazama pia Makala za Imani 1:4). Je, unaweza kufanya nini kuwasaidia watoto kuelewa umuhimu wa kanuni na maagizo haya katika maisha yao?
Shughuli Yamkini
-
Waombe watoto kusoma Musa 6:52, 57 ili kupata kanuni na maagizo ya injili yaliyotajwa katika makala ya nne ya imani.
-
Andika makala ya nne ya imani kwenye ubao, na uwaalike watoto kuisoma. Kisha futa neno moja au mawili, na uwaombe wasome tena, wakijaza maneno yaliyokosekana kutoka kwenye kumbukumbu. Rudia mchakato huu hadi watoto wajifunze makala ya imani.
-
Waalike watoto waandike hotuba fupi juu ya imani, toba, ubatizo, au kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, kitu ambacho wangeshiriki na familia zao. Kila hotuba inaweza kujumuisha andiko, uzoefu, na ushuhuda. Hotuba inaweza pia kuelezea jinsi kanuni inavyotusaidia kurudi kwa Baba wa Mbinguni.
Wazazi wanawajibika kuwafundisha watoto wao.
Mungu anawamini wazazi kuwa waalimu wa msingi wa injili katika familia zao. Unawezaje kuwahamasisha watoto kuwasaidia wazazi wao katika jukumu hili?
Shughuli Yamkini
-
Muombe mtoto asome Musa 6:58. Ni amri gani ambayo Baba wa Mbinguni aliwapa wazazi katika aya hii? Onyesha picha ya Adamu na Hawa wakiwafundisha watoto wao (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia), na acha watoto washiriki kile wanachofahamu kuhusu hadithi hii. Wahimize wazungumzie juu ya kweli za injili walizojifunza kutoka kwa familia zao.
-
Wasaidie watoto kuandika maandishi ya shukrani kwa wazazi wao au panga njia zingine rahisi za kuonyesha shukrani zao kwa wazazi wao. Imbeni wimbo kuhusu familia, kama vile “Love Is Spoken Here” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 190–91). Tunawezaje kuwasaidia wazazi wetu kuunda mazingira ya upendo katika nyumba zetu?
Himiza Kujifunza Nyumbani
Unawezaje kuwasaidia watoto kuendelea kujifunza nje ya darasa? Unaweza kuwahamasisha kukumbuka hadithi ya Henoko wakati wanapokumbana na kitu kigumu wiki hii.