“Malaika Wanarejesha Ukuhani,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Malaika Wanarejesha Ukuhani,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
1829
Malaika Wanarejesha Ukuhani
Uwezo wa kufanya kazi ya Mungu
Kadiri Joseph na Oliver walipotafsiri mabamba ya dhahabu, walijifunza kwamba Yesu alitaka kila mtu abatizwe. Pia aliwapa watu uwezo wa kuwabatiza wengine. Joseph hakuwa amebatizwa. Alitaka kujua mengi zaidi kuhusu ubatizo.
Joseph Smith—Historia ya 1:68; Saints, 1:65–66
Joseph na Oliver walijiuliza ni nani alikuwa na uwezo wa kuwabatiza watu sasa. Waliamua kumuuliza Mungu. Walienda msituni na kupiga magoti katika sala.
Joseph Smith—Historia ya 1:68; Saints, 1:66
Walipokuwa wakisali, malaika alitokea. Alisema alikuwa Yohana Mbatizaji, aliyembatiza Yesu Kristo zamani za kale. Aliwapa Joseph na Oliver Ukuhani wa Haruni. Ukuhani ni uwezo wa Mungu. Unatumika kuwabariki watoto wa Mungu.
Mafundisho na Maagano 13; Joseph Smith—Historia ya 1:69, 72; Saints, 1:66–67
Yohana Mbatizaji alisema kwamba mtu mwenye Ukuhani wa Haruni anaweza kuwafundisha watu kutubu na kuwabatiza. Yohana aliwaambia Joseph na Oliver wabatizwe. Walikwenda kwenye mto na kubatizana. Walipotoka majini, walijazwa na Roho Mtakatifu. Walikuwa na furaha sana!
Joseph Smith—Historia ya 1:70–73
Baadaye, malaika wengine walikuja. Watatu kati ya Mitume wa Yesu—Petro, Yakobo, na Yohana—waliwapa Joseph na Oliver Ukuhani wa Melkizedeki. Sasa Joseph na Oliver wangeweza kutoa kipawa cha Roho Mtakatifu. Joseph na Oliver pia wakawa Mitume. Wangeweza kuliongoza Kanisa na kuwa mashahidi maalumu wa Yesu Kristo.
Mafundisho na Maagano 27:12; Saints, 1:84