“Wasaidie Mababu Kupokea Ibada Takatifu,” Njia Yangu ya Agano (2020)
“Wasaidie Mababu Kupokea Ibada Takatifu,” Njia Yangu ya Agano
Wasaidie Mababu Kupokea Ibada Takatifu
Baba wa Mbinguni anawapenda wanafamilia wako ambao wamefariki na amewaandalia njia ya wao kupokea baraka za injili kupitia hekalu.
-
Jifunze kuhusu umuhimu wa familia na mahekalu. Fikiria kutumia:
-
“Historia ya Familia ni Nini?,” “Ninawezaje Kuanzisha Historia ya Familia Yangu na Huduma ya Hekalu?,” na “Mababu Zangu” katika Familia na Mahekalu, 15–19.
-
-
Kwa sala mtambue babu mmoja au zaidi wa jinsia sawa na yako yule ambaye ungependa kumhudumia hekaluni.
-
Jifunze jinsi ya kujiandaa kwa urahisi na kuchapisha kadi ya jina la familia unayoweza kuipeleka hekaluni. Fikiria kutumia:
-
Msaada wa Jina la Familia (familysearch.org/family-name-assist). Ili kutumia kifaa hiki, utahitaji namba yako ya kumbukumbu ya uumini wa Kanisa. Nambari yako ya kumbukumbu inapatikana kwenye kibali chako cha hekaluni, au unaweza kuipata namba yako ya kumbukumbu kutoka kwa karani wako wa kata.
-
-
Ikiwezekana, weka miadi ya kuhudhuria hekaluni pamoja na familia, marafiki, na waumini wa kata ili kufanya ubatizo kwa niaba ya mababu zako waliofariki. Unaweza kwenda ChurchofJesusChrist.org/temple/schedule/appointment na kuingia kwa kutumia akaunti yako ya Kanisa ili kupanga miadi.