“Boresha Kujifunza Injili,” Njia Yangu ya Agano (2020)
“Boresha Kujifunza Injili,” Njia Yangu ya Agano
Boresha Kujifunza Injili
Ni muhimu kusali na kujifunza maandiko kila mara, binafsi na pamoja na familia yako (kama inawezekana). Unapofanya hivyo, utamhisi Roho na kupata mwongozo katika maisha yako ya kila siku.
-
Jifunze kuhusu ksonga karibu zaidi na Mwokozi kupitia kujifunza maandiko na sala kila siku. Fikiria kutumia:
-
Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani. Nyenzo hii inaweza kuwa mwongozo katika kujifunza kwako maandiko kila siku.
-
“Sali Kila Mara” na “Jifunze Maandiko” katika Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Kushiriki Injili ya Yesu Kristo (2023), 77–79.
-
-
Ikiwa bado hujapakua , pakua aplikesheni ya Maktaba ya Injili au nenda kwenye ChurchofJesusChrist.org ili kupata hotuba, makala, video na mengine zaidi. Kama unatumia kifaa cha Android, unaweza kupakua aplikesheni hii kutoka Google Play store. Kama unatumia kifaa cha iOS, unaweza kupakua aplikesheni hii kutoka kwenye Apple App Store.
-
Majarida ya Kanisa yanaweza kukusaidia umfuate Mwokozi kama muumini wa Kanisa Lake.
-
Kuna majarida matatu ya Kanisa: gazeti la Liahona kwa ajili ya watu wazima, Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana kwa ajili ya vijana, na gazeti la Rafiki kwa ajili ya watoto. Unaweza kuyapata kidigitali bila malipo katika sehemu ya “Majarida” katika Gospel Library. Kama wewe ni muumini mpya na ungependelea nakala ya jarida lililochapishwa, wasiliana na askofu au rais wako wa tawi ili upate majarida ya mwaka mzima bure.
-
-
Kama wewe ni kijana mkubwa kati ya miaka 18 na 30, jifunze kuhusu chuo kwa kusoma “The Purpose of Institute” kwenye ChurchofJesusChrist.org na jifunze kuhusu Vijana Kila Wiki katika Maktaba ya Injili.
-
Azimia kujifunza maandiko kila siku, hasa kutoka katika Kitabu cha Mormoni, na sala (ona Matendo ya Mitume 17:11).