Kuwaimarisha Waumini Wapya
Pokea Endaumenti Yako


“Pokea Endaumenti yako,” Njia Yangu ya Agano (2020)

“Pokea Endaumenti Yako,” Njia Yangu ya Agano

Picha
watu wakiwa hekaluni

Pokea Endaumenti Yako

Ikiwa wewe ni mtu mzima, mara baada ya kuwa muumini kwa mwaka mmoja, unaweza kupata kibali cha hekaluni ambacho kinakuruhusu kushiriki katika ibada za ziada za hekaluni. Hekaluni utapokea ibada iitwayo endaumenti. Katika ibada ya endaumenti, utajifunza zaidi kuhusu injili ya Yesu Kristo na kualikwa kufanya maagano matakatifu na Baba yako wa Mbinguni. Kushika maagano haya kutaleta shangwe kubwa zaidi na nguvu za kiungu katika maisha yako. Baada ya kuwa umepata endaumenti, unaweza kuipokea ibada hii kwa niaba ya mababu zako.

  • Jifunze juu ya endaumenti na umuhimu wa mahekalu. Fikiria kutumia:

    • About the Temple Endowment,” temples.ChurchofJesusChrist.org.

    • How Can My Family Return to Live with God?,” “What Is the Purpose of the Temple?,” na “What Is the Temple Endowment?” katika Families and Temples, 2–5, 9–10, 21.

    • Prepare for the House of the Lord,” temples.ChurchofJesusChrist.org.

  • Unapokaribia kumbukumbu ya mwaka mmoja ya ubatizo wako, anza kuhudhuria madarasa ya maandalizi ya kwenda hekaluni. Panga usahili na askofu ili kupokea kibali cha hekaluni.

  • Panga tarehe na watu wa hekaluni ili ukapokee endaumenti yako.

Chapisha