“Jifunze kuhusu Ukuhani wa Haruni na Programu ya Wavulana,” Njia Yangu ya Agano (2020)
“Jifunze kuhusu Ukuhani wa Haruni na Programu ya Wavulana,” Njia Yangu ya Agano
Jifunze kuhusu Ukuhani wa Haruni na Programu ya Wavulana
Ukuhani ni uwezo na mamlaka ya Mungu yaliyotolewa kwa watumishi Wake duniani na hutumiwa kuwabariki watoto Wake, wote wanawake na wanaume. Wanaume wanaostahili wa umri wa miaka 11 na zaidi wanaweza kupokea Ukuhani wa Haruni ndani ya wiki moja baada ya kuthibitishwa. Wanapoendelea katika njia ya agano, wanaume wanaostahili wanaweza kupokea Ukuhani wa Melkizedeki.
-
Jifunze kuhusu mamlaka ya ukuhani na jinsi waumini wote wanavyobarikiwa kwa ukuhani. Ikiwa wewe ni mwanaume, zingatia sana maagano na majukumu yanayohusiana na Ukuhani wa Haruni na jinsi gani programu ya Wavulana inavyofanya kazi. Fikiria kutumia:
-
“Inamaanisha Nini Kutawazwa katika Ukuhani?” katika Familia na Mahekalu (kijitabu cha, 2016), 5–6.
-
“Kiapo na Agano la Ukuhani Linahusika kwa Wanawake,” ChurchofJesusChrist.org,
-
“Akidi za Ukuhani wa Haruni,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 10.1, ChurchofJesusChrist.org.
-
Urejesho wa Injili ya Yesu Kristo (kijitabu, 2008).
-
Mwongozo wa Utangulizi kwa Watoto na Vijana wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho (2019), ikiwa kinapatikana.
-
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo kwa ajili ya Kufanya Chaguzi (2022).
-
-
Ikiwa wewe ni mwanaume na una umri wa miaka 11 au zaidi, zungumza na askofu au katibu wake ili kuandaa usaili ili upokee Ukuhani wa Haruni.