10. Kanaani Nyakati za Agano la Kale
-
Dani (Laishi) Yeroboamu alimsimamisha ndama wa dhahabu kwa ajili ya kuabudiwa na Ufalme wa Kaskazini (1 Fal. 12:26–33). Dani ulikuwa ni mpaka wa Kaskazini wa Israeli ya Kale.
-
Mlima Karmeli Eliya alipambana na manabii wa Baali na akafungua mbingu ili mvua inyeshe (1 Fal. 18:17–46).
-
Megido Mahali pa mapambano mengi (Amu. 4:13–16; 5:19; 2 Fal. 23:29; 2 Nya. 35:20–23). Sulemani alianzisha ushuru ili kuijenga Megido (1 Fal. 9:15). Mfalme Yosia wa Yuda alijeruhiwa vibaya sana katika pambano dhidi ya Farao Neko wa Misri (2 Fal. 23:29–30). Wakati wa Ujio wa Pili wa Bwana pigano kuu la mwisho litafanyika katika Bonde la Yezereeli kama sehemu ya pambano la Armagedoni (Yoe. 3:14; Ufu. 16:16; 19:11–21). Jina la Armagedoni ni nukuu ya Kiyunani kutoka Har-megidoni, Kiebrania, au Mlima wa Megido.
-
Yezereeli Jina la mji katika bonde lililo kubwa zaidi na lenye rutuba sana la Israeli lenye jina hilo hilo. Wafalme wa Ufalme wa Kaskazini walijenga Kasri mahali hapa (2 Sam. 2:8–9; 1 Fal. 21:1–2). Malkia mwovu Yezebeli aliishi na kufa hapa (1 Fal. 21; 2 Fal. 9:30).
-
Beth-sheani Waisraeli walipambana na Wakanaani hapa (Yos. 17:12–16). Mwili wa Sauli ulikomewa kwenye kuta za ngome hii (1 Sam. 31:10–13).
-
Dothani Yusufu aliuzwa utumwani na kaka zake (Mwa. 37:17, 28; 45:4). Elisha alipata ono la mlima uliojaa farasi na magari yanayokokotwa na farasi wa moto (2 Fal. 6:12–17).
-
Samaria Mji mkuu wa Ufalme wa Kaskazini (1 Fal. 16:24–29). Mfalme Ahabu alimjengea hekalu Baali (1 Fal. 16:32–33). Eliya na Elisha walihudumu hapa (1 Fal. 18:2; 2 Fal. 6:19–20). Katika mwaka 721 K.K. Waashuru waliuteka, wakimalizia kukamata yale makabila kumi (2 Fal. 18:9–10).
-
Shekemu Ibrahimu alijenga madhabahu hapa (Mwa. 12:6–7). Yakobo aliishi karibu na hapa. Simeoni na Lawi waliwaua kinyama wanaume wote wa mji huu (Mwa. 34:25). Ushawishi wa Yoshua wa “chagueni—leo” kumtumikia Mungu ulikuja katika Shekemu (Yos. 24:15). Hapa Yeroboamu alijenga mji mkuu wa kwanza wa ufalme wa Kaskazini (1 Fal. 12).
-
Mlima Ebali na Mlima Gerizimu Yoshua aliwagawa Israeli juu ya milima hii miwili—baraka za torati zilitangazwa kutoka Mlima Gerizimu, wakati laana ilikuwa kutoka Mlima Ebali (Yos. 8:33). Wasamaria baadaye walijenga hekalu juu ya Gerizimu (2 Fal. 17:32–33).
-
Penueli (Penieli) Hapa Yakobo alishindana mweleka usiku wote na mjumbe wa Bwana (Mwa. 32:24–32). Gideoni aliiangamiza ngome ya Wamidiani (Amu. 8:5, 8–9).
-
Yafa Yona alisafiri kwa meli kutoka hapa kuelekea Tarshishi ili kuepuka huduma yake kwa Ninawi (Yon. 1:1–3).
-
Shilo Katika wakati wa Waamuzi, mji mkuu wa Israeli na hema vilikuwa hapa (1 Sam. 4:3–4).
-
Betheli (Luzu) Hapa Ibrahimu alijitenga na Lutu (Mwa. 13:1–11) na akapata ono (Mwa. 13; Ibr. 2:19–20). Yakobo alipata ono la ngazi iliyofika mbinguni (Mwa. 28:10–22). Hema liliwekwa hapa kwa muda (Amu. 20:26–28). Yeroboamu alimsimamisha ndama wa dhahabu kwa ajili ya kuabudu ufalme wa Kaskazini (1 Fal. 12:26–33).
-
Gibeoni Watu wa Hiti kutoka hapa walimlaghai Yoshua kuingia mkataba (Yos. 9). Jua lilisimama tuli wakati Yoshua aliposhinda vita (Yos. 10:2–13). Hili pia lilikuwa eneo la muda la hema (1 Nya. 16:39).
-
Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Ekroni, Gathi (miji mitano ya Wafilisti) Kutoka katika miji hii Wafilisti mara kwa mara walifanya vita dhidi ya Israeli.
-
Bethlehemu Raheli alizikwa karibu ya hapa (Mwa. 35:19). Ruthu na Boazi waliishi hapa (Rut. 1:1–2; 2:1, 4). Uliitwa mji wa Daudi (Lk. 2:4).
-
Hebroni Ibrahimu (Mwa. 13:18), Isaka, Yakobo (Mwa. 35:27), Daudi (2 Sam. 2:1–4), na Absalomu (2 Sam. 15:10) waliishi hapa. Huu ulikuwa mji mkuu wa kwanza wa Yuda chini ya Mfalme Daudi (2 Sam. 2:11). Inaaminika kwamba Ibrahimu, Sara, Isaka, Rebeka, Yakobo, na Lea walizikwa hapa katika pango la Makpela (Mwa. 23:17–20; 49:31, 33).
-
Engedi Daudi alijificha kumkimbia Sauli na hivyo kuokoa maisha ya Sauli (1 Sam. 23:29–24:22).
-
Gerari Ibrahimu na Isaka waliishi hapa kwa muda (Mwa. 20–22; 26).
-
Beer-sheba Ibrahimu alichimba kisima hapa na alifanya agano na Abimaleki (Mwa. 21:31). Isaka alimwona Bwana (Mwa. 26:17, 23–24), na Yakobo aliishi hapa (Mwa. 35:10; 46:1).
-
Sodoma na Gomora Lutu alichagua kuishi Sodoma (Mwa. 13:11–12; 14:12). Mungu aliiangamiza Sodoma na Gomora kwa sababu ya uovu (Mwa. 19:24–26). Yesu baadaye aliitumia miji hii kama mifano ya uovu (Mt. 10:15).