11. Nchi Takatifu Nyakati za Agano Jipya
-
Tiro na Sidoni Yesu alilinganisha Korazini na Bethsaida kwa Tiro na Sidoni (Mt. 11:20–22). Alimponya binti wa mwanamke Myunani (Mt. 15:21–28).
-
Mlima wa Kugeuka Sura Yesu aligeuka sura mbele ya Petro, Yakobo, na Yohana, na wakapokea funguo za ufalme (Mt. 17:1–13). (Wengine wanaamini Mlima wa Kugeuka sura ni Mlima Hermoni, wengine wanaamini ulikuwa Mlima Tabori.)
-
Kaisaria Filipi Petro alitoa ushuhuda ya kuwa Yesu ndiye Kristo na aliahidiwa funguo za ufalme (Mt. 16:13–20). Yesu alitabiri kifo Chake mwenyewe na ufufuko Wake (Mt. 16:21–28).
-
Eneo la Galilaya Yesu alitumia sehemu kubwa ya maisha Yake na huduma Yakekatika Galilaya (Mt. 4:23–25). Hapa alitoa Mahubiri ya Mlimani (Mt. 5–7); alimponya mkoma (Mt. 8:1–4); na alichagua na kutawaza na kuwatuma Mitume Kumi na Wawili, ambao wote isipokuwa mmoja tu Yuda Iskarioti ndiye hakuwa Mgalilaya (Mk. 3:13–19). Katika Galilaya Kristo mfufuka aliwatokea Mitume (Mt. 28:16–20).
-
Bahari ya Galilaya, baadaye iliitwa Bahari ya Tiberia Yesu alifundisha kutoka katika mashua ya Petro (Lk. 5:1–3) na akawaita Petro, Andrea, Yakobo, na Yohana kuwa wavuvi wa watu (Mt. 4:18–22; Lk. 5:1–11). Pia aliinyamazisha dhoruba (Lk. 8:22–25), alifundisha kwa mifano kwenye mashua (Mt. 13), alitembea juu ya bahari (Mt. 14:22–32), na akawatokea wanafunzi Wake baada ya ufufuko Wake (Yn. 21).
-
Bethsaida Petro, Andrea, na Filipo walizaliwa katika Bethsaida (Yn. 1:44). Yesu alienda zake kwa siri pamoja na Mitume karibu na Bethsaida. Makutano wakamfuata, naye akawalisha watu 5,000 (Lk. 9:10–17; Yn. 6:1–14). Hapa Yesu alimponya mtu aliyekuwa kipofu (Mk. 8:22–26).
-
Kapernaumu Hapa palikuwa ndiyo nyumbani kwa Petro (Mt. 8:5, 14). Katika Kapernaumu ambako Mathayo alipaita “mji wake” Yesu. Yesu alimponya mtu aliyepooza (Mt. 9:1–7; Mk. 2:1–12), alimponya mtumishi wa akida na alimponya mama wa mkwe wa Petro (Mt. 8:5–15), alimwita Mathayo kuwa mmoja wa Mitume Wake (Mt. 9:9), alifungua macho yaliyopofuka, alimfukuza ibilisi (Mt. 9:27–33), aliponyesha mkono wa mtu ulionyauka katika siku ya sabato (Mt. 12:9–13), alitoa mahubiri ya mkate wa uzima (Yn. 6:22–65), alikubali kulipa kodi, akimwambia Petro kupata fedha hiyo kutoka kinywa cha samaki (Mt. 17:24–27).
-
Magdala Hapa palikuwa nyumbani kwa Maria Magdalena (Mk. 16:9). Yesu alikuja hapa baada ya kuwalisha watu 4000 (Mt. 15:32–39), na Mafarisayo na Masadukayo walimwuliza kwamba Awaonyesheishara kutoka mbinguni (Mt. 16:1–4).
-
Kana Yesu aligeuza maji kuwa divai (Yn. 2:1–11) na alimponya mwana wa mtu maarufu ambaye alikuwa Kapernaumu (Yn. 4:46–54). Kana pia palikuwa nyumbani kwa Nathanieli (Yn. 21:2).
-
Nazarethi Kupashwa habari kwa Maria na Yusufu kulifanyika katika Nazarethi (Mt. 1:18–25; Lk. 1:26–38; 2:4–5). Baada ya kurudi kutoka Misri, Yesu alitumia utoto Wake na ujana Wakehapa (Mt. 2:19–23; Lk. 2:51–52), alitangaza ukweli wa kuwa Yu Mwana wa Mungu na alikataliwa na walio mwenyewe Wake (Lk. 4:14–32).
-
Yeriko Yesu alimpa kuona mtu aliyekuwa kipofu (Lk. 18:35–43). Pia alikula pamoja na Zakayo, “mkubwa mmoja miongoni mwa watoza ushuru” (Lk. 19:1–10).
-
Bethabara Yohana Mbatizaji alishuhudia ya kwamba yeye alikuwa “sauti ya mtu aliye nyikani” (Yn. 1:19–28). Yohana alimbatiza Yesu katika Mto Yordani na akashuhudia ya kuwa Yesu ndiye Mwanakondoo wa Mungu (Yn. 1:28–34).
-
Nyika za Uyahudi Yohana Mbatizaji alihubiri katika nyika hizi (Mt. 3:1–4) mahali Yesu alipofunga kwa siku 40 na kujaribiwa (Mt. 4:1–11).
-
Emau Kristo mfufuka alitembea kwenye barabara ya kwenda Emau pamoja na wanafunzi Wakewawili (Lk. 24:13–32).
-
Bethfage Wanafunzi wawili walimletea Yesu punda ambaye alimpandana kuanza kuingia Kwake kwa shangwe katika Yerusalemu (Mt. 21:1–11).
-
Bethania Hapa palikuwa nyumbani kwao Mariamu, Martha, na Lazaro (Yn. 11:1). Mariamu alisikia maneno ya Yesu, na Yesu alimwambia Martha juu ya kuchagua “fungu lililo jema” (Lk. 10:38–42); Yesu alimfufua Lazaro kutoka kwa wafu (Yn. 11:1–44); Mariamu alipaka mafuta miguu ya Yesu (Mt. 26:6–13; Yn. 12:1–8).
-
Bethlehemu Yesu alizaliwa na alilazwa horini (Lk. 2:1–7); malaika walitangaza kwa wachungaji juu ya kuzaliwa kwa Yesu (Lk. 2:8–20); mamajusi waliongozwa na nyota kwenda kwa Yesu (Mt. 2:1–12), na Herode aliwaua watoto (Mt. 2:16–18).