12. Yerusalemu Wakati wa Yesu
-
Golgotha Mahali panapowezekana kuwa Yesu alisulubiwa (Mt. 27:33–37).
-
Kaburi la Kwenye Bustani Hapa yawezekana kuwa ndipo mahali ambapo lile kaburi ambamo mwili wa Kristo uliwekwa (Yn. 19:38–42). Kristo mfufuka alimtokea Maria Magdalena katika bustani nje ya kaburi Lake (Yn. 20:1–17).
-
Ngome ya Antonia Yesu yawezekana alishtakiwa, kuhukumiwa, kudhihakiwa na kupigwa mijeledi katika mahali hapa (Yn. 18:28–19:16). Paulo alikamatwa na kusimulia upya hadithi ya uongofu wake (Mdo. 21:31–22:21).
-
Bwawa la Bethzatha Yesu alimponya mtu aliyekuwa hajiwezi siku ya sabato (Yn. 5:2–9).
-
Hekalu Gabrieli alimwahidi Zakaria ya kuwa Elisabeti angelimzaa mwana (Lk. 1:5–25). Pazia la hekalu lilipasuka wakati wa kufa kwa Mwokozi (Mt. 27:51).
-
Baraza ya Sulemani Yesu alitangaza ya kuwa Yeye alikuwa ni Mwana wa Mungu. Wayahudi walijaribu Kumpiga kwa mawe (Yn. 10:22–39). Petro alihubiri toba baada ya kumponya mtu aliyekuwa kiwete (Mdo. 3:11–26).
-
Lango Zuri Petro na Yohana walimponya mtu aliyekuwa kiwete (Mdo. 3:1–10).
-
Mnara wa Hekalu Yesu alijaribiwa na Shetani (Mt. 4:5–7). (Yawezekana sana kuwa hapa ndipo eneo kla tukio hili.)
-
Mlima Mtakatifu (maeneo ambayo hayajatajwa)
-
Mapokeo yanashikilia kwamba hapa ndipo Ibrahimu alipojenga madhabahu kwa ajili ya kumtoa dhabihu Isaka (Mwa. 22:9–14).
-
Sulemani alijenga hekalu (1 Fal. 6:1–10; 2 Nya. 3:1).
-
Wababilonia waliliangamiza hekalu takribani katika mwaka 587 K.K. (2 Fal. 25:8–9).
-
Zerubabeli alilijenga upya hekalu takribani katika mwaka 515 K.K. (Ezra 3:8–10; 5:2; 6:14–16).
-
Herode alipanua gulio la hekalu na alilijenga upya hekalu kuanzia katika mwaka 17 K.K. Yesu aliletwa hapa kama mtoto mchanga (Lk. 2:22–39).
-
Katika umri wa miaka 12, Yesu alifundisha katika hekalu (Lk. 2:41–50).
-
Yesu alilisafisha hekalu (Mt. 21:12–16; Yn. 2:13–17).
-
Yesu alifundisha katika hekalu katika mara kadha wa kadha (Mt. 21:23–23:39; Yn. 7:14–8:59).
-
Warumi chini ya Tito waliliangamiza hekalu katika mwaka 70 B.K.
-
-
Bustani ya Gethsemani Yesu aliteseka, alisalitiwa, na alikamatwa (Mt. 26:36–46; Lk. 22:39–54).
-
Mlima wa Mizeituni
-
Yesu alitabiri angamizo la Yerusalemu na hekalu. Pia alizungumzia juu ya Ujio wa Pili (Mt. 24:3–25:46; ona pia JS—M).
-
Kutoka hapa Yesu alipaa mbinguni (Mdo. 1:9–12).
-
Katika 24 Oktoba 1841, Mzee Orson Hyde aliiweka wakfu Nchi Takatifu kwa ajili ya kurudi kwa watoto wa Ibrahimu.
-
-
Chemchemi ya Gihoni Sulemani alipakwa mafuta kuwa mfalme (1 Fal. 1:38–39). Hezekia alichimbisha njia ya chini ya ardhi ili kuleta maji kutoka chemchemi hii hadi mjini (2 Nya. 32:30).
-
Lango la Maji Ezra alisoma na kufasiri torati ya Musa kwa watu (Neh. 8:1–8).
-
Bonde la Hinomu mungu wa uongo Moleki aliabudiwa, ambako kulijumuisha kafara ya toto (2 Fal. 23:10; 2 Nya. 28:3).
-
Nyumba ya Kayafa Yesu alipelekwa mbele ya Kayafa (Mt. 26:57–68). Petro alikana kuwa yeye hamjui Yesu (Mt. 26:69–75).
-
Chumba cha Orofani Eneo la kimapokeo ambako Yesu alikula chakula cha Pasaka na akaianzisha sakramenti (Mt. 26:20–30). Aliosha miguu ya Mitume (Yn. 13:4–17) na akawafundisha (Yn. 13:18–17:26).
-
Kasri ya Herode Yesu alipelekwa mbele ya Herode, yawezekana katika eneo hili (Lk. 23:7–11).
-
Yerusalemu (maeneo ambayo hayajatajwa)
-
Melkizedeki alitawala kama mfalme wa Salemu (Mwa. 14:18).
-
Mfalme Daudi aliuteka mji huu kutoka kwa Wayebusi (2 Sam. 5:7; 1 Nya. 11:4–7).
-
Mji huu uliangamizwa na Wababilonia katika takribani mwaka wa 587 K.K. (2 Fal. 25:1–11).
-
Wengi walijazwa na Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste (Mdo. 2:1–4).
-
Petro na Yohana walikamatwa hapa na kuletwa mbele ya baraza (Mdo. 4:1–23).
-
Anania na Safira walimdanganya Bwana na wakafa (Mdo. 5:1–10).
-
Petro na Yohana walikamatwa, lakini malaika aliwaokoa kutoka gerezani (Mdo. 5:17–20).
-
Mitume waliwachagua wanaume saba ili wawasaidie (Mdo. 6:1–6).
-
Ushuhuda wa Stefano kwa Wayahudi ulikataliwa, naye alipigwa mawe hadi kufa (Mdo. 6:8–7:60).
-
Yakobo aliuawa kifo cha kishahidi (Mdo. 12:1–2).
-
Malaika alimfungulia Petro kutoka gerezani (Mdo. 12:5–11).
-
Mitume waliamua juu ya suala la tohara (Mdo. 15:5–29).
-
Warumi chini ya Tito waliuangamiza mji huu katika mwaka 70 B.K.
-