Misaada ya Kujifunza
9. Ulimwengu wa Agano la Kale


9. Ulimwengu wa Agano la Kale

ramani ya Biblia 9

Kask.

Kaukao

Bahari ya Kaspia

Mlima Ararati?

Bahari Nyeusi

Urartu

Wahori

Troi

Wahiti

Uru?

Harani (Padani-Aramu)

Ashuru

Karkemishi

Mesopotamia

Ninawi

Mto Frati

Ashuru

Akadi

Uwanda wa Dura

Shushani (Susa)

Mto Tigri

Babiloni

Rodo

Kitimu (Kipro)

Babeli (Shinari)

Shamu

Kaftori (Krete)

Elamu

Sidoni

Foenike

Dameski

Babilonia

Tiro

Jangwa la Uarabuni

Uru?

Bahari ya Kinerethi (Galilaya)

Megido

Bahari Kuu au ya Juu (Bahari ya Mediterania)

Yerusalemu (Salemu)

Bahari ya Chini (Ghuba ya Uajemi)

Kanaani

Bahari ya Chumvi (Bahari ya Mauti)

Beer-sheba

Delta ya Nile

Gosheni

Midiani

Jangwa la Libya

Oni

Esioni-gberi

Misri

Nile

Mlima Sinai? (Horebu)

Bahari ya Shamu

Kilomita

0 100 200 300 400

A B C D E F G H

1 2 3 4

1

2

2

3

4

5

6

7

8

9

10

11

12

13

14

15

16

17

  1. Mlima Ararati Eneo la kimapokeo ambapo safina ya Nuhu ilishukia (Mwa. 8:4). Mahali sahihi hapajulikani.

  2. Uru Makazi ya Kwanza ya Ibrahimu, karibu na kinywa cha Ufrati, mahali ambapo alikaribia kuwa kafara ya kibinadamu, alimwona malaika wa Yehova, na alipokea Urimu na Thumimu (Mwa. 11:28–12:1; Ibr. 1; 3:1). (Kumbuka pia yawezekana kuwa na sehemu nyingine ya Uru katika Mesopotamia Kaskazini.)

  3. Babiloni, Babeli (Shinari) Kwanza ilikaliwa na Kushi, mwana wa Hamu, na Nimrodi. Eneo la asili la Wayaredi katika wakati wa Mnara wa Babeli katika nyanda za Shinari. Baadaye ulikuwa mji mkuu wa jimbo la Babilonia na makao ya wafalme wa Kibabilonia, ikiwa ni pamoja na Nebukadneza ambaye aliwachukua Wayahudi wengi mateka kwenye mji huu baada ya kuangamizwa kwa Yerusalemu (587 K.K.). Wayahudi walibakia katika utumwa katika Babiloni kwa miaka 70 hadi wakati wa Mfalme Koreshi, ambaye aliwaruhusu Wayahudi kurudi Yerusalemu ili kulijenga upya hekalu. Danieli nabii pia aliishi hapa chini ya Nebukadneza, Belshazari, na Dario Ⅰ (Mwa. 10:10; 11:1–9; 2 Fal. 24–25; Yer. 27:1–29:10; Eze. 1:1; Dan. 1–12; Omni 1:22; Eth. 1:33–43).

  4. Shushani (Susa) Mji mkuu wa Ufalme wa Waajemi chini ya utawala wa Dario Ⅰ (Dario Mkuu), Zerse (Ahusuero) na Artazerze. Makao ya Malkia Esta, ambaye ujasiri na imani yake viliwaokoa Wayahudi. Danieli na baadaye Nehemia walitumikia hapa (Neh. 1:1; 2:1; Esta 1:1; Dan. 8:2).

  5. Uwanda wa Dura Shadraka, Meshaki, na Abednego walitupwa ndani ya tanuru la moto mkali wakati walipokataa kuabudu sanamu ya dhahabu iliyoumbwa na Nebukadneza; Mwana wa Mungu akawaokoa, nao wakatoka katika tanuru bila kudhurika (Dan. 3).

  6. Ashuru Ashuru ulikuwa mji mkuu wa kwanza wa nchi ya Ashuru, ukifuatwa na Ninawi. Watawala wa Waashuru ni Shalmanasa Ⅴ na Sargon Ⅱ waliushinda Ufalme wa Kaskazini wa Israeli na wakayachukua utumwani yale makabila kumi katika mwaka 721 K.K. (2 Fal. 14–15; 17–19). Ashuru ilikuwa ni tishio kwa Yuda hadi mwaka 612 K.K.; wakati Ashuru iliposhindwa na Babiloni.

  7. Ninawi Mji mkuu wa Ashuru. Ashuru iliivamia nchi ya Yuda wakati wa utawala wa Hezekia na huduma ya nabii Isaya. Yerusalemu mji mkuu wa Yuda, uliokolewa kimiujiza wakati malaika alipowapiga askari 185,000 wa Ashuru (2 Fal. 19:32–37). Bwana alimwambia nabii Yona kuuitia mji huu toba (Yon. 1:2; 3:1–4).

  8. Harani Ibrahimu alikaa hapa kwa muda kabla ya kwenda Kanaani. Baba wa Ibrahimu na kaka yake walibaki hapa. Rebeka (mkewe Isaka), na Raheli, Lea, Bilha, na Zilpa (wakeze Yakobo), walitoka katika eneo hili (Mwa. 11:31–32; 24:10; 29:4–6; Ibr. 2:4–5).

  9. Karkemishi Farao Neko alishindwa na Nebukadneza, ambako kulimaliza utawala wa Kimisri katika Kanaani (2 Nya. 35:20–36:6).

  10. Sidoni Mji huu ulianzishwa na Sidoni, mjukuu wa Hamu, na ndiyo mji wa Kaskazini kabisa wa Wakanaani (Mwa. 10:15–20). Ulikuwa ni makao ya Yezebeli, ambaye alianzisha ibada ya kuabudu Baali katika Israeli (1 Fal. 16:30–33).

  11. Tiro Huu ulikuwa mji muhimu wa kibiashara na bandari katika Shamu. Hiramu wa Tiro alipeleka mbao aina ya mkangazi na dhahabu na wafanyakazi ili kumsaidia Sulemani katika ujenzi wa helaku lake (1 Fal. 5:1–10, 18; 9:11).

  12. Dameski Ibrahimu alimwokoa Lutu hapa. Ulikuwa mji mkuu wa Shamu. Katika wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, Waisraeli waliuteka mji huu. Eliya alimpaka mafuta Hazaeli kuwa mfalme juu ya Dameski (Mwa. 14:14–15; 2 Sam. 8:5–6; 1 Fal. 19:15).

  13. Kanaani Ibrahimu, Isaka, Yakobo na wazao wao walipewa na Bwana nchi hii iwe milki yao isiyo na mwisho (Mwa. 17:8; 28).

  14. Mlima Sinai (Horebu) Bwana alisema na Musa kutoka katika kichaka kinachowaka moto (Ku. 3:1–2). Musa alipewa Torati na Amri Kumi (Ku. 19–20). Bwana alisema na Eliya katika sauti ndogo, tulivu (1 Fal. 19:8–12).

  15. Esioni-gberi Mfalme Sulemani alijenga “merikebu” katika Esioni-gberi (1 Fal. 9:26). Huenda katika bandari hii malkia wa Sheba, baada ya kusikia umaarufu wa Sulemani, alishuka ili kumwona (1 Fal. 10:1–13).

  16. Misri Ibrahimu alisafiri na kuja hapa kwa sababu ya njaa kuu katika Uru (Ibr. 2:1, 21). Bwana alimwambia Ibrahimu kuwafundisha Wamisri yale aliyomfunulia (Ibr. 3:15). Baada ya kaka zake Yusufu kumwuza yeye utumwani (Mwa. 37:28). Yusufu akawa mtawala wa nyumba ya Potifa hapa. Alitupwa gerezani. Akatafsiri ndoto za Farao na akapewa cheo chenye mamlaka katika Misri. Yusufu na kaka zake wakakutanishwa. Yakobo na familia yake walihamia hapa (Mwa. 39–46). Wana wa Israeli waliishi katika Gosheni wakati wa kuishi kwao katika Misri (Mwa. 47:6).

    Waisraeli waliongezeka “na walizidi kuwa wenye nguvu zaidi” hatimaye waliwekwa katika utumwa na Wamisri (Ku. 1:7–14). Baada ya mfuatano wa majanga Farao aliwaruhusu Waisraeli kuondoka Misri (Ku. 12:31–41). Yeremia alipelekwa Misri (Yer. 43:4–7).

  17. Kaftori (Krete) Nchi ya kale ya Waminoa.