2. Kutoka kwa Israeli Misri na Kuingia katika Kanaani
-
Ramesesi Israeli waliondolewa na Farao kutoka Misri (Ku. 12; Hes. 33:5).
-
Sukothi Baada ya Waebrania kuondoka kambi hii ya kwanza, Bwana akawa pamoja nao katika wingu wakati wa mchana na katika nguzo ya moto wakati wa usiku (Ku. 13:20–22).
-
Pi-hahirothi Waisraeli walipita katikati ya Bahari ya Shamu (Ku. 14; Hes. 33:8).
-
Mara Bwana aliyaponya maji ya Mara (Ku. 15:23–26).
-
Elimu Waisraeli walipiga kambi karibu na chemchemi 12 (Ku. 15:27).
-
Nyika za Sini Bwana alileta mana na kware ili kuwalisha Waisraeli (Ku. 16).
-
Refidimu Waisraeli walipigana na Amaleki (Ku. 17:8–16).
-
Mlima Sinai (Mlima Horebu au Yebeli Musa) Bwana alizifunua Amri Kumi (Ku. 19–20).
-
Nyika za Sinai Waisraeli walijenga hema takatifu (Ku. 25–30).
-
Kambi za Nyikani Wazee sabini wa Israeli waliitwa ili kumsaidia Musa kutawala watu (Hes. 11:16–17).
-
Esioni-gberi Israeli walipita katikati ya nchi za Esau na Amoni kwa amani (Kum. 2).
-
Kadeshi-barnea Musa aliwatuma wapelelezi katika nchi ya ahadi; Israeli waliasi na kushindwa kuingia katika nchi hiyo; Kadeshi ilitumika kama kambi kuu ya Waisraeli kwa miaka mingi (Hes. 13:1–3, 17–33; 14; 32:8; Kum. 2:14).
-
Nyika za Mashariki Israeli waliepuka ugomvi na Edomu na Moabu (Hes. 20:14–21; 22–24).
-
Mto Arnoni Waisraeli waliwaangamiza Waamori waliopigana nao (Kum. 2:24–37).
-
Mlima Nebo Musa aliiangalia nchi ya ahadi (Kum. 34:1–4). Musa alitoa mahubiri yake matatu ya mwisho (Kum. 1–32).
-
Nyanda za Moabu Bwana aliwaambia Israeli kugawana nchi na kuwanyangʼanya wakazi wake (Hes. 33:50–56).
-
Mto Yordani Waisrael walivuka Mto Yordani juu ya nchi kavu. Karibu na Gilgali, mawe kutoka chini ya Mto Yordani yaliwekwa na Waisraeli kama mnara wa kumbukumbu ya kugawanywa kwa maji ya Yordani (Yos. 3:1–5:1).
-
Yeriko Wana wa Israeli waliuteka na kuuangamiza mji huu (Yos. 6).