Misaada ya Kujifunza
Maelezo ya Jumla na Ufunguo


Maelezo ya Jumla na Ufunguo

Muhtasari juu ya ramani za hapo chini huonyesha eneo lengwa la kila moja ya ramani iliyopewa nambari ambayo inafuata. Ramani hizi zinakuwa na sehemu za maeneo mapana na vile vile maeneo lengwa kwa makini kijiografia.

  1. Ramani ya Sura ya Nchi Takatifu

  2. Kutoka kwa Israeli Misri na Kuingia katika Kanaani

  3. Mgawo wa Makabila Kumi na Mawili

  4. Milki ya Daudi na Sulemani

  5. Milki ya Waashuru

  6. Milki Mpya ya Wababeli na Ufalme wa Misri

  7. Milki ya Waajemi

  8. Milki ya Warumi

  9. Ulimwengu wa Agano la Kale

  10. Kanaani Nyakati za Agano la Kale

  11. Nchi Takatifu Nyakati za Agano Jipya

  12. Yerusalemu Wakati wa Yesu

  13. Safari za Kimisionari za Mtume Paulo

  14. Miinuko ya Nchi Takatifu

Ramani ya Maelezo ya Jumla

Kask.

1

6

10

5

11

9

14

8

13

3

4

2

7

12

Unaofuata ni ufunguo wa kuelewa aina mbalimbali na alama na aina ya chapa zinazotumika katika ramani. Kwa nyongeza, ramani moja yaweza kuwa na funguo zenye maelezo ya mifano ya nyongeza zinazoihusu ramani husika.

ufunguo

Nukta nyekundu huwakilisha jiji au mji.

Pembetatu ndogo nyeusi huwakilisha mlima.

Bahari ya Chumvi

Aina hii ya chapa inatumika kwa maeneo ya kijiografia kama vile bahari, mito, milima, majangwa na visiwa.

Yerusalemu

Aina hii ya chapa inatumika kwa majiji na miji (na kwa maeneo madogo yaliyoko katika ramani ya jiji la Yerusalemu).

Moabu

Aina hii ya chapa inatumika kwa maeneo madogo zaidi kisiasa kama vile mikoa, watu, na makabila.

Uyahudi

Aina hii ya chapa inatumika kwa maeneo makubwa zaidi kisiasa kama vile falme, na mataifa.