Misaada ya Kujifunza
13. Safari za Kimisionari za Mtume Paulo


13. Safari za Kimisionari za Mtume Paulo

ramani ya Biblia 13

Kask.

Ufunguo

Safari ya Kwanza

Safari ya Pili

Safari ya Tatu

Safari ya kwenda Roma

Italia

Bahari Nyeusi

Roma

Makedonia

Ponto

Vilabu Vitatu

Bithinia

Baraza ya Apio

Thesalonike

Filipi

Puteoli

Troa

Berea

Galatia

Samothrake

Misia

Asia

Pergamamu

Kapadokia

Antiokia

Lidia

Frigia

Smirna

Ikonio

Tarso

Kio

Efeso

Pisidia

Listra

Athene

Korintho

Laodikia

Regio

Akaya

Mileto

Pamfilia

Derbe

Likia

Perga

Antiokia

Patmo

Silisia

Sirakusa

Mira

Nido

Rodo

Kipro

Salami

Melita (Malta)

Krete

Pafo

Sidoni

Shamu

Tiro

Kimbilio Jema

Foenike

Dameski

Ptolemo

Bahari ya Mediterania

Kaisaria

Samaria

Yafa

Yerusalemu

Gaza

Kirene

Iskanderia

Misri

Libya

Kilomita

0 100 200 300 400

A B C D E F G H

1 2 3 4

1

2

3

4

5

6

7

8

9

10

11

12

13

14

15

16

17

18

19

20

21

22

23

24

25

26

27

  1. Gaza Filipo alihubiri kuhusu Kristo na alimbatiza towashi wa Kushi akiwa njiani kwenda Gaza (Mdo. 8:26–39).

  2. Yerusalemu Ona ramani ya 12 kwa ajili ya matukio katika Yerusalemu.

  3. Yafa Petro alipokea ono kwamba Mungu ametoa kipawa cha toba kwa Wayunani (Mdo. 10; 11:5–18). Petro alimfufua Thabitha kutoka kwa wafu (Mdo. 9:36–42).

  4. Samaria Filipo alihudumu katika Samaria (Mdo. 8:5–13), na Petro na Yohana baadaye walifundisha hapa (Mdo. 8:14–25). Baada ya kutunuku kipawa cha Roho Mtakatifu, Simoni mchawi alitaka kununua kipawa hiki kutoka kwao (Mdo. 8:9–24).

  5. Kaisaria Hapa, baada ya malaika kumhudumia akida aliyeitwa Kornelio, Petro alimruhusu kubatizwa (Mdo. 10). Hapa Paulo alifanya utetezi wake mbele ya Agripa (Mdo. 25–26; ona pia JS—H 1:24–25).

  6. Dameski Yesu alimtokea Sauli (Mdo. 9:1–7). Baada ya Anania kumrudishia Sauli kuona kwake, Sauli alibatizwa na alianza huduma yake (Mdo. 9:10–27).

  7. Antiokia (katika Shamu) Hapa wanafunzi kwa mara ya kwanza waliitwa Wakristo (Mdo. 11:26). Agabio alitoa unabii kuhusu njaa (Mdo. 11:27–28). Mfarakano mkubwa ulijitokeza kuhusu tohara (Mdo. 14:26–28; 15:1–9). Katika Antiokia Paulo alianza huduma yake ya pili pamoja na Sila, Barnaba, na Yuda Barsabasi (Mdo. 15:22, 30, 35).

  8. Tarso Mji wa nyumbani wa Paulo; Paulo aliletwa hapa na viongozi wa Kanisa ili kulinda uhai wake (Mdo. 9:29–30).

  9. Kipro Baada ya kuteswa, baadhi ya Watakatifu walikimbilia katika kisiwa hiki (Mdo. 11:19). Paulo alisafiri kupitia Kipro katika safari yake kwanza (Mdo. 13:4–5) kama alivyofanya Barnaba na Marko baadaye (Mdo. 15:39).

  10. Pafo Paulo alimlaani mchawi hapa (Mdo. 13:6–11).

  11. Derbe Paulo na Barnaba walihubiri injili katika mji huu (Mdo. 14:6–7, 20–21).

  12. Listra Wakati Paulo alipomponya mlemavu, yeye na Barnaba walishangiliwa kama miungu. Paulo alipigwa kwa mawe na akadhaniwa kuwa amekufa lakini akahuishwa na aliendelea kuhubiri (Mdo. 14:6–21). Nyumbani kwa Timotheo (Mdo. 16:1–3).

  13. Ikonio Katika huduma yao ya kwanza, Paulo na Barnaba walihubiri hapa na walitishwa kupigwa mawe (Mdo. 13:51–14:7).

  14. Laodikia na Kolosai Laodikia ni moja ya matawi ya Kanisa ambayo Paulo aliyatembelea na kupokea barua kutoka huko (Kol. 4:16). Pia ni moja ya miji saba iliyorodheshwa katika kitabu cha Ufunuo (mingine ni Efeso, Smirna, Pergamo, Thyatira, Sardi, na Filadelfia; ona Ufu. 1:11). Kolosai ipo kilometa 18 mashariki mwa Laodikia. Paulo aliwaandikia Watakatifu walioishi hapa.

  15. Antiokia (katika Pisidia) Katika huduma yao ya kwanza, Paulo na Barnaba waliwafundisha Wayahudi kwamba Kristo alikuja kutoka katika ukoo wa Daudi. Paulo alitoa injili kwa Waisraeli, halafu kwa Wayunani. Paulo na Barnaba waliteswa na kufukuzwa (Mdo. 13:14–50).

  16. Mileto Wakati akiwa hapa katika safari yake ya tatu, Paulo aliwaonya wazee wa Kanisa kwamba “mbwa mwitu wakali” watalivamia kundi (Mdo. 20:29–31).

  17. Patmo Yohana alikuwa mfungwa katika kisiwa hiki wakati aliyapokea maono ambayo sasa yamo katika Kitabu cha Ufunuo (Ufu. 1:9).

  18. Efeso Apolo alihubiri hapa kwa uwezo mkubwa (Mdo. 18:24–28). Paulo katika safari yake ya tatu, alifundisha katika Efeso kwa miaka miwili, akiwaongoa watu wengi (Mdo. 19:10, 18). Hapa alitunukia kipawa cha Roho Mtakatifu kwa kuwawekea mikono (Mdo. 19:1–7) na alifanya miujiza mingi, ikiwa ni pamoja na kuwafukuza mapepo wabaya (Mdo. 19:8–21). Hapa watu waabuduo Diana walianzisha vurugu dhidi ya Paulo (Mdo. 19:22–41). Sehemu ya Kitabu cha Ufunuo kiliandikwa kwa Kanisa huko Efeso (Ufu. 1:11).

  19. Troa Wakati Paulo alipokuwa hapa katika safari ya pili ya kimisionari, aliona ono la mtu katika Makedonia akiomba msaada (Mdo. 16:9–12). Akiwa hapa katika safari yake ya tatu, Paulo alimfufua Utiko kutoka kwa wafu (Mdo. 20:6–12).

  20. Filipi Paulo, Sila, na Timotheo walimwongoa mwanamke aliyeitwa Lidia, wakimtoa pepo mbaya, na walipigwa (Mdo. 16:11–23). Walipata msaada wa kimungu uliowasaidia kutoroka gerezani (Mdo. 16:23–26).

  21. Athene Paulo, wakati akiwa katika safari yake ya pili kwenda Athene, alifundisha katika Kilima Marse (Areopago) kuhusu “mungu asiyejulikana” (Mdo. 17:22–34).

  22. Korintho Paulo alikwenda Korintho katika safari yake ya pili, ambako alikaa na Akwila na Prisila. Alifundisha hapa na alibatiza watu wengi (Mdo. 18:1–18). Kutoka Korintho, Paulo aliandika waraka wake kwa Warumi.

  23. Thesalonike Paulo alihubiri hapa wakati wa safari yake ya pili ya kimisionari. Kikundi chake cha Kimisionari kiliondoka kwenda Berea baada ya Wayahudi kutishia usalama wao (Mdo. 17:1–10).

  24. Berea Paulo, Sila na Timotheo walipata watu waungwana wa kuwafundisha wakati wa safari ya pili ya kimisionari ya Paulo. Wayahudi kutoka Thesalonike waliwafuata na waliwatesa huko (Mdo. 17:10–13).

  25. Makedonia Paulo alifundisha hapa katika safari yake ya pili na ya tatu (Mdo. 16:9–40; 19:21). Paulo aliusifia ukarimu wa Watakatifu wa Makedonia ambao walimpa yeye na Watakatifu walio maskini wa Yerusalemu (Rum. 15:26; 2 Kor. 8:1–5; 11:9).

  26. Melita Paulo alivunjikiwa na meli katika kisiwa hiki akiwa njiani kwenda Roma (Mdo. 26:32; 27:1, 41–44). Yeye hakudhurika kwa kungʼatwa na nyoka na aliwaponya wengi waliokuwa wagonjwa katika Melita (Mdo. 28:1–9).

  27. Roma Paulo alihubiri hapa kwa miaka miwili chini ya ulinzi akiwa amezuiliwa nyumbani (Mdo. 28:16–31). Pia aliandika nyaraka, au barua, kwa Waefeso, Wafilipi na Wakolosai na kwa Timotheo na Filemoni wakati akiwa gerezani katika Roma. Petro aliandika waraka wake wa kwanza kutoka “Babiloni,” ambayo huenda ilikuwa Roma, mara baada ya mateso ya Nero kwa Wakristo katika mwaka 64 B.K. Kwa ujumla inaaminika na watu mengi kwamba Petro na Paulo waliuawa kwa kifo cha kishahidi hapa.