Maandiko Matakatifu
Alma 29


Mlango wa 29

Alma anatamani kuhubiri toba na juhudi ya malaika—Bwana anatoa walimu kwa mataifa yote—Alma anafurahia kazi ya Bwana na kwa kufaulu kwa Amoni na ndugu zake. Karibia mwaka 76 K.K.

1 Ee vile natamani ningekuwa malaika, na ningekuwa na matarajio ya moyo wangu, kwamba ningeenda mbele na kuhutubia watu na parapanda ya Mungu, na sauti ya kutingisha ulimwengu, na kuhubiri toba kwa watu wote!

2 Ndiyo, ningemtangazia kila mtu, kwa sauti kama ya radi, na mpango wa ukombozi, kwamba watubu na waje kwa Mungu wetu, kwamba kusije kukawa huzuni zaidi juu ya dunia.

3 Lakini tazama, mimi ni mtu, na hukosa kwa matakwa yangu; kwani ninahitaji nitosheke na vitu ambavyo Bwana amenipatia.

4 Sitakiwi kubadilisha katika tamaa yangu amri imara na haki za Mungu, kwani najua kwamba hutoa kwa watu kulingana na kutaka kwao, kama itakuwa kwenye kifo ama kwenye uhai; ndiyo, ninajua kwamba hugawanyia watu, ndiyo, huamuru kwao sheria ambazo hazibadiliki, kulingana na kutaka kwao, ikiwa zitakuwa za wokovu au kwa uharibifu.

5 Ndiyo, na ninajua kwamba uzuri na uovu ulidhihirishwa mema na maovu yalidhihirisha mbele ya watu wote; yule asiyejua mema na maovu hana lawama; lakini yule ajuaye uzuri na uovu, kwake itatolewa kulingana na matakwa yake, kama anataka uzuri au uovu, uzima au kifo, shangwe au majuto ya moyo.

6 Sasa, nikiona kwamba najua hivi vitu, kwa nini nitamani kuliko vile ninavyoeza kazi ambayo nimeitiwa kufanya?

7 Kwa nini nitamani kwamba ningekuwa malaika, ili niwazungumzie watu wote wa ulimwengu?

8 Kwani tazama, Bwana huwakubali mataifa yote, kila taifa na lugha yake, kufundisha neno lake, ndiyo, kwa hekima, yote ambayo anaona sawa wawe nayo; kwa hivyo tunaona kwamba Bwana hushauri kwa hekima, kulingana na yale ambayo ni ya haki na kweli.

9 Najua ile ambayo Bwana ameniamuru mimi, na ninatukuza ndani yake. Sijitukuzi mimi mwenyewe, lakini natukuza ile ambayo Bwana ameniamuru; ndiyo, na hii ni furaha yangu, kwamba labda niwe chombo kwenye mikono ya Mungu kuleta nafsi moja katika toba; na hii ndiyo shangwe yangu.

10 Na tazama, ninapoona wengi wa ndugu zangu wametubu kweli, na kumkubali Bwana Mungu wao, ndipo nafsi yangu hujaa na shangwe; ndipo ninapokumbuka yale ambayo Bwana amenifanyia mimi, ndiyo, hata kwamba amesikia sala yangu; ndiyo, ndipo ninapokumbuka mkono wake wa huruma ambao alinyosha kwangu.

11 Ndiyo, na pia nakumbuka utumwa wa babu zangu; kwani kwa kweli najua kwamba Bwana aliwakomboa kutoka kwenye utumwa, na kufuatana na hayo alianzisha kanisa lake; ndiyo, Bwana Mungu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo, aliwaokoa kutoka kwenye utumwa.

12 Ndiyo, nimekumbuka kila siku utumwa wa babu zangu; na kwamba yule Mungu ambaye aliwakomboa kutoka kwa mikono ya Wamisri aliwakomboa kutoka kwa utumwa.

13 Ndiyo, na yule yule Mungu alianzisha kanisa lake miongoni mwao; ndiyo, na yule yule Mungu ameniita mimi kwa mwito mtakatifu, kuhubiri neno kwa watu wake, na amenifanikisha sana, matokeo ambayo shangwe yangu imejaa.

14 Lakini mimi sijawi shangwe tu kwa kufanikiwa kwangu pekee, lakini shangwe yangu imejaa zaidi kwa sababu ya kufanikiwa kwa ndugu zangu, ambao wamekuwa kwenye nchi ya Nefi.

15 Tazama, wamefanya kazi sana, na wameleta matunda mengi; na zawadi yao itakuwa kubwa aje!

16 Sasa, ninapofikiria mafanikio ya hawa ndugu zangu roho yangu inabebwa, hata kama imetenganishwa kutoka kwa mwili, vile ilikuwa, kwani shangwe yangu ni kubwa sana.

17 Na sasa Mungu angewakubalia hawa, ndugu zangu, kwamba waketi kwenye ufalme wa Mungu; ndiyo, na pia wale ambao ni matokeo ya kazi yao kwamba wasitoke nje tena, lakini kwamba wamtukuze milele. Na afadhali Mungu akubali kwamba itendeke kulingana na maneno yangu, hata vile nilivyosema. Amina.