Amri za Alma kwa mwana wake Shibloni.
Yenye mlango wa 38.
Mlango wa 38
Shibloni aliteswa kwa ajili ya haki—Wokovu uko ndani ya Kristo, ambaye ni uzima na mwangaza wa ulimwengu—Jifunze kuzuia tamaa zenu. Karibia mwaka 74 K.K.
1 Mwana wangu, sikiliza maneno yangu, kwani ninakwambia, vile nilimwambia Helamani, kwamba ikiwa utatii amri za Mungu utafanikiwa katika nchi; na kadiri hutatii amri za Mungu utaondolewa kwenye uwepo wake.
2 Na sasa, mwana wangu, ninaamini kwamba nitakuwa na shangwe kuu juu yako, kwa sababu ya uthabiti wako na imani yako kwa Mungu; kwani kwa njia hiyo umeanza katika ujana wako kumtegemea Bwana Mungu wako, hata hivyo natarajia kwamba utaendelea kutii amri zake; kwani heri yule atakayevumilia hadi mwisho.
3 Nakwambia wewe, mwana wangu, kwamba tayari nimekuwa na shangwe kwako, kwa sababu ya uaminifu wako na bidii yako na subira yako na uvumilivu wako miongoni mwa watu wa Wazoramu.
4 Kwani ninajua kwamba ulikuwa umefungwa; ndiyo, na pia najua kwamba ulipigwa kwa mawe kwa ajili ya kuhubiri neno; na ulivumilia hivi vitu vyote kwa sababu Bwana alikuwa nawe; na sasa unajua kwamba Bwana alikuokoa.
5 Na sasa mwana wangu, Shibloni, ningetaka wewe ukumbuke, kwamba kadiri utakavyoweka imani yako ndani ya Mungu hata hivyo zaidi utakombolewa kutoka kwenye majaribio yako, na taabu zako, na mateso yako, na utainuliwa juu siku yako ya mwisho.
6 Sasa, mwana wangu singetaka kwamba ufikirie kwamba ninajua vitu hivi kwa uwezo wangu, lakini ni Roho wa Bwana aliyo ndani yangu ndiyo anayefanya vijulikane kwangu; kwani kama nisingezaliwa kwa Mungu nisingejua vitu hivi.
7 Lakini tazama, Bwana kwa rehema yake kuu alimtuma malaika wake kutangaza kwangu kwamba nikome kazi ya kuangamiza miongoni mwa watu wake; ndiyo, na nimemwona malaika uso kwa uso, na akazungumza na mimi, na sauti yake ilikuwa kama radi, na ikatetemesha ardhi yote.
8 Na ikawa kwamba nilikuwa kwa siku tatu usiku na mchana ndani ya uchungu mkali na maumivu ya roho; na haikuwa mpaka nilipomlilia Bwana Yesu Kristo kwa huruma, ndipo nikapata kusamehewa dhambi zangu. Lakini tazama, nilimlilia na nikapata amani ndani ya roho yangu.
9 Na sasa, mwana wangu, nimekwambia hii ili ujifunze hekima, kwamba ungejifunza kutoka kwangu kwamba hakuna njia nyingine au kwa vyote ambayo binadamu anaweza kuokolewa, ila tu kwa na kupitia kwa Kristo. Tazama, yeye ni uzima na mwangaza wa ulimwengu. Tazama, yeye ni neno la ukweli na haki.
10 Na sasa, vile umeanza kufundisha neno hata hivyo ningetaka kwamba uendelee kufundisha; na ningetaka kwamba uwe na bidii na kiasi kwa vitu vyote.
11 Hakikisha kwamba hujiinui kwa kiburi; ndiyo, angalia kwamba hujisifu kwa hekima yako mwenyewe, wala kwa nguvu zako nyingi.
12 Tumia ujasiri, lakini usiwe mjeuri; na pia uone kwamba ujifunze kuzuia tamaa zako zote, ili uweze kujazwa na mapenzi; hakikisha kwamba uepuke kutokana na uvivu—
13 Usiombe kama vile Wazoramu wanavyofanya, kwani umeona kwamba wanaomba kuonekana na watu, na kusifiwa kwa hekima yao.
14 Usiseme: Ee Mungu, ninakushukuru kwamba tu wema kuliko ndugu zetu; lakini afadhali useme: Ee Bwana, unisamehe kwa kutokuwa na haki kwangu, na ukumbuke ndugu zangu kwa huruma—ndiyo, kubali kutokuwa na haki kwako mbele ya Mungu wakati wote.
15 Na Bwana aibariki roho yako, na akupokee katika siku ya mwisho ndani ya ufalme wake, kukaa chini kwa amani. Sasa nenda, mwana wangu, na ukafundishe neno kwa watu hawa. Uwe na busara. Mwana wangu, kwaheri.