Misaada ya Kujifunza
TJS, Mathayo 6


TJS, Mathayo 6:14. Linganisha na Mathayo 6:13; mabadiliko ya aina hiyo hiyo yalifanywa katika Luka 11:4

Bwana hatuongozi sisi katika majaribu.

14 Na usiache tutiwe katika majaribu, lakini tuokoe na yule mwovu.

TJS, Mathayo 6:22. Linganisha na Mathayo 6:22

Ikiwa macho yetu yatakuwa katika utukufu wa Mungu pekee, miili yetu yote itajaa nuru.

22 Taa ya mwili ni jicho; kwa hiyo kama jicho lako litakuwa katika utukufu wa Mungu pekee, mwili wako wote utajaa nuru.

TJS, Mathayo 6:25–27. Linganisha na Mathayo 6:25; 10:10

Yesu anawaonya wanafunzi wake juu ya ugumu wa kazi yao lakini anaahidi kwamba atawatayarishia njia na kwamba Baba wa Mbinguni atawapa mahitaji yao.

25 Na, tena, nawaambieni, Enendeni ulimwenguni, na msiujali ulimwengu; kwani ulimwengu utawachukia, na utawatesa, na utawafukuzeni kutoka masinagogi yao.

26 Hata hivyo, mtakwenda nyumba kwa nyumba, mkiwafundisha watu; na nitakwenda mbele yenu.

27 Na Baba yenu wa mbinguni atawapeni, vitu vyote mnavyohitaji kwa chakula, kile mtakachokula; na kwa mavazi, yale mtakayo vaa.

TJS, Mathayo 6:38. Linganisha na Mathayo 6:33

Yatupasa kutafuta kwanza kuujenga ufalme wa Mungu.

38 Kwa hiyo, usitafute mambo ya ulimwengu huu bali kwanza tafuteni kujenga ufalme wa Mungu, na kustawisha haki zake, na mambo haya yote mtazidishiwa.