“Salamu kutoka Thailand!” Rafiki, Jan. 2024, 8–9.
Salamu kutoka Thailand!
Jifunze kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni ulimwenguni kote.
Thailand ni nchi iliyopo Kusini Mashariki mwa Asia. Takribani watu milioni 72 wanaishi huko.
Lugha
Kithai ndiyo lugha rasmi ya nchi. Alfabeti za Kithai zina herufi 72.
Sherehe za Songkran
Watu wa Thailand husherehekea mwaka mpya wao kwa mchezo mkubwa ulimwenguni wa kupigana kwa maji. Wanarushiana maji ili kukumbuka kuosha mambo mabaya. Sherehe hudumu kwa siku tatu!
Pango la Chuimilia
Hekalu la Pango la Chuimilia ni hekalu la Kibudha ambapo watu wengi huabudu na kusali. Ili kulifikia, lazima upande ngazi 1,260 kuelekea juu mlimani. Kuna alama za nyayo za chuimilia ndani ya pango!
Masoko Yanayoelea
Nchini Thailand, watu huweza kufanya manunuzi kwenye mashua za mtoni, kama vile maduka madogo yanayoelea. Mito ni njia mojawapo ya kusafiri kuzunguka mji mkuu. Majengo mengi yapo juu ya nguzo ili yawe juu ya maji.