“Msikilize Roho Mtakatifu,” Rafiki, Jan. 2024, 17.
Kitu cha kuburudisha
Msikilize Roho Mtakatifu
Fanya shughuli hii na familia yako ili mjifunze kuhusu Roho Mtakatifu.
-
Mchague mtu awe “mtafutaji.” Mtu huyo anatoka nje ya chumba wakati wengine wakificha kitu kama jiwe au mwanasesere.
-
Mrudishe ndani mtafutaji.
-
Mtu mmoja ananong’ona ili kumsaidia mtafutaji ajue mahala kilipo kitu kilichofichwa. Wengine wanazungumza kwa sauti ya kawaida au sauti kubwa ili kuwavuruga mawazo.
-
Wakati mtu anapokipata kile kitu, chagua mtu mwingine awe mtafutaji.
Zungumza jinsi Roho Mtakatifu anavyozungumza na wewe kwa fikra katika mawazo yako na hisia katika moyo wako. Anaweza kukuongoza na kukusaidia ufanye chaguzi nzuri. Unapofuata mawazo na hisia hizo kutoka Kwake, unaweza kuhisi shangwe na amani.
Muda wa Kiburudisho
Tengeneza “biskuti” za matunda yaliyokatwa katwa kwa ajili ya kula na familia yako! Kata tufaha au pea katika vipande vidogo vidogo. Kisha ongeza vitu vya kuongeza ladha juu yake kama vile karanga za kusagwa, asali, korosho, chipsi au vipande vya nazi.