Rafiki
Shughuli za Njoo, Unifuate
Januari 2024


“Shughuli za Njoo, Unifuate,” Rafiki, Jan. 2024, 28–29.

Shughuli za Njoo, Unifuate

Kwa ajili ya jioni ya nyumbani au kujifunza maandiko—au kwa ajili ya burudani tu!

Januari 1–7

Ushuhuda Wako

Alt text

Vielelezo na Katy Dockrill

Kwa ajili ya Kurasa za Utangulizi za Kitabu cha Mormoni

Kitabu cha Mormoni mwanzoni kiliandikwa kwenye mabamba ya dhahabu. Watu walioyaona mabamba waliandika kwamba walijua kilikuwa cha kweli (ona Ushuhuda wa Mashahidi Watatu na Ushuhuda wa Mashahidi Wanane). Andika au chora ushuhuda wako mwenyewe wa Kitabu cha Mormoni na uweke ndani ya maandiko yako.

Januari 8–14

Kushiriki Hazina

alt text

Kwa ajili ya 1 Nefi 1–5

Maandiko ni hazina kuu (ona 1 Nefi 5:21). Chora baadhi ya maumbo ya johari kwenye karatasi na yakate. Mwombe kila mtoto aandike andiko la Kitabu cha Mormoni juu ya johari. Changanya johari na fanyeni zamu kuchagua moja na kusoma kila andiko.

Januari 15–21

Mabamba Rahisi Kueleweka na yenye Thamani

alt text

Kwa ajili ya 1 Nefi 6–10

Bwana alimwambia Nefi atengeneze seti nyingine ya mabamba kwa kusudi maalumu na lenye hekima (ona 1 Nefi 9). Tengeneza seti yako mwenyewe ya mabamba kwa kutumia karatasi iliyokunjwa au vipande vya ubao mgumu. (Unaweza hata kufunika karatasi yako au ubao mgumu kwa kutumia foili ya aluminiamu!) Andika au chora kile unachojifunza kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni kwenye mabamba yako.

Januari 22–28

Upendo wa Mungu

alt text

Kwa ajili ya 1 Nefi 11–15

Soma hadithi ya maandiko kuhusu ndoto ya Lehi kwenye ukurasa wa 26. Sasa chora mti. Mruhusu kila mwanafamilia aongeze jani kwenye mti na aseme kitu kimoja ambacho Baba wa Mbinguni ametupatia ambacho kinaonesha kwamba anatupenda.