Njia Yangu ya Agano
Kushinda Kukatishwa Tamaa na Vikwazo
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaweza kufanya nuru iangaze katika nyakati za giza kwenye maisha yetu.
Kila siku ina nyakati nyingi za shangwe zinazoweza kutambuliwa, kufurahiwa na kushukuriwa. Lakini wakati mwingine mawingu—majaribu, kukatishwa tamaa, hisia za uchungu, mtazamo ulioharibiwa—huingilia njia yetu na kuzuia vipaumbele vyetu vya milele. Maisha haya yamenuiwa kuwa ya uzoefu mkamilifu ambao utatusaidia kukua na kujiandaa kwa shangwe za umilele.
Kwa kurejelea kwenye kitabu chetu cha mwongozo wa kujifunza, Njoo, Unifuate, tunajifunza kutoka kwenye hadithi ya uumbaji kwamba Mungu anaweza kufanya kitu kikubwa kutokana na kitu kisicho na umbile. Huenda mara chache huwa tunakuwa “tusio na mpangilio” katika juhudi zetu za kuishi kanuni za injili.
“Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ni Waumbaji, na kazi Zao za ubunifu kwetu sisi hazijaisha. Wao wanaweza kufanya nuru ikaangaza katika nyakati za kiza katika maisha yetu. Wanaweza kutengeneza nchi kavu katikati ya bahari zenye dhoruba za maisha yetu . . . Wanaweza kutubadilisha sisi kuwa viumbe wazuri kama tulivyokusudiwa kuwa.”1
Wakati changamoto zetu zinapoonekana kuwa nzito na kukata tamaa kunapoingia, haya ni baadhi ya mambo halisi tunayoweza kufanya ili kupata tena kipawa cha upendo, amani, msamaha na ujasiri ambavyo mwokozi kwa rehema zake alitupatia:
-
Endelea kuomba—hasa tukijadili hofu zetu na kisha baki imara na sikiliza. Rais Nelson amesema, “Ninawaalika kuigeuza mioyo yenu, akili na nafsi kwa kiasi kikubwa kwa Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo.”2
-
Endelea kusoma maandiko—kwa kuyafananisha na sisi wenyewe tunaweza kupokea msukumo na umaizi.
-
Kwa msaada wa Bwana, tutathmini hofu zetu. Tunaweza kujiuliza maswali haya: Je, tunahitaji nini ili kutenda kwa utofauti? Je, sisi tunaweza kufanya nini; je, Bwana anaweza kufanya nini ili kutusaidia?
Je, tuko radhi kubadilisha njia zetu na kutunza mtazamo wetu wa milele? Je, tuko radhi kufunganisha mapenzi yetu kwa Bwana? Je, tuko radhi kugeukia kikundi chetu cha msaada—Mungu, familia, marafiki—kwa ajili ya mawazo mapya na uelewa mkubwa na ushauri? Je, tuko radhi kuitikia na kufuata misukumo ya Bwana?
-
Kujitahidi kuthamini wakati wa Bwana—kuwa na subira na changamoto zetu pamoja na sisi mwenyewe.
-
Kutenga muda wa kuonyesha shukrani zetu kwa Mwokozi wetu na kwa Baba wa Mbinguni kwa msaada na baraka Zao. Tunaweza kutambua na kusherehekea kila tone la maendeleo tunayofanya kwa msaada Wao.
Mzee Dieter F. Uchtdorf amesema, “Bila kujali hali yetu ya sasa, lipo tumaini kwa ajili yetu. Bila kujali mahangaiko yetu, bila kujali huzuni zetu, bila kujali makosa yetu, Baba yetu wa Mbinguni mwenye huruma isiyo na mwisho anatamani kwamba tusonge karibu Naye ili kwamba Naye aweze kusonga karibu nasi. [Yeye] hujaza mioyo yetu kwa shangwe isiyo na kipimo, huangaza masaa yetu ya giza totoro kwa amani, huweka katika akili zetu kweli za thamani, hutuchunga kupita nyakati za wasiwasi, hushangilia tunaposhangilia na kujibu maombi yetu ya haki”.3
Kwenye tamati ya Mkutano Mkuu mnamo Oktoba 2020, Rais Nelson alitupatia baraka hii: “Ninawabariki mjazwe na amani ya Bwana Yesu Kristo. Amani yake inapita uelewa wote wa mwanadamu. Ninawabariki kwa ongezeko la hamu na uwezo wa kutii sheria za Mungu. Ninaahidi kwamba mtakapofanya hivyo, mtafunikwa kwa baraka, ikiwemo ujasiri wa hali ya juu, ongezeko la ufunuo binafsi, utulivu katika nyumba zenu na shangwe hata katikati ya wasiwasi.”4