2022
Nyumba za ibada
Juni 2022


Dondoo za Kitabu cha Maelezo

Nyumba za ibada

Nyumba za ibada zinatofautiana kwa ukubwa na aina kutegemeana na mahitaji na hali za eneo husika. Nyumba ya ibada yaweza kuwa eneo lililojengwa au kununuliwa na Kanisa, nyumba ya muumini, shule au eneo la katikati la jumuia ya eneo husika, eneo la kupanga au chaguo lingine lililoidhinishwa.

Usafishaji na Utunzaji wa Nyumba za Ibada

Viongozi na waumini wa mahali husika, ikiwa ni pamoja na vijana, wana jukumu la kusaidia kuweka safi kila jengo na katika hali nzuri. Hii husaidia:

  • Kuhifadhi asili ya utakatifu ya jengo kama mahali ambapo Roho anaweza kuwepo.

  • Kuhimiza unyenyekevu.

  • Kuwasilisha taswira ya utu na heshima.

  • Kuendeleza maisha ya matumizi ya jengo.

Ratiba ya usafi haipaswi kuwa mzigo kwa waumini. Kwa mfano, ikiwa kusafiri kufikia jengo ni changamoto, waumini wanaweza kusafisha kama sehemu ya matukio ya kila wiki wakati wanapokuwa kwenye jengo.