“Mei 13–19: ‘Nuru … Ambayo Haiwezi Kutiwa Giza.’ Mosia 11–17,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2024)
“Mei 13–19. Mosia 11–17,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2024)
Mei 13–19: “Nuru … Ambayo Haiwezi Kutiwa Giza”
Mosia 11–17
Moto mkubwa unaweza kuanzishwa na cheche moja. Abinadi alikuwa mtu mmoja tu ambaye alikuwa akishuhudia dhidi ya mfalme mwenye nguvu na mahakama yake. Maneno yake yalikataliwa kwa sehemu kubwa, na alihukumiwa kifo. Lakini ushuhuda wake juu ya Yesu Kristo, ambaye ni “nuru … ambayo haiwezi kutiwa giza” (Mosia 16:9), ulichochea kitu fulani ndani ya kuhani kijana Alma. Na cheche hiyo ya uongofu ilikua pole pole wakati Alma alipokuwa akiwaleta wengine wengi katika toba na imani katika Yesu Kristo. Miale ya moto ambayo ilimuua Abinadi hatimaye ilizima, lakini moto wa imani ambao maneno yake yaliusababisha ungekuwa na ushawishi wa kudumu juu ya Wanefi—na juu ya wale wanaosoma maneno yake leo. Wengi wetu kamwe hatutakabiliana na kile hasa alichokabiliana nacho Abinadi kwa sababu ya shuhuda zetu, lakini sote tunazo nyakati ambapo kumfuata Yesu Kristo ni mtihani wa ujasiri na imani yetu. Pengine kujifunza ushuhuda wa Abinadi kutapuliza miale ya moto wa ushuhuda na ujasiri moyoni mwako pia.
Ona pia “Abinadi Testifies of Jesus Christ” (video), Gospel Library.
Mawazo kwa ajili ya kujifunza Nyumbani na Kanisani
Ninaweza kusimama kwa ajili ya Yesu Kristo, hata wakati ninaposimama peke yangu.
Wakati unajifunza Mosia 11–13; 17, angalia picha ya Abinadi kwenye muhtsari huu. Je, unajifunza kipi kuhusu kusimama kama shahidi wa Kristo? Hususani, ungeweza kufokasi kujifunza kwako kwenye vifungu vya maneno au maswali kama haya:
-
Ni kwa jinsi gani ungemwelezea Nuhu na watu wake? Kwa nini ilihitaji ujasiri kwa Abinadi kushiriki ujumbe wa Mungu pamoja nao? (ona Mosia 11:1–19, 27–29; 12:9–15).
-
Je, ungemwelezeaje Abinadi? Je, Abinadi alielewa kipi ambacho kilimsaidia awe jasiri kwenye ushuhuda wake? (ona Mosia 13:2–9, 28, 33–35; 17:8–10, 20).
Ni lini umehisi kama ulikuwa umesimama peke yako katika kumtetea Mwokozi na injili Yake? Je, ni kwa jinsi gani Yeye alikusaidia uhisi kwamba alikuwa pamoja na wewe? Wakati ukitafakari hili, ungeweza kusoma tukio la Elisha na mtumishi wake katika 2 Wafalme 6:14–17. Je, ni kitu gani kinakuvutia katika hadithi hii?
Ungeweza pia kuchunguza kurasa 31–33 za Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi ili kupata vifungu vya maneno ambavyo vinakupa ujasiri wa kuutetea ukweli. Au ungeweza kufanya vivyo hivyo katika mashairi ya nyimbo kama vile “Tenda Mema” au “Tusonge Mbele” (Kitabu cha Nyimbo za Dini, na. 133, 139)
Utawezaje kutumia kile unachojifunza kutoka kwa Abinadi? Video “Dare to Stand Alone” (Gospel Library) inaonesha hali ambapo unaweza kusimama kwa ajili ya Kristo na injili Yake. Je, ni mifano ipi mingine unaweza kuifikiria?
Ona pia Warumi 1:16; 2 Timotheo 1:7–8; “Chapter 8: The Call for Courage,” Teachings of Presidents of the Church: Thomas S. Monson (2022), 135–47; Mada za Injili, “Imani katika Yesu Kristo,” Gospel Library
Ninahitaji kutumia moyo wangu ili nielewe neno la Mungu.
Makuhani wa Mfalme Nuhu walikuwa wakiyafahamu maneno ya Mungu. Wangeweza kunukuu vifungu vya maneno vya maandiko na kudai walikuwa wakifundisha amri. Lakini bado, maisha yao yalionekana kutoguswa na injili ya Mwokozi. Kwa nini ilikuwa hivyo?
Fikiria kuhusu hili wakati ukisoma Mosia 12:19–37. Unafikiri inamaanisha nini kutumia moyo wako ili kuelewa neno la Mungu? Je, ni maneno au vifungu gani vya maneno vinakuvutia kufanya mabadiliko katika njia unayotumia kujifunza injili?
Amri za Mungu zinapaswa kuandikwa katika mioyo yetu.
Fikiria kuhusu maoni ya Abinadi kwamba sheria “zilikuwa hazijaandikwa katika mioyo” ya [wale] makuhani (Mosia 13:11). Je, kifungu hiki cha maneno huenda kikamaanisha nini? Wakati ukisoma Mosia 13:11–26, zingatia ikiwa amri hizi zimeandikwa katika moyo wako.
Ona pia Yeremia 31:31–34; 2 Wakorintho 3:3.
Yesu Kristo aliteseka kwa ajili yangu mimi.
Katika Mosia 14–15, tambua maneno na vifungu vya maneno vinavyomuelezea Mwokozi na mateso aliyoteseka kwa ajili yako. Ni mistari ipi inasaidia kuimarisha kwa kina upendo na shukrani zako Kwake?
Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo ni vyote Baba na pia Mwana?
Abinadi alifundisha kwamba Mungu Mwana—Yesu Kristo—angekuwa Mkombozi (ona Mosia 15:1), akikaa katika mwili, na kuwa vyote binadamu na pia Mungu (mistari 2–3). Yeye alijinyenyekeza kikamilifu kwenye mapenzi ya Mungu Baba (mistari 5–9). Kwa sababu ya hili, Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na mwakilishi mkamilifu wa duniani wa Mungu Baba (ona Yohana 14:6–10).
Yesu Kristo pia ni Baba kwa namna kwamba wakati tunapokubali ukombozi Wake, tunakuwa “uzao wake” na “warithi wa ufalme wa Mungu” (Mosia 15:11–12). Kwa maneno mengine tunakuwa tumezaliwa upya kiroho kupitia Yeye (ona Mosia 5:7).
Kwa nini unadhani ni muhimu kujua kweli hizi kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo? Je, ushuhuda wa Abinadi unaimarishaje imani yako katika Wao?
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Ninaweza kusimama kwa ajili ya Yesu Kristo, hata wakati ninaposimama peke yangu.
-
Wakati mwingine kwenye maisha yetu, sote tunakabiliana na shinikizo la kufanya maamuzi ambayo huenda kinyume na imani katika Yesu Kristo. Watoto wako wanaweza kujifunza kipi kutoka kwa Abinadi kuhusu kusimama kama mashahidi wa Yesu Kristo, hata kama kufanya hivyo hakuleti umaarufu? Sanaa iliyoko katika muhtasari huu au “Mlango wa 14: Abinadi na Mfalme Nuhu” (katika Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 38–42) ingeweza kuwasaidia wapate taswiira ya hadithi kutoka Mosia 11–13; 17. Waulize kitu gani wanakipenda kuhusu Abinadi.
-
Watoto wako wangefurahia kuigiza sehemu za hadithi ya Abinadi. Wangeweza kuigiza matukio halisi ya maisha ili kufanyia mazoezi kile ambacho wangefanya kama wengine wangewataka wafanye jambo baya. Au wangeweza kushiriki uzoefu ambapo walikuwa majasiri katika kumfuata Yesu Kristo. Je, ni kwa namna gani Abinadi alimfuata Yesu Kristo? (ona Mosia 13:2–9; 17:7–10). Je, ni kwa nini Mfalme Nuhu hakufanya kitu alichokijua kuwa kilikuwa sahihi? (ona Mosia 17:11–12).
Ninapaswa kutii Amri Kumi.
-
Makuhani wa Mfalme Nuhu walizijua amri lakini “hazikuwa zimeandikwa mioyoni [mwao]” (Mosia 13:11). Je, utawezaje kuwasaidia watoto wako wazijue amri na wazipende? Pengine wangeweza kuandika amri kutoka Mosia 12:33–36 na 13:11–24 kwenye karatasi lenye umbo la moyo. Wakati wakifanya hivyo, zungumza nao kuhusu amri hizi zinamaanisha nini na jinsi ya kuzifuata. Ni kwa namna gani tunaziandika amri hizi kwenye mioyo yetu?
-
Mngeweza pia kuimba pamoja wimbo kuhusu amri, kama vile “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47). Ni baraka zipi huja kutokana na kutii amri?
Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu Kristo ili aniongoze nirudi Kwake.
-
Ingawa ni mlango mfupi, Mosia 14 ina baadhi ya maneno na vifungu vya maneno ambavyo vinaeleza kuhusu Yesu Kristo. Pengine wewe na watoto wako mngeweza kuviorodhesha wakati mkisoma mlango huo pamoja. Kisha mngeweza kuzungumza kuhusu jinsi mnavyohisi kuhusu Mwokozi wakati mkijifunza maneno haya na vifungu hivi.
-
Akifundisha kuhusu Yesu Kristo, Abinadi alimnukuu nabii Isaya, ambaye alitufananisha na kondoo aliyepotea. Pengine watoto wako wangeshiriki uzoefu wao ambapo walipoteza kitu fulani au wao wenyewe walipotea. Je, walihisije? Je, walifanya nini? Kisha mngeweza kusoma pamoja Mosia 14:6 na 16:4–9. Je, ni kwa namna gani sisi ni kama kondoo wanaotangatanga kutoka kwa Mungu? Je, ni kwa jinsi gani Yesu Kristo hutusaidia sisi turudi?