“Kuitafuta Sayuni na Baraka za Bwana,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2021, 2–5.
Njoo, Unifuate
Kutafuta Sayuni na Baraka za Bwana
Kuijenga Sayuni ni wajibu mkubwa, lakini pia inaleta tunu kubwa.
ukweli mkuu wa kwanza wa mbinguni ni kwamba Mungu anatupenda kwa moyo Wake wote, uwezo, akili, na nguvu. Yeye anataka kilicho bora kwa kila mmoja wenu—Yeye siku zote anataka na siku zote atataka. Anataka sisi tuwe na furaha; sio kwa muda au kwa juujuu tu, bali kwa kina na kwa milele kama alivyo. Anatutaka sisi tukue na kufikia uwezo wetu wa milele kama mwana na binti wa Mungu.
Ninajua hii mara zote si rahisi. Wengi kati yenu mna kabiliana na matatizo na majaribu binafsi ambayo yanaweza wakati mwingine kuwashinda. Pengine mmetazama hali zenu wenyewe, kwa baadhi ya hali katika familia zenu, au matatizo miongoni mwa mataifa ulimwenguni kote, na kushangazwa “Jinsi gani ninaweza kupita mawimbi haya ya changamoto?” Jibu moja linaweza kukushangaza: Tafuta kuijenga Sayuni.
Sayuni iko wapi?
Kupitia historia yote Mungu kwa kawaida amewaita watu Wake kuanzisha Sayuni. Hiyo ilikuwa kwa kawaida sehemu maalumu ambapo watu wa Mungu wangeweza kuwa huru kutokana na ushawishi wa ulimwengu na kuishi kwa amani na kila mmoja. Lakini katika hiki kipindi kikuu cha mwisho, Sayuni haikomi kwa sehemu moja ya kijiografia. Katika siku zetu, Sayuni inaweza kuwa popote muumini mwaminifu wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho alipo. Bwana alielezea watu hawa wa Sayuni kama waliokuwa “wa moyo mmoja na wazo moja” (Musa 7:18) na “moyo safi” (Mafundisho na Maagano 97:21). Kwa kifupi, hatufikirii tena juu ya Sayuni kama wapi tutakapokwenda kuishi bali jinsi tutakavyoishi.
Baraka nyingi za kupendeza zimehifadhiwa kwa ajili yako unapofanya kwa uwezo wako wote kuijenga Sayuni, kuwa mtu yule ambaye Mwokozi anahitaji uwe, na kusaidia kutayarisha njia kwa ajili ya kurudi Kwake duniani. Juhudi kama hiyo inahitaji kazi na imani kubwa mno, bali pia itaweza kuleta shangwe isiyo na mwisho na furaha. Ninatumaini mtaona hii kuwa ya kusisimua na kufurahisha kama nionavyo! Kama Rais Russell M. Nelson alivyofundisha, hakuna—kiuhalisia chochote—ambacho kingekuwa cha umuhimu kuliko hili.1 Na tunapata Kushiriki! Sisi ni askari katika mistari ya mbele ya ukweli. Hatuchukui risasi; tunachukua bandeji! Tunaitwa kusaidia kuponya ulimwengu na kuandaa mkusanyiko mkubwa wa watu ulimwenguni ambao Mwokozi anaweza kuja kwao.
Mpende Mungu na Jirani
Tunaweza kufanilkisha aina hii ya familia au ujirani au taifa kwa kushika amri ya upendo. Na zaidi tunapo mpenda Mungu, zaidi tutawapenda majirani zetu na kuona ni kwa njia zipi tunaweza kuwabariki. Kuna majirani wa kuwasaidia, maskini wa kuwainua, na mema ya kuyafanya kila mahali.
Bwana wakati fulani alielezea wajibu huu na baraka kwa njia hii:
“Kwa hiyo, kuwa mwaminifu; … “Saidia wadhaifu, inyooshe mikono iliyolegea, na yaimarishe magoti yaliyo dhaifu.”
“Na kama utakuwa mwaminifu hadi mwisho nawe utapata tuzo la mwili usiokufa, na uzima wa milele katika makao ambayo nimeyatayarisha katika nyumba ya Baba yangu” (Mafundisho na Maagano 81:5–6).
Simamia Ukweli
Wakati Mungu anapotuita kuijenga Sayuni, Anatuita kusimama wima kwa ajili ya mafundisho Yake na kubaki imara katika imani yetu. Hii haitakuwa siku zote rahisi au yenye faraja kuifanya, lakini lazima tuifanye—kwa huruma, unyenyekevu, uelewa, na upendo usioshindwa kwa ajili ya wengine. Katika kutafuta kwetu kuijenga Sayuni, kwa hakika tutakutana na wale ambao hawaonekani, au hawavai au kujiheshimu ipasavyo. Wakati tukutanapo na watu kama hawa, lazima tuwe waangalifu kuwajibu kwa haki, sio kwa kujidai. Katika hali kama hizi kitu kizuri tunachoweza kufanya ni kujiheshimu vizuri na kuonesha “upendo wa kweli” kwa ajili yao (ona Mafundisho na Maagano 121:41).
Nataka wengine wafaidi baraka ambazo ninazo, bali wakati mwingine nina staajabu jinsi ya kuzishirikisha katika njia ambayo haitakuwa ya kuchukiza au isiyo eleweka. Somo hili limenisaidia wakati wote wa miito yangu ya Kanisa na wajibu wangu binafsi kama mfuasi wa Kristo:
“Kwa hiyo ninawaambia, pazeni sauti zenu kwa watu hawa; yasemeni mawazo nitakayoyaweka mioyoni mwenu, na ninyi hamtashindwa mbele za watu;
“Kwani mtapewa katika saa ile ile, ndiyo, katika wakati ule ule, kile mtakachosema.
“Lakini amri ninaitoa kwenu, kwamba mtakitangaza kitu chochote mtakachotangaza kwa jina langu, kwa taadhima moyoni, kwa roho ya unyenyekevu, katika mambo yote.
“Na ninatoa ahadi hii kwenu, ya kuwa alimradi mtayatenda haya Roho Mtakatifu atamwagwa katika kutoa ushuhuda kwa mambo yote mtakayosema ninyi.” (Mafundisho na Maagano 100:5–8).
Baraka Kusonga Mbele
Wapendwa marafiki zangu wadogo, kutakuwa na changamoto siku za mbele, bali maisha yenu hatimaye yatakwenda kuwa mazuri kabisa mnapotoa moyo wenu kwa Mungu, mnapompenda Bwana Yesu Kristo, na kujitahidi kwa uwezo wenu wote kuishi injili. Kama wewe ni mwaminifu, Sayuni itakuwa popote pale ulipo. Ninawabariki muikumbatie kwa furaha. Bwana ana mengi mno yaliyohifadhiwa kwa ajili yenu!