2021
Sikutengeneza Timu ya Dansi
Septemba 2021


“Sikuwa kwenye Timu ya Dansi,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2021, 10-11.

Sikuwa kwenye Timu ya Dansi

Jina langu halikuwepo kwenye orodha. Nilikuwa nimekatishwa tamaa. Lakini Bwana alinifundisha kitu fulani.

Picha
Wachezaji wa dansi

Vielelezo na Gabriele Cracolici

Nimependa kucheza dansi tangu nilipokuwa na umri wa miaka mitatu. Kwa hiyo nilipokuwa shule ya kati, nilisisimka wakati majaribio kwa ajili ya timu ya dansi yalipowadia. Sikuwa na wasiwasi na kipaji changu na uzoefu, nigeweza kirahisi kuwemo katika timu.

Siku chache baada ya majaribio, majina ya timu ya dansi yalibandikwa. Kwa mfadhaiko, sikuweza kuliona jina langu popote kwenye orodha. Nilikuwa nimekatishwa tamaa. Nilikwenda nyumbani na nililia kwenye kitanda changu. Nilikasirishwa sana na mwalimu wa dansi na kukatishwa tamaa kwamba sikuwa mzuri vya kutosha kuwemo ndani ya timu. Mama yangu pole pole aliingia kwenye chumba changu na kupendekeza kwamba nimwombe Baba wa Mbinguni kwa ajili ya nguvu za kuniwezesha kupita “tuta” hili katika maisha yangu. Kwa kusita nilikubali na kusali sala fupi. Baada ya sala sikujihisi vizuri, kwa hiyo niliendelea kuzunguka zunguka pande zote na kuwa mnyonge. Nililala vibaya usiku ule.

Asubuhi iliyofuata niliamka kivivu na kutoka kitandani. Kumbukumbu ya kushindwa kwangu ilikuwa mpya akilini mwangu, na nilitaka kurudi tena na kujifunika na shuka langu. Lakini kabla sijafanya hivyo, nilikumbuka ahadi askofu wangu aliyoitoa. Alisema kwamba kama ningesoma maandiko yangu kila siku, hata kama kwa dakika 15 tu, basi ningebarikiwa. Kama kwa wakati wowote nilihitaji baraka, ilikuwa sasa.

Nilipokuwa nasoma, niligundua mstari huu katika Mafundisho na Maagano:

“Ninawaambia marafiki zangu, msiogope, mioyo yenu na ifarijike; ndiyo, furahini siku zote, na toeni shukrani katika kila kitu;

“Mkimngoja Bwana kwa subira, kwani sala zenu zimeingia masikioni mwa Bwana wa Sabato, na zimeandikwa kwa muhuri na ushuhuda huu—Bwana ameapa na kutangaza kuwa atatoa.

“Kwa hiyo, yeye hutoa ahadi hii kwenu, kwa ahadi isiyobadilika kwamba zitatimizwa; na mambo yote ambayo kwayo mmeteswa yatafanya kazi kwa pamoja kwa faida yenu, na kwa utukufu wa jina langu, asema Bwana” (Mafundisho na Maagano 98:1-3)).

Nilishtuka. Nilikaa nikiwa kwenye nguo zangu za kulalia pamoja na nywele zangu zilizovurugika nikishangazwa kwa kiasi gani nilihitaji maandiko haya. Hisia zote za hasira na huzuni ziliondolewa katika mistari hiyo mitatu. Nilihisi upendo wa Baba yangu wa Mbinguni na nilijua kwamba alijua kile nilichokuwa napitia. Kwa mtizamo huu mpya, niliweza kuona kwamba kutokuchaguliwa kwa ajili ya timu ya dansi kwa kweli kulikuwa tuta dogo tu katika barabara ya maisha yangu. Nilipiga magoti kwa shukrani na nilimshukuru Baba wa Mbinguni.

Kwa siku nzima, Niliweza kumweka Roho pamoja nami na kuangalia majaribu yangu kama fursa kwa ajili ya ukuaji. Siku zote nitaishika mistari hii karibu na moyo wangu. Na nitakumbuka ahadi ya askofu wangu kuhusu baraka za kugeukia kwenye maandiko. Nina shukrani kubwa ninaweza kuwa sehemu ya Kanisa hili na kuwa na uelewa wa injili. Ninajua kwamba mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yetu kwa kweli ni mpango wa furaha.

Chapisha