2021
Ninawezaje kubakia kwenye viwango kwa ajili ya mahusiano?
Septemba 2021


Inaonekana vigumu kubakia kwenye viwango wakati kila ninaye mjua yuko katika mahusiano ya kina na mtu fulani Je, napaswa kufanya nini? Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Feb 2021, 9.

Maswali na Majibu

Inaonekana vigumu kubakia kwenye viwango wakati kila ninaye mjua yuko katika mahusiano ya kina na mtu fulani Je, napaswa kufanya nini?

Kujiendeleza

Picha
msichana

“Jaribu kuwa na taswira ya milele na tumia muda kuendeleza kwa kina mahusiano na familia yako na marafiki. Mipangilio hii yenye siha itawavutia wengine kwako kwa sababu wataona uzuri wako—jinsi ulivyo!”

Ellie S.,17, California, Marekani

Tafuta Mwongozo

Picha
mvulana

“Kama unapambana na hisia za kutojaliwa, mwombe Baba wa Mbinguni kwa ajili ya faraja. Roho Mtakatifu atakuongoza na kuwa pale kwa ajili yako. Pia, unaweza kila siku kuwaomba wazazi wako na viongozi kwa ajili ya ushauri, kwa sababu wamewahi kuwa pale ulipo!”

Jaime G., 17, Nuevo Casas Grandes, Mexico

Tengeneza Marafiki Wapya

Picha
msichana

Ninajikumbusha mwenyewe kwamba Mungu ananipenda. Kisha nitachukua fursa kuwasiliana na marafiki wa zamani, na nitaanzisha shughuli kuwapata marafiki wapya. Unaweza kutumia wakati huu kujenga matumaini, vipaji na ushuhuda wako, na itawezekana.”

Julia S., 12, Alberta, Kanada

Ushauri wa Manabii

Picha
msichana

“Inaweza kuwa vigumu kufikiri kuhusu milele wakati ‘sasa hivi’ inaonekana muhimu zaidi. Kumbuka kwamba manabii na viongozi wengine wa Kanisa wameshauri kwa uthabiti dhidi ya kuwa na mahusiano katika miaka yako ya ujana, hata baada ya umri wa miaka 16. Mahusiano ya kina wakati ukiwa mdogo yanaweza kusababisha kuvunjika moyo na ukosefu wa maadili. Unaweza pia kumwomba Baba wa Mbinguni kuhusu nini kingekuwa kilicho bora kwako kufanya.

Julia C.,17, Utah, Marekani

Jihusishe

Picha
msichana

“Njia nzuri ya kuhisi kujumuishwa ni kujihusisha katika vitu vingine. Jaribu mchezo mpya, kuigiza kwa ajili ya mchezo wa shule, au jiunge na klabu ya kujifunza kuhusu maroboti. Ikiwa unafanya kitu unachokipenda, utakutana na watu unaopenda kuwa karibu nao.”

Mayah S., 16, Beijing, China

Ni Uchaguzi Wako

“Kama tayari una umri wa miaka 16, unaweza kuchagua kama unataka kwenda miadi na mtu mmoja pekee kwa wakati. Lakini wakati unafanya uchaguzi huo, usifikirie kuhusu nini wengine wangeweza kufikiri juu yako. Kama unajiona upo tayari, basi fanya hivyo. Kama haupo tayari, usifanye.”

Felipe M., 14, Rio de Janero, Brazil

Mahusiano Mengine Muhimu

“Hata kama hautaweza kuwa katika mahusiano na ‘mwingine,’ bado una mahusiano mazuri na marafiki na familia inayokuzunguka. Uwe mwenye shukrani kwa ajili ya mahusiano hayo. Ili kuwaimarisha, kuwa kama Kristo na mfano mzuri.”

Taylee L.,17, Utah, Marekani

Subiri Kutengeneza Mahusiano ya Kina

“Ninapenda bado kutokuwa katika mahusiano. Baadhi ya marafiki zetu hawatakuwa nami kwa sababu wanatumia muda wao wote na marafiki zao wa kiume. Najihisi kama nipo huru kukutana na watu bila kufanya maamuzi muhimu mapema mno.”

Gina C., 16, Nuevo Casas Grandes, Mexico

Usijisumbue mwenyewe.

Nimehisi hisia zilezile, lakini kumuomba Mungu, kusoma maandiko, na kuzungumza na wazazi wangu kumenisaidia. Hatuhitaji kuhisi kushinikizwa, kwa sababu Bwana atatusaidia kujua wakati gani ni muda sahihi. Furahia maisha yako, na tumia muda na marafiki na familia wakati ukiwa kijana! Kipindi hiki cha maisha yetu kinatokea mara moja tu, kwa hiyo usihisi kushinikizwa kuya harakisha.”

Victoria G., 16, Nuevo Casas Grandes, Mexico

Chapisha