2021
Kujijenga Vyema Mwenyewe
Septemba 2021


“Kujijenga Vyema Mwenyewe,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2021, 6-7.

Njoo, Unifuate

Kujijenga Vyema Mwenyewe

Njia tano zakujenga maisha ya furaha na yenye shangwe.

Mafundisho na Maagano 95:13-14

Eksirei ya msichana, ramani ya hekalu

Vielelezo na Juliet Percival

Wakati Bwana alipomwamuru Joseph Smith kujenga hekalu la Kirtland, Hakumwacha afikirie jinsi ya kufanya vyote yeye peke yake. Alimwonyesha ramani ya jengo ambayo ingeelekeza kwenye mafanikio.

“Acha nyumba ijengwe, siyo kwa jinsi ya ulimwengu,” Bwana alitangaza. “Acha ijengwe kwa jinsi ambayo nitaionyesha” (Mafundisho na Maagano 95:13–14.); Bwana kisha alitoa maelekezo juu ya jinsi ya kulijenga hekalu (ona Mafundisho na Maagano 95:15–17).

Kwa shukrani, Bwana ametuonyesha zaidi kuliko jinsi tu ya kujenga mahekalu. Pia ametupa maelekezo kutusaidia kuwa watu wema kadiri tuwezavyo. Tunapoyafuata, tutajenga maisha yetu “si kulingana na jinsi ya ulimwengu” bali kulingana na jinsi Bwana alivyoyasanifu.

Hizi hapa ni njia tano za kujenga maisha ya furaha na yenye shangwe yenye kiini chake kwa Yesu Kristo.

Jenga Msingi wa Uhakika

Msanifu yoyote wa majengo au mjenzi atakuambia kwamba msingi imara ni muhimu kwa jengo lolote. Helamani alifundisha kwamba msingi mzuri sana kwa ajili ya maisha yetu ni “mwamba wa Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu” (Helamani 5:12). Tunaweza kumfanya Kristo msingi wetu kwa kwenda Kwake na kufuata mafundisho Yake. Unahisi unaendelea vipi katika kumfanya Kristo msingi wa maisha ako?

Hudumia wengine

Miguu

Njia nyingine kuu ya kuyajenga maisha yetu, kufuatana na Rais Dieter F. Uchtdorf, wakati huo akiwa Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, huja wakati “tumesimama kumhudumia Bwana na kuwahudumia wale wanaotuzunguka.”1 Wakati unapowahudumia wengine, unafanya kile Yesu alichokifanya na kujifunza kuwa zaidi kama Yeye. Na hutabariki maisha ya watu unaowahudumia pekee, bali wewe utabarikiwa vilevile.

Tengeneza utaratibu wa kawaida wa Sala na kujifunza maandiko

mikono ya sala

Njia nyingine ya kujenga maisha ya furaha ni kujenga mahusiano na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Njia kuu ya kufanya hivyo ni kupitia sala na kujifunza maandiko.

Rais Uchtdorf alisema: “Kuimarisha mahusiano yetu na Mungu, tunahitaji muda kiasi wenye maana peke yetu na Yeye. Kwa ukimya tukifokasi kwenye sala binafsi ya kila siku na kujifunza maandiko… itakuwa uwekezaji wa busara wa muda wetu na juhudi zetu kumkaribia zaidi Baba yetu wa Mbinguni.”2

Sala ni fursa ya kuwasiliana na Baba yetu wa Mbinguni. Anatujua, anatupenda, na anataka kusikia toka kwetu! Wakati tunaposali kwa dhati, tukitoa shukrani zetu, na kuomba vitu tunavyohitaji, Yeye anasikiliza na siku zote anajibu kwa njia na wakati wake.

Kuhusu kujifunza maandiko , hakuna njia moja sahihi ya kufanya hivyo. Kitu cha muhimu ni kwamba unafanya hivyo! Rais Russell M. Nelson amefundisha, “Tafakari ya kila siku katika neno la Mungu ni muhimu sana kwa ajili ya kupona kiroho.”3 Kutumia muda kila siku katika maandiko kutaweza, bila wasiwasi, kukusaidia kujenga maisha ya imani na nguvu.

Changamana na Wale Wanaokutia Moyo Kufanya Mema

Mvulana na mikono iliyonyooshwa

Baba wa Mbinguni anatutaka tuunganishe na kujenga mahusiano na wengine—hususani familia na marafiki. Mara kwa mara tunatengenezwa kupitia wale tunaokuwa pamoja nao. Iwe ni waumini wa Kanisa au la, unapaswa kuchangamana na watu wanaokusaidia kuishi injili, kushika viwango vya Bwana, na kuwa mtu mwema zaidi. Unaweza pia kuwasaidia wale wanaokuzunguka kufanya vivyo hivyo. Yupi kati ya rafiki zako anakusaidia kujenga msingi wako juu ya haki?

Pata furaha katika Kujenga Msingi Wako

Kuna njia nyingine nyingi unazoweza kujenga maisha yako yawe imara kiroho na kuwa na furaha, ikijumuisha kwenda kanisani na kushiriki sakramenti, kufanya na kutunza maagano, na kufuata ushauri wa manabii wanaoishi.

Ni muhimu kukumbuka kwamba vyote hivi vinahitaji kazi na muda. Mara zote kuna kujenga na kujifunza kunakofanyika, lakini huna haja ya kufanya hili peke yako. Bwana atakusaidia kila siku unapojaribu kwa uwezo wako wote kujenga maisha ambayo wewe na Yeye mnaweza kujivunia na kwamba utapata furaha.