2021
Chaguzi
Septemba 2021


“Chaguzi,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2021, 12-14.

Chaguzi

Picha
Mbwa mwitu

Picha kutoka Getty Images

Miaka mingi iliyopita, mmoja kati ya Viongozi wetu Wakuu wenye Mamlaka alishiriki hadithi hii yenye changamoto:

Cherokee mwenye busara, mmoja wa makabila ya asili huko Marekani, alimweleza mjukuu wake hadithi ya mafumbo kuhusu maisha. “Ndani yangu mimi kuna ugomvi wa kutisha kati ya mbwa mwitu wawili,” babu alisema. “Mmoja ni muovu: amejawa na hasira na wivu, kujihurumia,na huzuni, ulafi na uongo. Mwingine ni mwema: amejaa upole na huruma , unyenyekevu na ukweli, upendo na furaha. Ugomvi unaendelea ndani ya kila mmoja wetu.”

“Mbwa mwitu gani atashinda?” mjukuu aliuliza.

“Yule unaemlisha”, babu kwa busara alimjibu.1

Hadithi hii ya mafumbo ya mbwa mwitu wawili inaonesha ukweli wa milele. Watoto wa Mungu wanazaliwa kufanya chaguzi kati ya mema na uovu. Upinzani unaturuhusu kufanya chaguzi za maana, na za haki. Kitabu cha Mormoni kinafundisha ukweli huu ndani ya lugha ya kimaandiko: “Kwani lazima, kuwe na upinzani katika vitu vyote,”2

Mpango wa Baba Yetu wa Mbinguni unatoa angalau karama hizi kusaidia katika chaguzi hizi: (1) Anatupa sisi Roho Mtakatifu kuongoza chaguzi zetu, na (2) anatupa sisi Mwokozi ambaye Upatanisho wake unafanya kuwezekana kwa toba yetu kuondoa athari za chaguzi mbaya —wakati wamemlisha mbwa mwitu muovu.

Picha
Yesu Kristo

1.Toba na Utambuzi

Kama nilivyozungumza kwa vijana, moja ya masomo wanayouliza mara kwa mara mno ni toba. “Jinsi gani unaweza kujua wakati ambapo umefanya toba vya kutosha?” “Jinsi gani unaweza kujua wakati ambapo kwa dhati umesamehewa?” Majibu kwa maswali haya yanakuja kupitia Roho Mtakatifu, mshirika wa Uungu ambaye analeta jumbe kutoka mbinguni.

Karama ya toba imeitwa “habari njema ya injili.”3 Inaturuhusu kufuta athari za chaguzi ovu ambazo zilimlisha mbwa mwitu na kudhoofisha uwezo wetu wa kusikia ushawishi wa Roho Mtakatifu. Toba inajumuisha kutambua kwamba tumefanya makosa, kutupilia mbali makosa yale, na kuamua kuugeuza moyo kwa Mungu na kutii amri zake. Wakati tunapo tubu, tunaweza kuomba msaada wa nguvu za Upatanisho wa Yesu Kristo, ambazo zinaongeza shukrani zetu na upendo kwa ajili Yake kama Mwokozi wetu.

Hitaji kwa ajili ya toba halina kikomo kwa dhambi kubwa ambazo zinahitaji kuungamwa kwa askofu. Toba ni hitaji la kila siku. Toba nyingi zinajumuisha utambuzi binafsi kuwa tumekosea, kuamua kubadilika, na kujaribu kurekebisha pale tulipowakosea wengine. Kwa maudhui ya fumbo la mbwa mwitu wawili, toba inahusiana na kuacha kumlisha mbwa mwitu muovu hata milo midogo, kama vile wakati tunapochagua kuwa na hasira au wivu. Pia tunahitaji kutubu (kubadilika) wakati tumechagua kupoteza bure muda tuliopewa na Mungu kwenye baadhi ya shughuli nyingi zilizopo ambazo hazina uwezo wa kutufanya wema zaidi.

II. Kutambua Tofauti Muhimu

Matokeo mazuri ya toba ni kuimarisha ustahiki wetu wa kupokea hisia kutoka kwa Roho Mtakatifu, ambaye hutusaidia kufanya uchaguzi wa busara na kutujaza furaha. Vijana wengi pia wanastaajabu: Ninajuaje kama ushawishi au jibu ambalo ninalipata kwa kweli limetoka kwa Bwana na sio tu kile Mimi ninachokitaka?”

Kutambua kama ushawishi ni ujumbe kutoka kwa Roho Mtakatifu au matamanio binafsi, tunahitaji kutumia kweli tatu.

  1. Katika ibada ya sakramenti, ahadi kwamba daima “tutakuwa na Roho wake pamoja [nasi]” inafuatia ahadi yetu kwamba tutajichukulia jina lake juu yetu, na daima kumkumbuka Yeye, na kutii amri Zake.4 Wakati tukishindwa kuweka ahadi hizi, tupo kwenye hatari ya kuchanganya chanzo cha ushawishi cha msukumo tunaohisi.

  2. Ushawishi kutoka kwa Bwana kawaida hupokelewa wakati wa utulivu au katikati ya ibada, kusoma maandiko, au maombi au wakati wa huduma katika wito wetu, sio katika harakati za ubinafsi au wakati umezungukwa na shughuli za ulimwengu.

  3. Mwishowe, tunahitaji kuwa hususani wepesi kuhisi mwelekeo ili kubadili njia ambayo tayari tumeichukua. Msukumo wa kubadili njia unaweza kuwa wa kuaminika zaidi kuliko msukumo wa kuendelea na kitu fulani ambacho tayari tunataka kufanya.

III. Sahihi bado ni Sahihi

Wapendwa marafiki zangu vijana, mnakuja kwenye kupevuka katika ulimwengu tofauti sana kuliko wazazi na mababu zenu waliouzoea. Hivyo inafanya hususani muhimu kwa ajili yenu kukumbuka kwamba maadili ya kale na amri bado zinatumika. Sisi ni watoto wa Mungu, na amri Zake zinabaki muhimu, iwe tunasafiri na gari la mkokoteni au chombo cha anga, ama tunawasiliana kwa sauti au kwa maandishi.

Sahihi bado ni sahihi, na isiyo sahihi si sahihi, bila kujali nini kimesemwa au kufanywa na wacheza sinema, watangazaji wa TV, au wanamichezo maarufu. Viwango katika maandiko, mafundisho ya manabii wanaoishi, na maadili katika kijitabu cha Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana bado ni mwongozo wako mzuri mno kwa ajili ya chaguzi binafsi katika usafi wa kimwili, afya ya mwili, uaminifu, mavazi na mwonekano, na mambo yake mengine. Yafuate kwa imani, na utabarikiwa. “Kijitabu kiitwacho Kwa ajili ya nguvu kwa Vijana kinapaswa kuwa kiwango chako,” Rais Russell M. Nelson alitufundisha. “Ni kiwango ambacho Bwana anategemea vijana wake wote kutetea.”5

Katika ibada hii ya vijana ulimwenguni kote, nabii wetu aliahidi:

“Kama mtafanya kwa dhati na kuendelea kushikilia kufanya kazi ya kiroho inayohitajika kuendeleza umahiri wa kiroho wa kujifunza jinsi ya kusikia minon’gono ya Roho Mtakatifu, utapata maelekezo yote utakayohitaji katika maisha yako. Utapewa majibu ya maswali yako katika njia yake Bwana mwenyewe na muda Wake mwenyewe.”6

Ninaunganisha ahadi zangu kwenye Zake, ninaposhuhudia juu ya Mwokozi wetu, ambaye mafundisho Yake na Upatanisho yanafanya yote yawezekane katika jina la Jesu Kristo, Amina.

  1. Ona Shayne M. Bowen, “Agency And Accountability,” New Era, Sept. 2021, 8.

  2. 2 Nefi 2:11.

  3. Dale G. Renlund, mkutano mkuu wa Oktoba 2016 (Ensign au Liahona, Novemba 2016, 124).

  4. Mafundisho na Maagano 20:77.

  5. Russell M. Nelson, “Tumaini la Israeli” ( ibada ya vijana kote ulimwenguni, Juni 3, 2018), 16, HopeofIsrael.ChurchofJesusChrist.org.

  6. Russell M. Nelson, “Tumaini la Israeli,” 3.

Chapisha