2021
Kuijenga Sayuni kupitia Umoja
Septemba 2021


“Kujenga Sayuni kupitia umoja,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2021, 20.

Neno la Mwisho

Kuijenga Sayuni kupitia Umoja

Imetokana na hotuba ya mkutano mkuu wa Oktoba 2008.

Sayuni ni vyote mahali na Watu. Sayuni lilikuwa jina lililotolewa kwa jiji la kale la Henoko. Bwana akawaita watu wa Henoko Sayuni “kwa sababu walikuwa wa moyo mmoja na wazo moja, na waliishi katika haki; na hapakuwa na maskini miongoni mwao’ (Musa 7:18). Mahali pengine Alisema, “Kwani hii ni Sayuni—walio safi moyoni” (Mafundisho na Maagano 97:21).

Kuanzisha Sayuni majumbani mwetu, matawi, kata, na vigingi, tunahitaji (1) kuwa tulioungana katika moya mmoja na wazo moja; (2) kuwa watu watakatifu; na (3) kuwajali maskini na wenye mahitaji. Hatuwezi kusubiri mpaka Sayuni ije kwa vitu hivi kutokea—Sayuni itakuja tu ikiwa vitafanyika.

Tutakuwa wa moyo mmoja na wazo moja wakati sisi binafsi tunapomweka mwokozi katikati ya maisha yetu, kuwafuata wale aliowaidhinisha kutuongoza, na kuungana katika upendo na kujaliana. Umoja huu na upendo kwa kila mmoja wetu, vikizidishwa mara elfu katika njia tofauti, “italeta tena Sayuni” (Isaya 52:8).

Picha
Mwonekano wa mitaa ya jiji kutoka juu

Kielelezo na Alberto Pinilla

Chapisha