“Jaribu la Imani,” Kwa ajili ya Nguvu ya Vijana, Sept. 2021, 18-19. Njoo, Unifuate Jaribu la Imani Imeandikwa na Eric B. Murdock Vielelezo na Darren Rawlings Mafundisho na Maagano 102–105 1833 Jimbo la Jackson, Missouri, MAREKANI. Kundi la Majambazi liliwalazimisha Watakatifu waliokuwa wanaishi pale kuziacha nyumba zao. Joseph Smith alijiuliza afanye nini. Mara ufunuo ulikuja. Joseph aliambiwa awaandikishe wanaume kusafari kwenda Missouri na kuwasaidia Watakatifu kurudisha nyumba zao. Joseph aliondoka kwenda Missouri pamoja na kundi la watu wa kujitolea. Kundi baadaye liiljulikana kama Kambi ya Sayuni. Safari ilikuwa ngumu wakati mwingine, lakini wengi waliifurahia. Baada ya kutembea mwezi mzima, kambi ilisimama karibu na mto. Walisikia kwamba wanaume upande mwingine walikuwa wanawasubiri kuwashambulia Tutafanya nini? Tulia … … Na uuone wokovu wa Mungu. Mara tufani ilikuja. Mungu yupo katika tufani hii. Mvua ilisababisha mto kujaa sana kiasi kwamba maadui wasingeweza kuuvuka. Baada ya siku chache, Joseph alipokea ufunuo kwamba ulikuwa muda wa kurudi nyumbani, japokuwa hawakuwasaidia watakatifu wa Missouri kurudi kwenye nyumba zao. Bwana amekubali juhudi zetu. Tumefikishwa hapa tulipo kwa sababu ya jaribu la imani yetu. (Ona Mafundisho na Maagano 105:19.) Baadhi walifikiri safari ilishindwa. Tulikuja njia yote hii bila maana yoyote! Kwa nini tunakwenda nyumbani kabla ya kuwasaidia Watakatifu hapa? Wengi waliiona kama heshima kuwa na Nabii na kujifunza kutoka kwake. Kambi ya Sayuni ilisaidia kuwaanda viongozi wa baadaye wa Kanisa. Wanaume wanane waliotembea pamoja na Kambi ya Sayuni waliitwa kwenye Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.