2021
Mungu Atapigana Vita Vyenu—kwa Njia Yake
Septemba 2021


“Mungu atapigana Vita Vyenu—kwa Njia Yake,” Kwa ajili ya Nguvu kwaa Vijana, Sept. 2021, 15-17.

Njoo, Unifuate

Mungu Atapigana Vita Vyenu—kwa Njia Yake

Watakatifu wa mwanzo walijifunza kitu kimoja au viwili kuhusu njia za Mungu.

Mafundisho na Maagano 103-105

Picha
Kambi ya Sayuni kwenye Fishing River

Kambi ya Sayuni na Judith Mehr

Pamoja na kundi la majambazi zaidi ya 300 lenye hasira likiahidi kuwaangamiza asubuhi, kundi la Watakatifu walioifanya kambi ya Sayuni lilikuwa likitegemea na kuomba kwa ajili ya muujiza.

Chini ya uongozi wa Joseph Smith, Kambi ya Sayuni imekuwa ikitembea kwa wiki kadhaa kutoka Ohio kwenda Missouri. Waumini hawa wa Kanisa walikuwa wakitegemea kuwasaidia Watakatifu ambao walikuwa wamefukuzwa kutoka jimbo la Jackson, Missouri, Marekani kuipata tena ardhi yao. Lakini walikumbana na vitisho na upinzani katika mwendo wao wote. Na sasa, bado kundi lingine la majambazi lilikuwa likiwatishia.

Muujiza ambao Kambi ya watakatifu ya Sayuni iliomba kwa ajili yao ungewasili mapema. Ulikuja katika umbo la mawingu mazito meusi yakikusanyika kwa mbali. Mvua ya ngurumo kali ilinyesha pande zote ikiwa ni ya mawe. Dhoruba ilisimamisha kundi la majambazi katika maeneo yao.

“Ilionekana kama vile agizo la kisasi limetokea kutoka kwa Mungu wa vita kuwalinda watumishi wake kutoka kuharibiwa na maadui zao,” historia ya Joseph Smith inaelezea. “Mvua ya mawe iliwanyeshea, na si sisi, na hatukuteseka na madhara yoyote isipokuwa kuangushwa kwa baadhi ya mahema yetu na baadhi kuloa, wakati maadui zetu kwa upande mwingine walipata uharibifu wa kuwa na matundu katika kofia zao na hata kuvunjika kwa vitako vya bunduki zao na kutorokewa na farasi wao.”1

Uhabirifu wa mvua ya mawe ulikuwa tu sehemu moja ya dhoruba. Mvua ilinyesha kwa nguvu kiasi kwamba Fishing River, mto unaotenganisha makundi hayo mawili, ulijaa kina takribani futi 40 (mita 12). Hapo kabla wakati wa asubuhi ile ulikuwa tu usawa wa kifundo cha mguu.

Bwana aliwaahidi washiriki wa Kambi ya Sayuni, “Nitapigana Vita Vyenu” (Mafundisho na Maagano 105:14). Wakati hilo linatokea, hakuna wasiwasi upande gani utashinda.

Miujiza ya siku za leo.

Wakati mwingine unaposoma maelezo kama haya, unaweza kustaajabu kwa nini miujiza ya kuvutia kama hii haionekani kutokea kwenu ninyi katika jitihada zenu.

Mzee JeffreyR. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili hivi karibuni alishiriki tambuzi ambazo zinaweza kukusaidia. Alisema: “Tafadhali fahamuni kwamba Yeye ambaye kamwe halali wala kusinzia anajali furaha na hatimaye kuinuliwa kwa watoto Wake juu ya vitu vingine vyote ambavyo kiumbe mtakatifu atafanya. Yeye ni upendo safi, kiumbe aliyetukuka, na Baba Mwenye Huruma ndilo jina Lake.

“‘Vyema, kama hivyo ndivyo,” ungeweza kusema, “je, kwa nini upendo Wake na rehema Yake visingeigawa Bahari yetu binafsi ya Shamu na kuturuhusu sisi kutembea ili kuvuka matatizo yetu juu ya nchi kavu?’”

Kwa maneno mengine, kama Mungu amepigana vita kama hivyo kwa ajili ya watoto Wake hapo zamani, kwa nini asifanye hivyo sasa? Kwa nini asifute kabisa magonjwa yote? Kwa nini asimalize vita na njaa na mateso kote ulimwenguni?

Au kwa nini angalau asimzuie yule mnyanyasaji ambaye hataki kukuacha? Au kuisaidia familia yako kuelewana vizuri zaidi?

Mzee Holland alifundisha zaidi: “Jibu kwa swali kama hilo ni “Ndiyo, Mungu anaweza kutoa miujiza wakati huo huo, lakini punde au baadae tunajifunza kwamba nyakati na majira ya safari yetu duniani ni Yake na Yake yeye pekee kuongoza.’ Huitawala kalenda ile binafsi ya kila mmoja wetu binafsi.”2

Wakati unapofuata amri za Mungu, unastahili msaada wa Mungu. Lakini hakuna kati yetu anayeweza kuchagua jinsi au wakati msaada ule utakapokuja.

Baraka Zisizotegemewa

Acha turudi kwenye Kambi ya Sayuni kwa muda mfupi. Muujiza kwenye Fishing River ulikuwa kwa hakika wa kuvutia. Na haukuwa muujiza pekee washiriki wa Kambi ya Sayuni waliuona wakati wa matembezi yao. Lakini utakapokuwa unasoma katika Njoo, Unifuate na kujifunza katika seminari mwezi huu, vitu havikuwa jinsi ambavyo Watakatifu walikuwa wamepanga.

Walifikiri sababu kamili ya Kambi ya Sayuni ilikuwa kusaidia kurudisha ardhi katika jimbo la Jackson ambayo ilikuwa imeporwa kutoka kwa Watakatifu na kundi la majambazi wenye hasira.

Je, Watakatifu waliweza kurudisha ardhi yao? Hapana.

Je Watakatifu waliteseka kwenye mwendo wao kurudi Missouri karibia maili 900 (kilomita 1,448)? Ndiyo. Wakati mwingine kwa wingi. Katika tukio baya kuliko yote, kuzuka kwa kipindupindu katika kambi mzima na kiliua watu13.

Kwa nje, inaweza kuonekana kama juhudi yote ilishindwa Lakini hivyo sivyo wengi waliotembea katika kambi walivyoona. Brigham Young alisema juu ya uzoefu huu, “Nililipwa vizuri—Nililipwa na riba kubwa—ndio … .kipimo changu kilijazwa mpaka kumwagika na uelewa ambao nilikuwa nimepokea kwa kusafiri pamoja na Nabii [Joseph Smith]. ”3

Washirika wengi wa Kambi ya Sayuni pia walizungumza kuhusu masomo yaliyofunzwa na thamani ya kwenda kwao. Nabii Joseph Smith mwenyewe alisema: “Ndugu, baadhi yenu mna hasira na mimi, kwa sababu hamkupigana Missouri; lakini acha niwaambieni, Mungu hakutaka ninyi mpigane. Asingeweza kuratibu ufalme wake … isipokuwa awachukue [viongozi wake] kutoka jamii ya wanaume waliokwisha kutoa maisha yao, na waliokwisha toa dhabihu kubwa kama Ibrahimu alivyofanya.”4

Picha
Kambi ya Sayuni

Kambi ya Sayuni na C.C.A. Christensen

Uaminifu wao unaweza usiwe wa kuleta matokeo ya ardhi yao kurudishwa. Lakini walikuwa wamebarikiwa kwa njia nyingi. Huo ni mpangilio unaoweza kuuona katika maisha yako pia. Na kile Mungu anatusaidia kuwa kupitia majaribu yetu mara nyingi ni muujiza mkubwa kuliko kutukomboa kutoka majaribu yetu.

Ushindi wa Uhakika wa Mungu

Unapojifunza maisha ya Watakatifu wa mwanzo, unaweza kugundua ushawishi wa Mungu mara kwa mara. Unasoma kuhusu baraka kubwa. Pia unaona nyakati za masumbuko makubwa. Lakini kwa wale waliomwamini Mungu mpaka mwisho, zawadi yao ya milele ilikuwa ya uhakika.

Unapomfuata Mungu na kumwamini Yeye, Atapigana vita vyenu na kutoa miujiza unayoihitaji! Miujiza hii itakuja katika njia yake mwenyewe na muda Wake, lakini matokeo ni ya uhakika. Jaribu lolote hatimaye litatatuliwa—katika maisha haya au yajayo. Muhimu, unampomfuata, kamwe hutatembea peke yako. Kwa hiyo, kuweni waaminifu; na tazama, na lo, Mimi nipo pamoja nanyi hadi mwisho” (Mafundisho na Maagano 105:41).

Muhtasari

  1. Historia, 1838–1856, juzuu A-1 [23 Disemba 1805–30 Agosti 1834),” 497, josephsmithpapers.org.

  2. Jeffrey R. Hplland, mkutano mkuu wa Oktoba 2020 (Ensign, au Liahona, Novemba 2020, 116).

  3. “Hotuba” ya Brigham Young, Deseret News, Nov. 3, 1862, 177.

  4. Joseph Smith, katika Joseph Sr., History of the Organization of the Seventies (1878), 14.

Chapisha