“Uongofu Kwenye Mapenzi ya Mungu,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Mei. 2022.
Kikao cha Jumamosi Alasiri
Uongofu Kwenye Mapenzi ya Mungu
Dondoo
Katika huduma ya maisha yote na uzoefu wa kiroho, nimekuja kuelewa kwamba uongofu wa kweli ni matokeo ya kukubali mapenzi ya Mungu kwa kudhamiria na kwamba tunaweza kuongozwa na Roho Mtakatifu katika matendo yetu. …
Je, ni majukumu gani huja kutokana na uongufu? …
… Mwokozi kwa neema anatualika tuwe sauti Yake na mikono Yake. Upendo wa Mwokozi utakuwa nuru yetu ya kuongoza. Mwokozi aliwafundisha wanafunzi Wake, “Enendeni, mkawafundishe mataifa yote.” [Mathayo 28:19]. Na kwa Joseph Smith, Yeye alitamka, “Hubirini injili yangu kwa kila kiumbe ambacho bado hakijaipokea.” [Mafundisho na Maagano 112:28]. …
Ili agizo la Mwokozi la kushiriki injili liwe sehemu ya utu wetu, tunahitaji kuwa waongofu kwenye mapenzi ya Mungu; tunahitaji kuwapenda jirani zetu, kushiriki injili iliyorejeshwa ya Yesu Kristo na kuwaalika wote waje na waone. …
Uongofu wetu binafsi hujumuisha jukumu la kushiriki injili ya Yesu Kristo kwa ulimwengu.
Baraka za kushiriki injili zinajumuisha ongezeko la uongofu wetu kwenye mapenzi ya Mungu na kumuacha Mungu ashinde katika maisha yetu. Tunawabariki wengine kupata “badiliko kuu” la moyo.” [Alma 5:14]. Kuna shangwe ya kweli ya milele katika kusaidia kuleta nafsi kwa Kristo. Kufanyia kazi uongofu wa mtu binafsi na ule wa wengine ni jukumu takatifu.