2022
Kristo Huponya Kile Kilichovunjika
Mei 2021


“Kristo Huponya Kile Kilichovunjika,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.

Kikao cha Jumapili Asubuhi

Kristo Huponya Kile Kilichovunjika

Dondoo

Picha
bango la Yesu Kristo akimkumbatia mtu

Pakua PDF

Picha na Mark Mabry

Tunaweza kujifunza mengi kutoka kwenye maandiko kuhusu jinsi Mwokozi wetu, Yesu Kristo, atakavyotusaidia kwa mafanikio kurekebisha mambo katika maisha yetu ambayo yamevunjika, bila kujali umri wetu. …

Wakati Mwokozi alipokuwa akifundisha hekaluni, mwanamke aliletwa Kwake na waandishi na Mafarisayo. Hatujui hadithi yake kamili, ila tu kwamba alikuwa “aliyefumaniwa katika uzinzi.”[Yohana 8:4]. …

Jibu la Kristo kwa binti huyu wa thamani wa Mungu lilikuwa “Wala mimi sikuhukumu: enenda zako; wala usitende dhambi tena.” [Yohana 8:11]. Jinsi nyingine ya kusema “enenda, wala usitende dhambi tena” inaweza kuwa “nenda ukabadilike.” Mwokozi alikuwa anamualika atubu. …

Bwana anatufundisha kwamba kuwasamehe wengine ni amri ya ulimwengu wote: “Mimi, Bwana, nitamsamehe yule nitakaye kumsamehe, lakini ninyi mnatakiwa kuwasamehe watu wote.”[Mafundisho na Maagano 64:10]. …

Mara nyingi tunajipata wenyewe, kama vile mwombaji kiwete kwenye lango la hekalu, kwa subira—au wakati mwingine bila subira—“[tukimngojea] Bwana.” [Isaya 40:31]. …

Kuonesha imani katika Kristo kunamaanisha kutumainia siyo tu mapenzi ya Mungu bali pia ratiba Yake. Kwa kuwa Yeye anajua hasa kile tunachohitaji na wakati maalum tunapokihitaji. …

… Hakuna kitu chochote maishani mwako ambacho kimevunjika ambacho ni zaidi ya nguvu ya uponyaji, ukombozi na ya kuwezesha ya Yesu Kristo.

Chapisha