2022
Uhusiano Wetu na Mungu
Mei 2021


“Uhusiano Wetu na Mungu,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Nov. 2022.

Kikao cha Jumapili Asubuhi

Uhusiano Wetu na Mungu

Dondoo

bango la mikono ya sala

Pakua PDF

Hatupaswi kufikiri juu ya mpango wa Mungu kama mashine ya kiulimwengu yenye kujiendesha yenyewe ambapo sisi (i) tunachagua baraka tuitakayo, (ii) tunaingiza jumla ya kiasi kinachotakiwa cha kazi njema na (iii) oda yetu mara moja inatoka. …

Toba na utii wetu, dhabihu zetu na matendo yetu mema ni muhimu. Tunataka kuwa miongoni mwa wale ambao walielezewa na Etheri kama “daima wakizidi sana kutenda kazi njema.” [Etheri 12:4]. Lakini siyo sana kwa sababu ya hesabu inayotunzwa katika vitabu vya selestia. Mambo haya ni ya muhimu kwa sababu yanatuingiza sisi katika kazi ya Mungu na ndiyo njia ambayo sisi tunashirikiana na Yeye katika kubadilika kwetu sisi wenyewe kutoka kuwa mwanadamu wa tabia ya asili na kuwa mtakatifu. Kitu ambacho Baba wa Mbinguni anatupatia sisi ni Yeye Mwenyewe na Mwana Wake, uhusiano wa karibu na wa kudumu pamoja Nao kupitia neema na upatanisho wa Yesu Kristo, Mkombozi wetu.

… Baba yetu yuko tayari kumwongoza kila mmoja wetu kwenye njia Yake ya agano kwa hatua zilizosanifiwa kulingana na mahitaji yetu binafsi na kufumwa kwenye mpango Wake kwa ajili ya kilele cha furaha pamoja Naye. …

Hata hivyo, njia hii haiwezi kuwa rahisi kwa yeyote. Kuna kutakaswa kwingi kunakohitajika ili iwe rahisi. …

Kwa hiyo, katikati ya moto huu wa utakasaji, badala ya kumkasirikia Mungu, jisogeze karibu na Mungu. Mlingane Baba katika jina la Mwana. Tembea pamoja Nao katika Roho, siku hadi siku. Waruhusu Wao kadiri muda unavyosonga wadhihirishe uaminifu Wao kwako. Tafuta kwa hakika kuwajua Wao na kwa hakika kujijua wewe mwenyewe. Acha Mungu Ashinde.