2022
Masomo Kisimani
Mei 2021


“Masomo Kisimani,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.

Kikao cha Wanawake

Masomo Kisimani

Dondoo

Picha
bango la njia kando ya eneo lililofunikwa kwa maji

Pakua PDF

Ningependa kushiriki nanyi masomo matatu ninayojifunza kadiri ninavyoendelea kunywa kutoka kwenye kisima cha [Mwokozi] cha “maji ya uhai.” [Yohana 4:10].

Hali zetu zilizopita na za sasa haziamui kesho yetu …

Mfikirie mwanamke kisimani. …

Alikuwa shahidi shujaa, akitangaza kwa watu wa mji wake kwamba Yesu alikuwa Kristo. “Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke” [Yohana 4:39].

Hali zake zilizopita na za sasa hazikuamua kesho yake. Kama yule mwanamke, tunaweza kuchagua kumgeukia Mwokozi leo kwa ajili ya nguvu na uponyaji utakaotusaidia kutimiza yale yote tuliyotumwa kuyatimiza hapa.

Pili: Uwezo Upo Ndani Yetu [Mafundisho na Maagano 58:28] …

Akina dada, uwezo upo ndani yetu wa kutekeleza haki nyingi! …

Tatu: “Kutokana na Mambo Madogo Huja Yale Yaliyo Makuu” (Mafundisho na Maagano 64:33] …

Akina dada, mioyo inaweza kubadilishwa na maisha kubarikiwa pale tunapotoa kiasi kidogo cha chumvi, kijiko cha hamira na mwale wa nuru.

Ninashuhudia kwamba Mwokozi ni chumvi katika maisha yetu, akitualika sisi kuonja shangwe na upendo Wake. Ni Yeye ambaye ni chachu wakati maisha yetu yanapokuwa magumu, akituletea sisi tumaini na kunyanyua mizigo yetu kupitia nguvu Zake zisizo na kifani na upendo wa kuokoa. Yeye ni nuru yetu, akiangazia njia yetu kurudi nyumbani.

Chapisha