“Kuhubiri Injili ya Amani,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.
Kikao cha Jumamosi Asubuhi
Kuhubiri Injili ya Amani
Dondoo
Tangu mkutano uliopita, magumu ulimwenguni yameendelea. Janga la ulimwenguni kote bado linaathiri maisha yetu. Na sasa ulimwengu umekumbwa na mgogoro. …
Akina kaka na akina dada, injili ya Yesu Kristo kamwe haijawahi kuhitajika zaidi kama ilivyo leo. … Ninampenda Bwana Yesu Kristo na kushuhudia kwamba injili Yake ni suluhisho pekee la kudumu la amani. …
… Tuna jukumu takatifu la kushiriki nguvu na amani ya Yesu Kristo kwa wale wote ambao watasikiliza na kuacha Mungu ashinde katika maisha yao.
Kila mtu ambaye ameshafanya maagano na Mungu ameahidi kuwatunza wengine na kuwatumikia wale walio na uhitaji. Tunaweza kuonesha imani katika Mungu na daima kuwa tayari kutoa jibu kwa wale wanaouliza kuhusu “tumaini lililo ndani [yetu]” [1 Petro 3:15]. …
Leo, ninahakikisha kwa dhati kwamba Bwana ameamuru kila mvulana mwenye kustahili, anayeweza ajiandae kwa ajili ya na kutumikia misheni. …
Kwenu ninyi akina dada mnaoweza, misheni pia ni kitu chenye nguvu, lakini ni fursa isiyo ya lazima, kwenu. …
… Pia tunawaalika wanandoa wazee kutumikia wakati hali zao zinaporuhusu. …
Wamisionari wote wanafundisha na kushuhudia juu ya Mwokozi. Giza la kiroho katika ulimwengu hufanya nuru ya Yesu Kristo kuhitajika zaidi kuliko hapo awali. Kila mmoja anastahili fursa ya kujua kuhusu injili ya urejesho ya Yesu Kristo.