2022
Hisia Zetu Zote za Moyoni
Mei 2021


“Hisia Zetu Zote za Moyoni,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.

Kikao cha Jumapili Alasiri

Hisia Zetu Zote za Moyoni

Dondoo

Picha
bango la senti ya mjane

Pakua PDF

Kuwa mfuasi wa Yesu Kristo siyo tu moja ya vitu vingi tunavyofanya. Mwokozi ndiye nguvu ituhamasishayo nyuma ya vyote tunavyofanya. …

Na vipi kuhusu kazi nyingi na majukumu ambayo hufanya maisha yetu kuwa na shughuli nyingi? …

“Baba yenu wa mbinguni anajua kwamba mna mahitaji ya vitu hivi vyote.

“Lakini utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa.” [3 Nefi 13:32–33; ona pia Mathayo 6:32–33].

Lakini hiyo haimaanishi kwamba ni rahisi. Inahitaji vyote dhabihu na uwekaji wakfu.

Inahitaji kuachilia baadhi ya vitu viondoke na kuruhusu baadhi ya vitu vikue.

… Kutoa dhabihu inamaana kuachana na kitu fulani kwa ajili ya kitu kingine chenye thamani kubwa zaidi. …

Uwekaji Wakfu ni tofauti na dhabihu kwa angalau njia moja muhimu. Wakati tunapoweka wakfu kitu, hatukiachi ili kiliwe madhabahuni. Badala yake, tunakiweka kitumike katika huduma ya Bwana. Tunakitoa kwa dhati kwa Bwana na makusudi Yake matakatifu. …

Tunapotazama maisha yetu na kuona mamia ya mambo ya kufanya, tunahisi kuzidiwa. Tunapoona jambo moja—kumpenda na kumtumikia Mungu na watoto Wake, katika njia mia moja tofauti—ndipo tunaweza kufanyia kazi mambo hayo kwa shangwe.

Hivi ndivyo tunavyotoa nafsi zetu zote—kwa kutoa dhabihu kitu chochote kinachotuzuia sisi na kuweka wakfu vinavyobakia kwa Bwana na makusudi Yake.

Chapisha